Sera ya CHADEMA "Kupunguza Matumizi ya Serikali yasiyo ya Lazima"

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,428
Wadau nawasalimuni!

Kama kumbukumbu zangu ziko sawa, miongoni mwa sera za CHADEMA Katika uchaguzi 2010,ilikuwa ni pamoja na kupunguza matumizi ya serikali yasiyokuwa ya lazima.Miongoni mwa matumizi ambayo chama kilisisitiza kwamba ni lazma yapunguzwe (kwa kuwa si ya lazima) ni pamoja na posho (sitting allowance ndani ya bunge) ambapo hoja ilikuwa kwamba; hela zitakazookolewa kutokana na ubanaji huo wa matumizi yasiyo ya lazma, ziwanusuru wananchi masikini.. Sasa mimi ningependa kujua kwa yeyote anayefahamu vizuri. mambo yafuatayo;

(a.) Je! wabunge wa CHADEMA walishaacha kuchukua posho hizo ili kuonesha mfano juu ya kile walichokiongea! kama wameaacha, ningependa kufahamu wameaacha tokea lini.

(b.) Kama hawajaacha, ningependa kufahamu ni kwa nini hawajaacha na ni lini wataacha na kwa nini kipindi hicho, au kama hawana mpango wa kuacha tena, ningependa kufahamu vile vile!.

(c.)Mwisho ninge furahi kama ningefahamu kama chama kitaingia na sera hiyo (miongoni mwa zingine) au ni miongoni mwa sera zitakazofanyiwa "editing" kuelekea uchaguzi 2015.

Nadhani hili si eneo la matusi, kwa hiyo kabla ya mtu kutukana, kwanza ajiridhishe ikiwa kuna ulazma wa kutukana.Vinginevyo, propaganda ya kwamba nimetumwa na CCM, Inaruhusiwa kutumika kwa anayetaka.

Hawajaacha kupokea Sababu Bunge halijapitisha hilo Azimio.
Wabunge wote wangeazimia hii ingekua ni hatua Nzuri sana.
Pamoja na Sera ya Chadema kupunguza gharama zisizo za lazima, Inakua vema na bora zaidi kama mkiamua jambo wote kwa pamoja, Lakini pia haiingii akilini unakataa kupokea posho wakati hujatafuta Mfuko kwa ajili ya hizo posho ili kuhakikisha zitumika ipasavyo.
Rai yangu ni kuwa ili hii sera ya Chadema ipate nguvu ni lazima Bunge liazimie kutokupokea posho.

Vinginevyo wale wanaokataa wakati hawajui zile zinakwenda wapi ni unafki
 
Sasa inamaana kwamba wakati ule tulipomlaumu Mzee Shibuda kwa kutetea kuendelea kuchukua posho, tulimlaumu kwa makosa?

Hivi kama wabunge wote wa CHADEMA wangekataa kwa umoja wao, wasingeweza kuwashinikiza na wa CCM pia kukataa kupitia ushawishi wa ndani ya bunge, na ikishindikana kupitia kuwashitaki kwa wananchi kupitia nguvu ya umma kama wanavyofanya katika mambo mengine? hivi bila kuanza jambo (kwa hoja ya kwamba mtu ataanza mwenyewe na haitasaidia), jambo linaweza kukamilika?
 
Wadau nawasalimuni!

Kama kumbukumbu zangu ziko sawa, miongoni mwa sera za CHADEMA Katika uchaguzi 2010,ilikuwa ni pamoja na kupunguza matumizi ya serikali yasiyokuwa ya lazima.Miongoni mwa matumizi ambayo chama kilisisitiza kwamba ni lazma yapunguzwe (kwa kuwa si ya lazima) ni pamoja na posho (sitting allowance ndani ya bunge) ambapo hoja ilikuwa kwamba; hela zitakazookolewa kutokana na ubanaji huo wa matumizi yasiyo ya lazma, ziwanusuru wananchi masikini.. Sasa mimi ningependa kujua kwa yeyote anayefahamu vizuri. mambo yafuatayo;

(a.) Je! wabunge wa CHADEMA walishaacha kuchukua posho hizo ili kuonesha mfano juu ya kile walichokiongea! kama wameaacha, ningependa kufahamu wameaacha tokea lini.

(b.) Kama hawajaacha, ningependa kufahamu ni kwa nini hawajaacha na ni lini wataacha na kwa nini kipindi hicho, au kama hawana mpango wa kuacha tena, ningependa kufahamu vile vile!.

(c.)Mwisho ninge furahi kama ningefahamu kama chama kitaingia na sera hiyo (miongoni mwa zingine) au ni miongoni mwa sera zitakazofanyiwa "editing" kuelekea uchaguzi 2015.

