Sera ya Rais Mwinyi ya Uchumi wa Bahari " Blue Economy" ni alama ya ukombozi kwa wanyonge kiuchumi

Deogratias Mutungi

Senior Member
Oct 1, 2019
137
178
Salaam Wana JF.

Wakati wa kipindi cha kampeni Rais wa sasa wa Zanzibar aliongelea kwa kina maono yake na mtazamo wake juu ya uchumi wa baharini yaani "blue Economy" bila shaka hii ilikuwa ni ahadi nzuri na sera yenye mantiki katika kukuza uchumi wa watu wa Zanzibar hasa wanyonge, kwa maana kuwa itawezesha kuvuna rasilimali za baharini na kuongeza pato la wavuvi.

Aidha kupitia sera hii ya Rais Mwinyi juu ya uchumi wa baharini inalenga kulinda rasilimali za baharini kwa kizazi cha sasa na hapo badae, ni wazo la kizalendo ambalo viongozi wengi Afrika na dunia kwa ujumla wake wameshindwa kulitekeleza ipasavyo na badala yake tumekuwa tukiona athari cha uchafuzi wa mazingira ambazo ni hatari kwa nchi zinazoendelea kama Zanzibar.

Endapo Rais Mwinyi atatekeleza ipasavyo sera hii ya uchumi wa bahari kama inavyotakiwa bila shaka tutegemee mambo makubwa ikiwa ni pamoja na miradi mikubwa ya uhifadhi wa mikoko ambayo itasaidia kupambana na mabadiliko ya tabia nchi na gesi za viwandani hususani carbon dioxide, aidha uwepo wa misitu utasaidia samaki kupata maeneo ya kutagia mayai ikiwa ni pamoja na ardhi iliyo karibu kusombwa na maji.

Kwa nukta hiyo Wanazanzibar wakae mkao wa kula na wajivunie kuwa na viongozi wenye mawazo chanya yanayofikri katika uratibu wa ukombozi hasa wa jamii za watu walio wanyonge na si viongozi wanaofikri katika kujilimbikizia mali, Huu ndio uongozi unao hitajika katika mataifa yanayoendelea hapa Afrika na si vinginevyo.

Baada ya muhtasari huo mfupi juu ya uchumi wa bahari niwatakie wikendi njema na maandalizi mema ya sikukuu ya Christmas.
 
Mbona unasifia mapema sana sera tu ambayo ni maneno matupu kabla ya utekelezaji!

Na hata nukta zako hujazichambua vizuri, katika hiyo unayoita "uchumi bahari" umejikita kwenye uvuvi tu.

Misitu sijui mikoko, na utagaji wa samaki... huu ni mzaha si mzaha!
 
Mbona unasifia mapema sana sera tu ambayo ni maneno matupu kabla ya utekelezaji!

Na hata nukta zako hujazichambua vizuri, katika hiyo unayoita "uchumi bahari" umejikita kwenye uvuvi tu.

Misitu sijui mikoko, na utagaji wa samaki... huu ni mzaha si mzaha!
in( kigwangala voice)
 
Back
Top Bottom