Sera ya Kilimo kwanza nini msingi wake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sera ya Kilimo kwanza nini msingi wake?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nemesis, Sep 8, 2009.

 1. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Chama cha Mapinduzi (CCM), Serikali yake na watendaji wa umma (civil servants) wanatangaza na kuhamasisha sera/kauli mbiu mpya ya KILIMO KWANZA. Taifa letu limepita katika vipindi mbalimbali vilivyopelekea kutungwa kwa sera/kaulimbiu kadhaa. Mfano Siasa ni kilimo, Kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa nk. Kauli hizo zilikuwa na mwanzilishi, msingi na msukumo wake japo hazikufanikiwa.

  Hii kauli ya sasa, imeanza ghafla, ni kama mtu ametoka usingizini na kutoa kauli ndipo Serikali na CCM wakapanga siku ya kuzindua sera hiyo. Nimekuwa nikifuatilia nini chanzo na msingi wa kauli mbiu hii bila mafanikio. Viongozi wamekuwa wagumu kueleza uwazi wa sera hii.

  Laghaula, leo nimepata kusikiliza kipindi cha MUVIWATA kupitia Radio Maria Tanzania 89.1FM. Kipindi hicho kimejitahidi kuweka wazi kwa sehemu na kujaribu kujibu baadhi ya maswali ya msingi juu ya kaulimbiu au sera hii.

  KILIMO KWANZA ni kauli mbiu iliyoanzishwa na WAFANYABIASHARA ili kutimiza malengo yao ya kibiashara. Kauli hii haikutoka kwa mkulima wala Serikali au viongozi wa kisisa. CCM na Serikali yetu walipoipata hiyo kauli wakaichukua kama kawaida yao, bila hata kuitafakari kwa umakini na kuanza kuihubiri.

  Kutokana na msingi huu, Je sera hii itasaidia kuinua kilimo? Ni nini malengo ya KILIMO KWANZA?

  Naomba wenye taarifa zaidi watusaidie kuweka wazi chanzo, msingi, malengo ya kauli hii. Binafsi nipo very pessimistic kutokana na sababu nilizozitoa hapo juu.
   
 2. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280

  Huu ni usanii mwingine. Haifiki kokote!!! Inahitaji pesa nyingi kutekeleza hizo pillars zao. Je serikali ya awamu ya nne imejiandaa kwa hili??? Kuna programmes nyingi na bado hazijatekelezwa, kwa kukosa funding. Hata development parners were a bit shocked na kuanza kuuliza kama wana acha kutekeleza ASDP (Agricultural Support Development Programme) ambayo wanaifadhili!!! Walitulizwa kuwa KILIMO KWANZA (GREEN REVOLUTION) ni sehemu ya utekelezaji wa ASDP???!! Mimi sijui hapo tena wakuu na mipango ya nchi hii. Hii imeingia kichwakichwa!!! Politics is the dirtiest game ever!!!

  2010 is just at the corner!!1 Wapiga kura wengi ni wakulima, viini macho vya kuomba kura!!
   
 3. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Huu ndio msingi wa kilimo kwanza, mkulima original wa Tanzania amewahi kuangaliwa na kujaliwa na mtu yoyote? Kidogo wakati wa Siasa ni Kilimo subsidy ya mbolea na pembejeo mpaka vijijini, kilimo ni uti wa mgongo wa nchi hii pale mkulima alithaminiwa lakini sasa SIJUI LABDA MAAJABU YATOKEE!!!!!!!!!!!
   
 4. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Ndo hao ya kukurupuka, sera hii imetangazwa kama wiki moja baada ya bajeti kutangazwa. Wangekuwa wameipata mapema maybe wangeweza kuiingiza kwenye bajeti.

  ASDP inafanya vizuri, tena ukaguzi wake unafanywa na LOcal Government Support Program au Local Government Development Grant (LGSP au LGDG) hawa jamaa hawana mchezo. Endapo Serikali ingeongeza mchango wake hapo yaani kuongezea ktk kile wanachotoa wafadhili tungeweza kufanya vema zaidi.

  Hii ya kuanzisha sera kwa lengo la kupata kura, itashia kushindwa kama zilivyoshindwa vibaya kauli mbiu za maisha bora kwa kila Mtanzania na ile ya kasi mpya.
   
 5. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Ulimwengu sasa unafuata nadharia ya 'bottom up'. Tena wakulima wanaibiwa na kunyonywa sana na wafanyabiashara. Wafanyabiashara ndiyo wanaopanga bei ya mazao, ndio wanaoamua vipo na lopesa. Kweli leo wanaweza kuanzisha kitu chema kwa mkulima?
   
 6. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Serikali hii ni ya kupiga kelele tu za majukwaani, walipiga marufuku wakulima kulazimishwa kuuza mazao kwenye magunia kwa mtindo wa lumbesa lakini walishindwa kusimamia. Makelele mengi sana.
   
 7. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kwamba kukosekana kwa vipimo ni tatizo pia na ni moja ya vyanzo wa kuibiwa kwa wakulima hata kile kidogo wanachokipata kwa shida. Nchi zilizoendelea mkulima hauzi kitu bila mizani (beam balance), hata nyanya, viazi, mboga za majani, vitunguu swaumu (galic), matunda nk vinapimwa kwenye mizani.

