MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,565
- 836
Uko sawa lakini tukitaka kupata defintion sahihi ya mzeee tunayetaka kumsadiai tunatakiwa kuangalia beyong age?
Nimelisoma wazo lakini ingawa kuna complication katika kuwatambua lakini bado ni wazo sahihi . Hii complication ni kama ya wanafuzi wa vyuo vikuu kupata mikopo. nadhani tujairibu kupendekeza njia sahihi za kuweza kuwaweka watu katika kundi hili la "wazee" wanahitaji msaada.
Kwa hiyo tukichanganya umri, location, vipato, rasilimali na tukiwashirkiza viongozi wa mitaa tunaweza kupata wazee sahihii wanaotakiwa kusaidiwa.
- Mfano mzee mwenye miaka 50 yuko dar na mwingine ana miaka 50 yuko mAnyoni. Kama ni definiton sahii basi huyu mwenye makazi manyoni ni ndio anaqaulify kupata upendeleo wa afya .
- Kama mzee ana nyumba zake mbili anapata kodi mwingine anategemea wajukuu na watoto. yupi ana qualify
- Kuna wazee ambao walikuwa wakulima hawakuwai kupata mishahara na ajira za ofisini na wameishiwa nguvu
Ni kweli mkuu kupata standard definition ni ngumu na ni swala linalo hitaji majadiliano mazito na si kwa serikali kulala leo na kuamka Jumatatu na kuamua kupachika pachika vitu. It is very hard kuja na standard definition kwa sababu Tanzania yenyewe haiko uniform. Kwa nchi kama za wenzetu hata uishi wapi ndani ya nchi standard of living ni almost za same kwa hiyo hata life expectancy kimaeneo haipishani. Lakini kwa Tanzania mtu wa Dar Es Salaam na mtu wa vijijini mikoani ni kama vile wanaishi dunia mbili tofauti.
Mkuu Kibunago alitoa point moja nzuri sana ambayo nadhani ndiyo tatizo letu kubwa nalo ni kuidentify watu hata hapo ambapo tumesha pata definition ya kitu fulani. Tuseme kwa mfano tu tuna kubaliana mzee ni mtu mwenye miaka 50 je hii healthcare ya bure apewe hata mtu wa miaka 50 ambae bado ana fanya kazi? Maana kwa wenzetu mfano Marekani Medicare ya wazee inaanzia 65 ambayo ndiyo umri nao wa kustaafu.
Halafu pia kama tukisema healthcare ya bure kwa wazee ina maana lazima iwe standard. Huwezi kusema healthcare ya bure kwa mzee halafu uanze kubagua na useme lakini mzee mwenye kipato fulani au uwezo fulani au mwenye watoto wenye kipato fulani asipewe. Haiwezekani. Marekani Medicare ni kwa mtu yoyote 65+ regardless ya kipato chake. Sasa sisi mtu akisha kuwa mzee lakini tuseme mzee mwenye uwezo fulani haqualify basi hiyo siyo free healthcare kwa wazee tena tuite kitu kingine. Maana as the name suggest free healthcare for the elderly should be free healthcare for the elderly sasa kama siyo kila mzee ana qualify tutai itaje free healthcare for the elderly?
Ndiyo maana mimi nasuggest tuwe na free healthcare for the poor tukiangalia kipato cha mtu. Hata kama wazee wengi ni masikini kama unavyo sema haina shida because kama ni masikini it means they will fall under the policy. Kuhusu nani ni masikini hiyo ni easy kudefine kwa sababu tuna weza kusema kwa standard za Tanzania mtu mwenye kipato chini ya kiwango fulani basi ni masikini.