Sera ya Chadema ya Usalama wa Taifa na Ulinzi ni ipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sera ya Chadema ya Usalama wa Taifa na Ulinzi ni ipi?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 16, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Baada ya ajali ya ndege ya mafunzo na matukio ya hivi karibuni ya ujambazi ambayo yamesababisha mauaji ya watu mbalimbali na vile vile vitendo vya wananchi kujichukulia sheria mikononi na kuwatia mafuto wanaowatuhumu kuwa ni vibaka kumenifanya nihoji maswali fulani. Nikiangalia vile vile kuvuja na kulega lega kwa idara ya usalama wa taifa na mfumo mzima wa usalama wa taifa sina budi kuhoji Chadema chama ambacho kinataka kushika "madaraka" ya nchi kina sera gani juu ya:

  a. Usalama wa Taifa
  b. Mfumo wa usalama wa taifa
  c. Muundo wa Jeshi la Polisi
  d. Na kushughulikia uhalifu mdogo

  Najua kwamba wengi hamtaki kujua sera hizo hadi itakapoingia madarakani ndiyo mtataka kujua, miye ningependa kujua sasa.
   
 2. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mwanakijiji si tusubiri ilani yao ya uchaguzi karibu itatoka sasa wakianza kujibu kila mmoja kwa sasa na resources zenyewe sio nyingi utakuwa ni divert resources bila mpangilio. Swali ni zuri lakini uwe na subira. Unanikumbusha enzi za shule jamaa akiwa ametoka likizo na amepandisha kituition kidogo basi mwalimu akianza tu topic kesha anza kumuuliza maswali tena ya mwisho wa topic halafu wote tunamwona genius. lakini baada ya wote kuipitia anarudi kwenye position yake
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwenye ilani yao iliyopita waliwahi kuwa na sera kama hiyo ni ipi?
   
 4. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tukiandika kila kitu cha kiserikali kwenye sera basi ujue kuwa tutakuwa na kitabu kimoja kikubwa sana. Hivyo huwa ni mambo muhimu tu ambayo huwa ndiyo yanaandikwa tena kwa mtasari tu lakini bado page zinakuwa 100 na kitu. Sera haitaweza kuelezea njisi ya kununua silaha au kupandisha mishahara. Kama kuna kitu muhimu ambacho wanaona kuwa watakifanya tofauti ndiyo inabidi waseme, kwa mfano kutengeneza silaha za nyuklia. Lakini wakisema kuwa wataimarisha jeshi na kuwa la kisasa atakayetoa maelekezo atakuwa ni mtaalamu wa jeshi anayelipwa na serikali au unataka chadema wamuajiri mtaalamu wa mambo ya kijeshi wao kazi yao ni kusema nia yao ni nini mambo mengine yatafanywa na wataalamu bwana. Ruzuku yenyewe kiasi gani nai waajiri ma consultant wangapi jamani ku cover shughuri zote za serikali?
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Of course.. sera muhimu kwa taifa zinatakiwa zijulikane kwani siyo siri. Au hizi sera zimebakia tu vichwani mwa watu na tutazijua zikapoanza kutekelezwa?

  Of course lakini tutajua kuwa hata mna pango wa kununua silaha! au hilo nalo ni siri?

  Kwa hiyo wataendelea na ndege zile zile za 1967? hamna mpango wa kuupgrade our military arsenal au kuileta TISS katika ulimwengu wa kiileo.

  Sasa mtatengeneza sera bila kuwahusisha watu wa jeshi? Kuna mambo ya kisiasa ambayo yanatoa uongozi wa kijumla na yale yenye kuhitaji details za kijeshi yanafanywa hivyo lakini kwa vile jeshi letu liko chini ya raia ni lazima raia watoe uongozi wake wa kisiasa wakisikiliza maoni na mahitaji ya kijeshi.

  Kimsingi hamna sera inayoeleweka ya usalama wa taifa au ulinzi kama hadi hivi sasa hamjaweza kuiandaa. Nimekuelewa.
   
 6. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  MKJJ naelewa hali yako uliyonayo kwa sasa si ya kawaida, kuna wengine wamekuambia 'you are wounded', ni muda mwafaka sana kwako kutumia akili ya ziada kui control hali hii vinginevyo unaweza kujikuta unapoteza hata kile kidogo ulichoanza kukijenga.

  Kisaikolojia ukiona mtu anakuja na maswali mengi mengi yasiyo na mpangilio tena akiomba apatiwe jibu wakati huo huo jua kuna walakini. Mfano unakutana ghafla na mtu anayekudai na kukuambia anataka hela yake sasa hivi huku akijua fika hakuna uwezekano kwa wakati huo. Mtu wa aina hiyo hata asipopata alichokitaka lakini moyoni atajiridhisha, leo nimemkomoa.

  Inawezekana kabisa akawa kati ya makundi ya jamii ifuatayo; amekasirika, amesusa, amezira, anakomoa, anajionyesha, analipiza, anakejeri au anataka shari. Atakuwa anafanya hayo kwa kuwa kuna kitu kimembana rohoni naweza kusema kama pumzi sasa anatafuta pa kupumulia 'mind refreshment'

  MKJJ kulazimisha Chadema leo wakuambie mipango ya usalama wa Taifa ni sawa na niliyoyasema hapo juu hata CCM sijui kama watakuambia in short it is impossible. Kwa maoni yako unafikiri Chadema inaweza kukuambia jeshi lao la polisi litakuwa say na polisi wangapi, nafikiri hii ni hasira, unafanya hivi ili Chadema ionekane imeshindwa kujibu useme si unaona hawajui hata wanataka kufanya nini.

  Kuhusu uhalifu mdogo mdogo, unataka Chadema wakuambie polisi yao itapambanaje na wamachinga wa mitaani au vibaka wa mifukoni au vijeba wa Tannesco na Deiwaka wa daladala, sioni maswali kama haya yanaleta mantiki yeyote kama si hali ya mtu kuzira au kukomoa.

  Mara chache sana sera kutaja kwa idadi sera mara nyingi zinataja asilimia, tutapunguza uhalifu kwa asilimia 10 au tutaongeza bajeti ya elimu toka asilimia 20 ya sasa hadi asilimia 35 nk. Mambo ya mipango sijui ya Usalama wa taifa au polisi huwezi kukuta yameandikwa wazi sehemu yeyote ili kila mtu ayasome.
   
 7. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Sina uhakika lakini kuseam CHADEMA AU CUF an CCJ waeleze sera zao za usalama na ulinzi itakuwa kama si kuwaonea ni kutaka waoe matamshi ya kisiasa. Kutoa sera zenye maneno ya kisiasa sio kazi kubwa mfano

  • Kuimarisha Majeshi ya ulinzi na usalama (JWTZ,Polisi,Magereza) kuwa ya kisasa
  • Kuimarisha ulinzi wa raia na mali zao
  • etc
  Kifupi nadhani sera Ulinzi na usalama ya CHADEMA , CUF an CCj inaweza iswe tofauti na ya CCM kinachoweza kuwa tofauti ni muundo.Kwa sera ya CHADEMA ya majimbo inawezekana sera zile zile za CCM zikafanikishwa kifanisi zaidi tofauti na Jeshi linalondesha from Dar. Najua kwa sera ya CHADEMA viongozi wa majimbo watatakiwa kupigiwa kura inaweza kwenda mbali hata wanachi wakawa wana say/nguvu juu ya utendaji wa Viongozi wa kipolisi.

  Kitu kingine nahakika kuna usiri kwenye mambo ya usalama na utendaji wa jeshi letu. Sasa CHADEMA, CUF watakuja na detail gani wakati hata hao CCM hawawi wawazi kusema wanafanya nini wananunua nini, etc. Ni rahisi kwa chadem kuwa na sera ya uchumi sababu wanajua na wote tunajua VAT ya CCM ni 20% makusanyo ya TRA ni kiasi kadhaa, export ya dhahabu ni once XX. Nina maana Laizma chadema wawe na kianzio cha basic information kuwa na sera za ulinzi. Kama current basic information wanazo basi wanaweza kuogopa kuzitaja na kufanyia comparison na sera zao kwa sababu tunazozijua wote.

  Siwezi kushangaa mtu kuwa matatani kusema sera ya cham fulani itabadilisha organisation structure XXX na idara JJJJi za UWT na kutumia organisation structure CCCC na idara JJJ kuvunjwa.

