Uchaguzi 2020 Sera ya majimbo sio ya CHADEMA, ilipendekezwa kwenye rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba

Subira the princess

JF-Expert Member
Mar 3, 2018
2,424
2,587
Wasalaam,

Huwa inashangaza kwa mtu msomi mwenye akili timamu anapoamua kwa makusudi kupotosha jambo lenye maslahi kwa umma, ambalo linatambulika vema kwa jamii husika.

CCM wameparamia kujibu hoja Lissu kuhusu sera ya majimbo eti tutarudi enzi za ukoloni, ukiisoma rasimu ya katiba ya Warioba suala la majimbo limependezwa na viongozi wake wachaguliwe na wananchi wa eneo husika tofauti na sasa ambapo wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa halimashauri wanachaguliwa na MTU mmoja ambae ni mwenyekiti wa CCM.

Lengo la majimbo ni kuepusha matumizi mabaya ya madaraka, upendeleo, ukanda na ukabila na undugu kama inavyotumika leo hii na Chama cha Mapinduzi

Leo hii cheo cha Mkuu wa Mkoa au wilaya ni cheo cha hisani na huruma, ni cheo cha kuhongana na undugu.
Ova.

Maendeleo yana vyama
 
Mzee Warioba bado ninamkubali sana, natamani mara nyingi ajitokeze asimamie na kutetea ukweli aliousimamia kiu ya Watanzania kupata Katiba wanayoihitaji.
 
Lakini pia ikumbukwe hadi kuingizwa kwenye Rasimu ya Warioba mwanzilishi na mtetezi wa sera hiyo ni Chadema ambao walizindua wananchi usingizini long before kabla hata ya Tume ya Warioba kuundwa. At least wapewe credits maana yale "majizi" kadiri sera hii inavyopata nguvu yatakuja kuigeuza yao kujizolea kura.
 
Mzee Warioba bado ninamkubali sana, natamani mara nyingi ajitokeze asimamie na kutetea ukweli aliousimamia kiu ya Watanzania kupata Katiba wanayoihitaji.
Akisindikizwa na Prof. Kabudi.
 
Mzee Warioba bado ninamkubali sana , natamani mara nyingi ajitokeze asimamie na kutetea ukweli aliousimamia kiu ya Watanzania kupata Katiba wanayoihitaji.
Aliambulia kupigwa na kijana anayeweza kuwa mjukuu wake.

Makonda alimzaba makofi mzee wetu hadharani hadi IQ ya mzee ikarudi kama ya makada wenzake.
 
Nilianza kuisikia kwa Mbowe mwaka 2005 alipogombea uRais. Katiba ya Warioba Ni ya mwaka 2014.

Labda kama 2005 hukufuatilia kampeni.
Hakuna jipya chini ya jua. Ni mwendelezo na maboresho ya mifumo bora.
 
Pole pole ndiyo anamuingiza jiwe chaka maana Pole pole naye alishiriki kwenye hiyo tume
 
Mbali na kwenye Rasimu ya Warioba, sera hii pia aliinadi Mbowe wakati akigombea urais 2005 ilikuwepo kwenye ilani ya Chadema kipindi hicho.

All in all ni sera nzuri inayo rejesha mamlaka kwa wananchi kuchagua viongozi wanao wataka na kujiwekea utaratibu wa namna ya kuendesha serikali ya jimbo lao kulingana na fursa na rasilimali za eneo husika katika kujiletea maendeleo.

Ccm lazima waipinge kwa sababu itaondoa utawala unao wafavor kama vile MaDc, MaRc, wakurugenzi nk ambao huteuliwa na rais na ndio wanatumika kuibeba ibaki madarakani pamoja na kuwa imechokwa kila kona.
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom