Sera na Maamuzi ya serikali vinarudisha nyuma maendeleo ya kilimo Tanzania

Manelezu

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
1,510
2,000
Nimetafakari kwa muda sana baada ya mimi binafsi kuamua kujiingiza kwenye kilimo kama mkakati wa kujiajiri na kuajiri watu wengine. Kama kijana wenye uelewa na nilipata elimu nzuri na kupambana na tatizo la ajira, kilimo ingekuwa njia nzuri ya kunikomboa, bahati mbaya sana naona maamuzi ya serikali kwenye kilimo yanaturudisha nyuma nap engine kutukatisha tamaa.

Leo unawekeza mtaji, na labda unakopa vifaa vya kilimo unaamua kulima kisasa kabisa kwa mfano zao la mpunga ambalo binafsi niliamua kulima. Pembejeo ziko juu, na gharama zingine za uzalishaji. Kwa mfano kama unaamua kulima kilomo cha kisasa mvua zinapokata inabidi kutumia mafuta ku pump maji kwenye mashamba. Zote hizi ni gharama za uzalishaji na zitarudi pale utakapokutana na bei nzuri ya soko.

Kwa bahati mbaya sana serikali imekuwa ikifanya juhudi kudhibiti bei na kumdhibi mkulima, kwa lugha nyingine serikali inanyonya watu wake yenyewe. Inafikia sehemu tunasikia kauli kwamba chakula kisitoke nje ya mkoa kwenda mkoa mwingine. Maamuzi ya aina hii hayana tija na hayawezi saidia kukuza kilimo.

MAOMBI:

Serikali iache soko huru. Ipunguze excessive regulation ya bei na soko. Unaweza kukuza kilimo pale kunapokuwa na uhakika wa soko na bei. Mkulima atafute soko la nje kama soko la ndani si zuri. Auze mazao yake sehemu yoyote ile anayoona itamlipa.

Pia serikali isaidie kupunguza gharama za uzalishaji kwa kuweka miundombinu ya umwagiliaji na kukodisha kwa vijana walioamua kujiajiri kwa bei nafuu ili gharama za uzalishaji zisiwe kubwa.
 
maganjwa

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
2,300
2,000
ndo umejua vizur baada ya kwenda kwenye field akili za kuambiwa changanya na zako tulikuwa tunasema siku nyingi sana kwamba serikali hii haijali wakulima
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
30,752
2,000
ndugu mleta mada ndio umejua leo? angalia signature yangu ndio ujue wenzio tuliona lini hili tatizo.
 
Manelezu

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
1,510
2,000
ndugu mleta mada ndio umejua leo? angalia signature yangu ndio ujue wenzio tuliona lini hili tatizo.
Its a serious problem. serikali ijipange kusaidia kukua kwa kilimo. Inakatisha tamaa sanaa
 
gogo la shamba

JF-Expert Member
Mar 1, 2013
6,675
2,000
mtafahamu kidogokidogo maana akili zenu bado ni za ndio tu,mpaka yawakute nyinyi ndio maana mlikuwa mnafurahia kuona mapambano kati ya watu wasikuwa na silaha na watu wenye silaha za vita na mkajitayarisha kushangilia ushindi mkifikiria kwamba watakaouwawa hawatokuwa na uhusiano wowote na nyinyi. ndio maana nasema mtaelewa tu,mambo yatakuwa magumu kwetu na yatafika kwenu hapo ndipo mtakapoelewa maana yatakuwa yamearibika kabisa ingawa sisi tunajitahidi kutoa ujumbe hili yasifike huko
 
Kilimo kinaweza leta tija kama kuna maamuzi yenye tija. Kwa mtazamo wangu kilimo kina fursa sana kama serikali itasaidia. Si kuwa na maamuzi ya kumkandamiza mkulima
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom