Sera ya CCM ya kula na kila anayebwatuka na kusema udhaifu na ubadhirifu wake, umeonesha jinsi gani viongozi wetu wanavyopenda pesa na si kutetea

Paulsylvester

JF-Expert Member
Oct 15, 2021
1,467
3,381
Hii ni dhahiri kuwa, Kwa Africa na Tanzania, kuwapata viongozi wenye focus na maisha ya watu wao ilivvyo ngumu kupatikana.

Sera ya CCM ya kuwalambisha Asali wote wenye vidomodomo na kiherehere, imetuomyesha jinsi watu hao malengo yao si kuwatetea wananchi, Bali kutafuta furusa za kwao na upigaji tuu, na kwamba, ikiwa watatosherezwa matumbo yao, hawako tayari tena kujihusisha na kutetea wananchi!

Tangu tusikie yule mwenzetu aliyeko nje akutane na mlambisha asali na kutangaza kulipwa haki zake zote, amebadirika na kuwa mpole kana kwamba watanzania aliokuwa akiwapigania maisha yao yamekuwa bora na mazuri na kwamba umasikini wa watanzania umeisha!

Viongozi wetu wote wa Upinzani Kwa sasa wote wamekula asali na wamekaa kimya huku wananchi wakishuhudia kupaa Kwa bei za bidhaa zote na kuwa na maisha magumu zaidi tangu Uhuru

Kwa hali ilivyo, tangu kuundwa Kwa CCM, Kwa miaka hii, ndio tunashuhudia kuwa na CCM iliyoshindwa kila pahala,

CCM ya walaji na inayotengeneza tabaka kubwa kati ya walionacho na wasiokuwa nacho Kwa sababu ya Sera zake mbovu na zilizoshindwa!

Na Kwa kuwa CCM imelijua hili kuwa haiwezi kabisa kuwakwamua wananchi, inachokifanya ni kuangalia kila mtu anayepiga kelele ili kuwaamusha wananchi kwamba mnaliwa, basi atatafutwa ili tu apate asali yake na atulie!

Kwa miaka michache iliyopita, CCM haikuwa na hii Sera ya kulambisha asali wapinzani, embu angalia zile kelele zilizokuwa zikiimbwa kila kona ya nchi na hata nje ya nchi.

Kwani kumetokea nini sasa?

Wananchi wamekuwa na maisha mazuri kuliko awali.

Kumebadirika nini? Ufisadi umeisha? Rushwa imekoma? Uzembe maofisini umekoma? Vyama vya siasa vinafanya siasa Kwa sasa? Wananchi wanapata huduma bora sasa?

Katiba imeshaandikwa na kupitishwa sasa?
Ndege kununuliwa Kwa cash, hakupo tena?

Sasa kimetokea nini

Nani tena asimame kuwapinga CCM na Sera zao mbovu za kuwafiris wananchi Kwa tozo za ajabuajabu na kuhimiza wananchi kuhusu katiba mpya ikiwa hawa wengine wanakula asali.?
 
Mkuu nadhani hii nchi ilipofikia ni pabaya mno, watu ambao wamekua mbele kupigania maslahi ya wananchi nao wamegeuka sehemu ya kula na kukaa kimya

Tozo zinaumiza wananchi, na viongozi wanaaminisha tozo ni nzuri na haziathiri chochote. Makato ya tozo yamekua makubwa mno, tena mno. Jana nimeenda benki kutoa laki nne, nimekatwa elfu 29, jaribu kuona makato yalivyo makubwa. Na bado CCM itaaminisha imefanya makubwa kwa ajili ya wananchi.

Walitangaza midmshahara watawapandishia watumishi kwa asilimia 23.3%, cha kushangaza wameongeza 0.3%.

Ni mambo ya kuumiza sana, jaribu kuangalia bei ya mafuta (nishati), bei imekua mkasi balaa.

Hivi kweli kwa maisha haya tunaweza kuwa wazalendo kweli???
 
Mkuu nadhani hii nchi ilipofikia ni pabaya mno, watu ambao wamekua mbele kupigania maslahi ya wananchi nao wamegeuka sehemu ya kula na kukaa kimya.

Halafu mtu mmoja aje aseme eti tunalalamika!

Tunalalamikaaa au tunasema ukweli jinsi wananchi tunavyoumizwa?
 
Imefika kipindi sipendi kutazama picha ya kiongozi yeyote,nawachukia mno!ingawa haisaidii,dawa ni kupambania familia zetu kwa namna zote,ingawa kwakweli hali ngumu sana.
 
Mkuu nadhani hii nchi ilipofikia ni pabaya mno, watu ambao wamekua mbele kupigania maslahi ya wananchi nao wamegeuka sehemu ya kula na kukaa kimya.
Walipopigania mlisema wanapigania matumbo yao.

Sasa wacha wajikalie kimya tu.
 
Pumbavu kweli, tulisema sisi mkasema tunatumiwa na mabeberu! Haya sasa Wacha tupigwe na TOZO Hadi akili zitukae vizuri
 
Halafu mtu mmoja aje aseme eti tunalalamika!

Tunalalamikaaa au tunasema ukweli jinsi wananchi tunavyoumizwa?
Sasa mkuu si umlalamikie anaekuumiza?

Unasubiri unaedai analamba asali akusaidie kulalamika wakati unaeumia ni wewe,
Pia unajua chanzo cha hayo maumivu yanasababishwa na nani?

Watoze kodi hadi ya kichwa, pengine ujinga utawatoka watanzania,
Tunaacha mambo ya maana tunashabikia udaku na conection za kipuuzi,
 
..wananchi wote tuwe na viherehere na vidomodomo ili Ccm itulambishe asali wote.

..au ikiona haiwezekani kutulambisha asali itatue changamoto ilizozisababisha.
 
Acheni kulia lia. Wakati ule mliwaita mabeberu. Jiteteeni nafsi zenu. Hakuna wa kuwatetea maana hamueleweki. Mkipewa 10.000 mnakaa kimya. Na yeye kaamua kula ya kwake ili anyamaze. Na wewe kula ile 10.000
 
Back
Top Bottom