SoC01 Sera na Sheria za Tanzania inavyowanyima Vijana Michongo

Stories of Change - 2021 Competition

Gwamanga

Member
Jun 25, 2021
66
138
Mifano ya sera na sheria za tanzania zinavyowanyima vijana wengi michongo.

# Mashariti ya kumiliki na kusajili maudhui ya mtandaoni( Youtube channels, Blog, website, etc)
00B8BBC0-921C-4242-B277-FD7C76912961.jpeg

Chanzo: https://www.tcra.go.tz/uploads/documents/sw-1619110553-The Regulator Special Edition.pdf

Ni vijana au wahitimu wachache wenye uwezo wa kumdu gharama hizo kuanzisha youtube channel na blog au application, Mtaji wake ni mkubwa ukizingatia biashara hiyo inahitaji mwanzoni kuwa na uvumilivu kutengeneza jina kabla ya kuanza kujipatia kipato.

Chanzo kingine: Punguzo la tozo usajili mitandao sawa, lakini…



#Sheria za kusajili pamoja na kumiliki kampuni.
Sheria hizi kwa tanzania zinawanyima vijana wengi fursa ya kufungua makampuni, pamoja na kuwepo sera mbovu pia tanzania mifumo haipo imara pia Haijafungamanishwa, mfano ili usajili kampuni upite, TRA, BRELA, TCRA wakati mwingine TFDA na Taasisi nyingine nyingi kwanini mifumo yote isifungamanishwe kuwa kitu kimoja, kote huko kuna tozo na kucheleweshewa huduma.

Chanzo: Jinsi ya Kusajili Kampuni Tanzania | FiFi Finance Kiswahili

# Urasimu kwenye kutafta leseni ya Biashara na Namba ya Mlipa kodi.

Urasimu upo kwenye kukadiliwa, milolongo ya kupata leseni na namba ya kupata namba ya mlipa kodi.

# Ubovu wa sera ya Elimu, Ukinganisha na mahitaji ya karne ya 21

Haihitaji maneno elfu kumi kuelezea jinsi elimu yetu ilivyo duni, kungundua hilo jiulize maswali haya yafuatayo, 1. Tunamtegemea nani kama mtengenezaji mkuu wa barabara zetu kama sio Mchina hali ya kuwa tuna vijana Tunaowaita Mainjinia wamehitimu pale UDSM na pale UDOM. 2. Ni vijana wangapi wanaoweza kushindana kwenye soko la nje la Ajira. 3. Tunazalisha Madktari bigwa wangapi wenye ujuzi na wanao weza kushindana kwenye soko la kimataifa. Just to mention Few. Fikilia Mimi mwalimu niliyehitimu pale chuo kikuu cha Dodoma nimetumia zaidi ya miaka 15 nikiwa Darasani pamoja na umri wangu nimehitimu nikiwa na miaka 23 Je nini nimekitoa Darasani kwa yule lecturer anayejali maksi kuliko ujuzi? Mwisho wa siku Ualimu wangu haunisaidii chochote zaidi ya kuwa tegemezi, elimu ya tanzania inahitaji maboresho ili iweze kuwa msaada kwa wahitimu.

# Mafungu ya mikopo ya kila wilaya kwa vijana pamoja na elimu kuhusu mikopo hiyo.

Mikopo hii haiwafikii vijana moja kwa moja kwa upande mwingine tunaweza walaumu vijana lakini lawama kwa asilimia 90 zinaenda kwa serikali, Kwenye andiko langu moja Jinsi ambavyo serikali inaweza kupunguza ukosefu wa ajira kwa kuwapa vijana majengo yasiyotumika, kwanini Majengo hayo yasiambatanishwe na mikopo hii kwa mashariti nafuu ili vijana wahitimu wajiajiri, nijukumu la serikali kutoa elimu kuhusu hiyo mikopo badala yake serikali imeigeuza mikopo hiyo kuwa mikopo ya vyama vya siasa kiasi kwamba haiwafaidishi vijana badala yake vijana wa vyama hasa kilichopo madalakani huikopa fedha hio kinyume na malengo waliyoyaambatanisha hivyo mikopo hiyo ielekezwe kwenye makundi ya vijana wanaohitimu.