  Any way tutafurahi kusikia sera zao wote hata CUF pia
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Jul 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  r u guys serious? yaani mnataka kukipa chama nchi na hamjui, hamtaki kujua au hamjali sera zao za usalama na ulinzi? you must be kidding me? Sasa watu waache kuuliza maswali kwa sababu ati wako wounded? Na CCM iliniumiza nini mimi kuuliza maswali kuhusu TAKUKURU, Richmond, Dowans? n.k Sikuwa wounded then, and I'm not now.

  Sasa mkina na sera au mkianza kuja na mipango (maana hamna sasa) ya kulinda taifa kwa kutumia mishale na marungu na kuanzisha vikosi vya maninja tuje kushtuka?
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,525
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, nimeanza kwa kungoli kitufe cha 'thanks' kwenye thread hii,sio kwa kukushukuru, bali just kukujulisha nimekusoma, labda mbele ya safari, JF B itaongeza vitufe, ili kiwepo cha 'point noted' sio lazima 'thanks'.

  Nilisema hapo nyuma, Mzee Mwanakijiji, you are wounded!. Ukubali usikubali, kupasuka kwa ngoma ya CCJ uliyoipiga sana, kumekuathiri kisaikolojia na kukuumiza.

  Ili kuendelea kuonyesha you are still strong, hujaumia, sasa inaibuka na style ya ku hit back, na hapa na hapa target ni Chadema, walikokimbilia hao wa CCJ wengine, ili kuidiscredit Chadema.

  Hakuna ubishi kuhusu uwezo wako wa uchambuzi na maono. Hakuna ubishi kuhusu vision yako na insight kwenye baadhi ya issues zenye maslahi kwa taifa, hili la kuanza kuuliza sera za Chadema kwenye national security, sio tuu ni uonevu, bali pia zinaweza kuidiscredit Chadema ionekane security risk, hivyo isichaguliwe.

  Mzee Mwanakijiji, mimi binafsi, nakukubali, in fact naadmire sana uwezo wako na nasoma sana makala zako na kutembelea sana 'Mwanakijiji .com', nakuomba sana, kipindi hiki kifupi tumia uwezo wako katika kujenga, sio kubomoa. Silazimishi lazima ujenge Chadema, jenga hata CUF ama endelea kuimarisha CCM kama ulivyokuwa ukifanya kule nyumba kwa makala za kuibeba CCM, but now not at the expense of Chadema, please!.
   
 10. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mwanakijiji kumbuka kuna chama kimoja kiliibuka na suala la Mahakama ya Kadhi kama ajenda lkn chama kingine kilidakia na kutumbukiza kwenye ilani yake ya uchaguzi. Bahati nzuri jambo hilo limekuwa gumu kutekelezwa vinginevyo tambo zingekuwa nyingi sana. Nachelea kusema kuwa kama sera ya CHADEMA kwenye mambo yaliyoainishwa ni nzuri, chama kilichodaka hoja ya Mahakama ya Kadhi kinaweza kunyakua sera hizo pia, nafikiri ni vyema tusubiri kipenga kitakapopulizwa kila mtu aanze kuanika mpunga wake; hata hivyo umewapa mwanga CHADEMA na vyama vingine walau kuzingatia mambo hayo kwenye sera zao kama walikuwa hawajafanya hivyo!
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Jul 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  duh.. hata kuanza kuchambua sera za Chadema bado.... nafikiri ukikaa na kufikiria utaona labda mimi naisaidia Chadema zaidi kuliko wale ambao hawataki kuuliza maswali wanataka waimbe kumbaya tu.
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Jul 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo mnataka tuwape nchini chama ambacho hatujui sera yake kuhusu national security. My position ni kuwa it has to be stronger and more articulate kuliko ya CCM, would you agree? au tuwape tu uongozi wa nchi watajua mbele ya safari kama wengine wanavyotaka iwe? Au tuamini tu kuwa wanayo hata kama hatujui kama wanayo au kutuambia japo kwa juu juu ikoje?
   