  Ni vema idara ya vipimo, wizara ya kilimo, TCCIA nk kutafuta vipimo vya mazao. Itakuwa rahisi hata kufuatilia kodi.
   
 8. M

  Magezi JF-Expert Member

  #8
  Sep 8, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hii ni misemo tu ya CCM hakuna lolote, mbona kasi mpya, nguvu mpya na ari mpya imefulia siku nyingi na hakuna anyeitaja hadharani hata kikwete mwenyewe. Hii ya kilimo kwanza hata january haifiki.
   
 9. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #9
  Sep 8, 2009
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu kama wewe ni Mtanzania na unajua mwaka huu na ujao kuna nini, utajua kwanini Kilimo Kwanza sasa hivi. Tatizo jamaa wameshtuka mmekuwa wajanja mno mnachokonoa kila mahali mara Richmond, mara BOT mara Kiwira. Sasa wanawatwanga dozi kwenye mshipa, waone jeuri yenu
   
 10. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #10
  Oct 1, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Hii ndiyo kilimo kwanza. Maswali ya kujiuliza je, matatizo ya kilimo chetu ni nini? vipaumbele ni vipi?
  well, kwa hapa inaonekana matatizo ni magari, pikipiki, baiskeli na nyumba. Je, hii ni kweli?
  Sera ya Serikali ktk kilimo kwanza inaonekana kuto mlenga mkulima moja kwa moja. Je, itafanikiwa kuleta mapinduzi ya kilimo?

  My opinion, Serikali ingeweka mikakati na mipango ya kuongeza uzalishaji na tija (productivity) ktk kilimo. Baada ya kufanikiwa ktk hilo ndipo tatizo la watalaam kukosa usafiri lingejitokeza kutokana na uwingi wa uhitaji wa huduma yao. Anyway I'm done
   
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Oct 1, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  CHANZO CHA HIZO KELELE ZA KILIMO KWANZA NI KUWA SIKU MOJA
  MJINGA MMOJA ALIKUWA ANATAZAMA TV YA MLIMANI AKAONA

  WAMEANDIKA ELIMU KWANZA......
  NA yeye akaamua kujifanya mbunifu na kuja
  na huo upuuzi wa KILIMO KWANZA...
  HIII NCHI HAMNA KITU KABISA...
   
 12. K

  Koba JF-Expert Member

  #12
  Oct 1, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  badala ya hata kufikiria kumwaga pesa kwenye matrekta,mbolea yakayosaidia wakulima moja kwa moja wao wanaongea kununua magari na pikipiki za maofisa kilimo!
   
 13. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #13
  Oct 2, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Koba, tumesalitiwa mkuu, yaani hii ni aibu kubwa. Huu ni ufujagi wa fedha za umma. Fikiria kuna Wilaya ngapi, kata ngapi na vijiji vingapi ndo utajua kuwa hiyo pesa ni nyingi sana.

  Kwanini wasichague maeneo machache wakazalisha chakula cha kutosha hasa kwa kuanzia? Let say wakaamua kuanzisha mashamba ya umwagiliaji bonde la Rufiji, Ruaha na Kilombero. Wakazalisha chakula kingi na kukisambaza nchi nzima.
   
 14. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #14
  Oct 2, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hivi unapoongelea mikakati na mipango ya kuongeza uzalishaji hili la vitendea kazi kwa maafisa ugani sio moja kati ya hiyo mikakati unayoongelea ya kuongeza uzalishaji?
   
 15. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #15
  Oct 2, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Mkuu ngoja nikuambie a simple logic: Kunapokuwa na upanuzi wa kilimo, uzalishaji na shughuli ndipo kunakuwa na uhitaji wa mkubwa wa watalaam. Hapo ni kunakuwa na tatizo la watalaam kushindwa kufika maeneo yanayotakiwa kwa wakati, ndipo uhitaji wa magari, pikipiki na baiskeli unapotokea. But not fro nothing!

  Mkuu mimi nahoji: Kilimo kwnza inataka kuleta mapinduzi ya kilimo sasa Je, matatizo ya sasa ktk kilimo ni yapi?

  Kwani huwezi kuleta mapinduzi ya kilimo bila kujua hali halisi ya sasa (situational analysis). Huwezi kupanga kupanga na kutekeleza mikakati bila kujua tatizo (undesirable situation) ni nini? Huwezi kufikia lengo bila kujua unataka kuvuna nini (goal/desirable situation).

  Serikali imekurupuka tu na kutenga mabillioni ya walipa kodi kununulia magari, pikipiki, baiskeli na kujenga nyumba bila kupitia mchakato stahili.

  Kimey, nadhani unatakiwa kuwa na huruma japo kidogo kwa nchi yako. This is a false start of 'Kilimo Kwanza'.
   
 16. B

  Bongo Lala Member

  #16
  Oct 2, 2009
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kilimo kwanza ni idea ya best yake mkuu wa kaya, dunstan mrutu, the executive secretary of tanzania national business council (tnbc). aliibuni na akaipropose katika local investors roundtable ndipo watu wa serikali wakaiadopt, haina kubwa jipya ukilinganisha na mipango kama hiyo iliyokwisha kufanywa huko nyuma. in other words its is new wine in an old bottle
   
Loading...