Nadhani hili si eneo la matusi, kwa hiyo kabla ya mtu kutukana, kwanza ajiridhishe ikiwa kuna ulazma wa kutukana.Vinginevyo, propaganda ya kwamba nimetumwa na CCM, Inaruhusiwa kutumika kwa anayetaka.

Weka picha basi na source ya hii hadithi
 
Ukiacha kuchukua Posho CHADEMA wanakuona MSALITI .
Mkuu MSALANI wewe unaonaje msimamo wa kuchukua posho za kukaa, unaoungwa mkono na wabunge wenu CCM? Unaona kwamba mtizamo wao ni sahihi hasa ukizingatia kwamba tayari wanalipwa mishahara tena mikubwa kwa ajili ya kazi hiyo?
 
Last edited by a moderator:
Weka picha basi na source ya hii hadithi
keep it up! ukiendelea hivyo karibuni utailelea nchi hii ukombozi mkubwa.Watu kama ninyi ndio mtakao ikomboa nchi hii kusema ukweli.Endelea hivyo hivyo
 
Only three contributors?.....Mmmh
Hivyo ndivyo hali ilivyo kwa sasa na hata hao wanaochangia wanachangia michango kama hii
quote_icon.png
By Safari_ni_Safari

@BETLEHEM umeshahama tena CHADEMA?

Kwa kweli inasikitisha sana kusema ukweli.
 
@BETLEHEM umeshahama tena CHADEMA?

mkuu ukihoji ukitofautiana kimtazamo unakua hauko chadema?alichokiuliza ni facts sema siku zote mimi nasema vijana wengi wa humu ni mamluki,na hata siku CDM ikichukua dola kwa kua hawajui wanaipendea nini CDM watakuja kubadilika tu na ku vote kwingine
 
pole sana..........kwa masikitiko yako!
ungechangia mada ungesaidia kurudisha hadhi ya jukwaa la siasa.au na wewe ni miongoni mwa wale wanaofanya jitihada za kulifanya jukwaa hili lipoteze muelekeo na hatimae watu wanaopenda mijadala walikimbie, wabakie wapenda udaku?
 
mkuu nakupongeza kwa uchambuzi yakinifu mimi nadiliki kusema hiyo sera anatekeleza ZZK tu basi kwa CDM!!
Mtu kama lema alikanusha hadharani kwamba hawezi kuacha posho,kwa mustakabali huo basi SHIBUDA ndo mtekelezaji wa kwanza wa ilani na sera wanai practise wabunge wa chadema........walimpinga mwishowe wakaungana nae kimya kimya halafu hadithi zinaonyesha aliitwa msaliti,KWAHIYO DHANA USALITI NDANI YA CHADEMA NI MTU YEYOTE ANAYETOFAUTIANA MAWAZO NA MBOWE PAMOJA NA SLAA
 
mkuu ukihoji ukitofautiana kimtazamo unakua hauko chadema?alikiuliza ni facts sema siku zote mimi nasema vijana wengi wa humu ni mamluki,na hata siku CDM ikichukua dola kwa kua hawajui wanaipendea nini CDM watakuja kubadilika tu na ku vote kwingine

Bahati mbaya mimi sio kijana!
 
mkuu, nadhani huu ndio muda wa yale yalioko ndani ya vifua vya watu kudhihirika.

Ndugu mwekundu , huu ndio muda muafaka wa kujua nani mnafiki na nani si mnafiki kwa kuangalia matendo badala ya maneno.

Ndugu mwekundu , kuna watu wanataka kuliharibu kabisa jukwaa hili la siasa na kulifanya lipoteze maana ya kuwepo kwake.Sasa ni rahisi kujua nani ni nani.Ni jukumula kila mwenye mapenzi mema na jukwaa hili akasaidia kulinusuru kulingana na umuhimu wake katika kuibua hoja za msingi,

Ndugu mwekundu , naamini vijana hatukuumbwa ili kazi yetu iwe ushabiki. Naamini tumepewa akili kubwa zaidi kidogo ya hapo.Hata hivyo ni jukumu la kila kijana kuamua kuziweka fikra zake katika level fulani.

Ndugu mwekundu , kwa muelekeo ninaouona Tanzania bado tuna kazi ngumu sana kwa kweli.

Ndugu mwekundu , tusikate tamaa kwani hata mandela angekata tamaa, Afrika kusini isingepata uhuru.
 
Last edited by a moderator:
Bahati mbaya mimi sio kijana!
Hongera kwa mchango wako mzuri.Kimsingi mchango wako huu unamashiko sana na utasaidia sana katika mabadiliko ya kisiasa nchini.Keep it up.Wanahitajika watu kama ninyi ili kulikomboa taifa hili.Hongera sana!
 
Back
Top Bottom