 13. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  [FONT=Tahoma,Bold]Hii ni Ilani ya CCM 2010-2015 kuhusu Ulinzi na Usalama. Usitegemee CCM au chama chochote kuja na more detailed documents kwa masuala kama haya. Sidhani kuandika maandishi kama haya Chadema wanashindwa, kitu kinachotakiwa ni udhati wa kuyatekeleza.[/FONT]​


  [FONT=Tahoma,Bold]
  [/FONT]


   
 14. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #14
  Jul 17, 2010
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mwkjj punguza jazba hebu soma hii............kutoka kwa Naibu Katibu mkuu wa Chadema na hiyo ilikuwa Mei 2008
   
 15. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #15
  Jul 17, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo utachagua CCM kwa sababu Chadema haina sera kamili inayolenga Usalama wa Taifa na Ulinzi? kazi kweli kweli...
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Jul 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kwa mtindo huu wa uelewa naweza kusema kwa uhakika tuna tatizo kubwa zaidi kuliko CCM; watu wawili ambao wangeweza kuelezea suala la Chadema na usalama wa Taifa wamebakia kunipa mifano ya CCM! Na mwingine ndiyo kabisa haelewi ninazungumzia nini.
   
 17. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #17
  Jul 17, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  there u go...thinking u know it all...hahaha! haya kila la kheri na uelewa wako uliokupeleka kushabikia CCJ iliyokuwa haina sera hata moja!
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Jul 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  classical Tanzanian mentality!!! mtu akizidiwa hoja anakimbilia "anajifanya anajua sana",.. "ana ringa sana'.. "oo anatamba mno"..
   
 19. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #19
  Jul 17, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji,
  Naona jaribu pia kukubali maoni ya watu wengine kuhusiana na jambo hili. Limekuwa mwiba na watu watadhani uko against Chadema yetu kwa kuwa tu imebeba baadhi ya wanachama wa sisi j. Kitu ambacho kinaonekana kama ndivyo ilivyo maana hukuwahi kuuliza maswali yote haya kabla.

  Najua utasema nilishawahi kuwapa ushauri lakini hawataki, plz elewa chama upokea ushauri mwingi na si lazima ipokee shauri zote zinazoletwa na kuzichukua kama zilivyo. Chama kina haki ya kukataa baadhi ya ushauri.

  Sipendi kuwaita wale waliohama chama na kuja Chadema kama viongozi wa sisi j maana uongozi wao haukuipeleka sisi j popote. Daima nitawaita tu wanachama wa sisi j wakati ule uliopita. Na kwa kuja Chadema watatakiwa kujenga chama kwa misingi waliyoikuta. Hawatakiwi kulazimisha kwamba ni lazima mawazo yao yakubalike. Lakini wanaruhusa yote kuleta mawazo mazuri kwa ajili ya ujenzi wa Chadema na nchi kwa ujumla wake.

  Kwa upande wangu kwa hali ilivyo sasa naona kama haupo kwa ajili/niaba ya sisi m, bado unayo nafasi ya kuijenga hiyo sisi j unayodhani ni bora sana kisera na kimtazamo hadi kwenye kiwango unachodhani ndicho unahitaji na sisi baada ya hapo tutakuja nyuma yako. Na kama unadhani na sisi j haina unachohitaji unaruhusa kujiunga na sisi m na kuwa mpinzani within sisi m ukiwa umejiunga na lile kundi la wakina dkt Mwakyembe na wenzie. Bado una ruhusa.

  Tena ujue ili na sisi tujiunge na chama chako tueleze yooooote unayotuuliza.

  Otherwise ni watu wachache wataendelea kuwa upande wako na utashusha credibility yako hapa. Plz ebu pumzisha akili kidogo maana hata mimi naamini una majeraha hata kama hujaona damu ikitoka.
   
 20. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #20
  Jul 17, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Sasa wewe MM,kwanini usisubiri Ilani ya Chadema ya uchaguzi iwekwe hadharani,kwa nini usisubiri wakati wa kampeni uwasikie watazungumzia nini kuhusu sera yao ya Usalama wa Taifa.Kumbuka hata ung'ang'anize vipi huwezi kupata jibu kwa wakati huu mbali na jibu kama kuboresha jeshi liwe la kisasa.kuboresha maisha ya askari polisi ili kuwapa motisha ya kazi n.hayo ndiyo majibu ambayo utayapata ambayo kila chama cha siasa kitakwambia hivyo hivyo.hata mwananchi wa kawaida tu atakuwa na maoni hayo hayo.Usubiri wakati wa kampeni watajieleza kwa kila nyanja,hapo ndipo uulize kama haujaridhika,au kukipa kura chama kikingine ambacho utaridhishwa na sera zao
   
Loading...