# Serikali ya viwanda.
Chanzo: https://www.tanzania.go.tz/egov_uploads/documents/Sustainable-Industries-Development-Policy_sw.pdf

Hii ilikuwa sera na wimbo wa serikali iliyoingia madarakani 2015 lakini serikali hii imeshindwa kuifanyia kazi sera hiyo badala yake imekuwa serikali ya ndege na serikali ya MAKATO, Fikilia serikali ingeamua kulivalia njuga swala hili Tanzania tungekuwa tumepiga hatua kiasi gani, tunakaribia kila kitu kinachoweza kutufanya tusiwe masikini, Tuna Ardhi nzuri, Madini, Maziwa, Bahari, Utalii, Marisho ya mifugo na rasilimali watu, kwanini kwenye sera hiyo serikali isingeamua kujenga mitalo ya kilimo cha umwagiliaji kwa mikoa inayoruhusu kufanya hivo? kwanini vijana na wawekezaji wa ndani wasingepewa vipaumbele na mikakati ya kuanzisha viwanda? Sera bila uelekeo ni sawa na kuwa na ramani bila dira.
#Sarafu za kidijitali pamoja na Forex

#Umiliki wa shule za awali, msingi na vituo vya kufundishia. vijana wengi wahitimu hasa kada ya Ualimu walitakiwa wawe wanufaika hapa, lakini serikali imeweka kibano hapa, juu ya Mitaji takiwa kwenye uanzishaji na Mashariti kwa ujumla, hivyo vijana wengi tunashidwa kumdu gharama hizo hivyo tunabaki kutegemea ajira za serikalini Lai yangu kwa serikali ifanye mapitio ya Mtaji na Sheria zingine juu ya uanzishaji na umiliki wa shule hizi mfano Badala ya kupeleka benki statementi yenye millioni 62 kwa Afisa Elimu kiongozi waweke shariti la angalau nusu ya hio fedha.
Chanzo: Kuanzisha Shule ya Msingi na Sekondari: Utaratibu wa Kiserikali, Ushauri, Changamoto na Faida


Hitimisho, Kuna sera mbovu kwenye Michezo, kilimo, masoko, utandawazi, sayansi na utafiti ambazo ndizo nyanja kuu kwa ukombozi wa kijana wa kitanzania.

NAWASILISHA.
 
Unafikiria solution gani kwa wazo lako
Asante Ndugu! Mosi, Masharti na sheria za kusajili na kuanzisha Maudhui mtandaoni yawe jumuishi kwa mana kwamba yahusishe walengwa kwa asilimia zote pia yaangalie uhalisia wa mazingira ya kitanzania fikilia ni wahitimu wangapi wanauwezo wa kuweka akiba hata milioni mbili ili wakitoka waitumie kama mtaji, tuache wanaopokea mikopo ya elimu ya juu, tuchukulie Watu wa cheti na Diploma
Pili, Hakuna ulazima wa kusoma miaka zaidi ya 15 ( Formal education) haliyakuwa life span yenyewe ni miaka 50 hivyo tuseme umeandikishwa darasa la kwanza ukiwa na miaka 7 hivyo utahitimu shahada ya kwanza ya miaka mitatu ukiwa na miaka 23 hivyo unakuwa na miaka kama 25 au 28 ya uzalishaji, ambayo kimsingi ni kidogo, pia elimu yetu ni nadhalia sana badala ya vitendo, mazingira ya ujifunzaji haya mshawishi mwanafunzi kuwa mvumbuzi fikilia ni shule ngapi zenye hata hizo maabara za hovyo!??
Nafikili utakuwa umepata point to start with!
 
Tunavote namnagani mkuu?
Ok! Mwishoni mwa uzi kuna sehemu kuna kialama cha kupanda na kushuka kumeandikwa idadi ya kula una gote kwa kukibofya kialama hiko! kialama kama cha hivi ( > ) lakini chenyewe kimekaa kwa kusimama au kushuka ukibofya hicho unakuwa umepiga kula au kupunguza kula uliyokwisha piga.
 
HAYO MAMBO YAPO SANA WEWE FIKILIA HAYA MAKATO YA MIAMALA YALIVYO VIJANA TULIKITAA KUFANIKIWA KWETU KUGUMU UKIKATIZA HUKU SERIKALI INAWEKA KIKWAZO
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom