Sera Mpya ya Habari - Je ni kwa ajili ya kumbana Mengi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sera Mpya ya Habari - Je ni kwa ajili ya kumbana Mengi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by NgomaNzito, May 29, 2009.

 1. NgomaNzito

  NgomaNzito JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 561
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wadau wa habari wayakataa mapendekezo ya sera mpya ya habari Tanzania


  WADAU wa sekta ya habari nchini jana walikataa mapendekezo ya sera mpya ya habari na kuunda kamati itakayokusanya maoni kabla ya kuwasilisha rasimu mpya ya sera ya rasnia hiyo.

  Mapendekezo ya sera hiyo yaliwasilishwa jana kwenye mkutano wa wadau ulioitishwa na Idara ya Habari (Maelezo) kwenye Ukumbi wa Karimjee kwa lengo la kuboresha sera ya mwaka 2003, lakini ikakutana na upinzani mkali kutoka kwa wanahabari na wadau wengine.

  Wadau hao walikosoa uandishi wa sera hiyo, nia ya kuitoa sasa, maboresho yaliyoongezwa kwenye sera ya mwaka 2003 na vipengele kadhaa, hasa cha umiliki na hivyo kukubaliana kuunda kamati ambayo itakutana tena na wadau wa sekta hiyo ndani ya kipindi cha miezi mitatu.

  Akiongoza mjadala huo mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Clement Mshana alikubaliana na hoja za wadau kuwa isingekuwa rahisi kujadili sera hiyo yote katika muda mfupi baada ya mapendekezo hayo ama kuchelewa kuwafikia walengwa na hivyo kukosa muda wa kuisoma kabla ya kuijadili.

  "Sera hii ya mwaka 2003 ilitolewa baada ya mchakato mrefu sana," alisema mhariri wa Nipashe, Jesse Kwayu. "... kwa hiyo ndugu mwenyekiti, kama kuna nia ya kuweka sera mpya ya habari, basi hatuna budi kukubali kufuata mchakato mwingine.

  "Tupewe mapendekezo haya, halafu watu waingie mtaani kwenda kutafuta ushauri na baadaye turudi tujadili kwa kina ili tutoke na kitu kizuri."  Wajumbe wengine watatoka vyuo vikuu vya uandishi wa habari na vyama vya siasa, Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Idara ya Habari (Maelezo) na asasi zisizokuwa za kiserikali.

  Katika mjadala huo, moja ya masuala makubwa yaliyotawala ni kipengele namba 2.3.2 ambacho kinataka mtu mmoja asimiliki vyombo vingi vya habari, sera iliyotafsiriwa na wajumbe kuwa inamlenga mtu mmoja tu.

  Sera hiyo inataka mtu mmoja asimiliki vyombo kama televisheni, redio au magazeti kwa wakati mmoja kwa maelezo kuwa anaweza kutumia vibaya na kuathiri jamii.

  Mhadhiri wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Sengondo Mvungi alipinga kipengele hicho akisema kuwa kinalenga kumdhibiti mtu mmoja(MENGI) badala ya kushughulikia tatizo.

  Mvungi, ambaye pia alikosa uandishi wa sera hiyo, alisema hakuna sababu za kuzuia watu kumiliki zaidi ya chombo kimoja kwa kisingizio hicho cha kuogopa kuwa anaweza kutumia vibaya vyombo vyake.

  Mvungi, ambaye ni mmoja wa wadau wakubwa wa tasnia ya habari, pia alisema kitendo cha kipengele cha 2.3.2 kinachotaka wawekezaji kutoka nje wafuate sera hiyo badala ya ile ya Kituo cha Uwekezaji (TIC) na kwamba raia wa nje wanaweza kuwekeza katika chombo cha habari kwa ubia na raia, ili mradi hisa za Mtanzania zisiwe chini ya asilimia 51, si sahihi.

  Mvungi alisema haoni sababu za suala la umiliki wa vyombo vya habari liondolewe kwenye sheria iliyopo na inayofanya kazi vizuri ya TIC na kuipeleka chini ya sera ya habari.

  Wadau wengine walihoji sababu za serikali kutaka kumiliki umiliki wa vyombo vya habari wakati tayari imeshakiri kuwa tasnia ya habari ni biashara kama zilivyo nyingine.


  "Kama tumeshasema kuwa vyombo vya habari ni biashara, kwa nini tuanze kuwekeana masharti," alihoji mpiga picha mkuu wa Mwananchi, Mpoki Bukuku.

  "Waachieni watu wamiliki vyombo vya habari kwa kadri ya uwezo wao. Tena wamiliki wengi wa vyombo hivi ni wazalendo na hivyo wamesaidia sana kutoa ajira, ndio maana mnatuona sisi wengine tuko hivi."

  Naye mwandishi wa The Express, Freddy Okumu alisema hakuna utafiti wowote ulioonyesha kuwa mtu mwenye vyombo vingi vya habari aliweza kutumia vyombo vingi na kunufaika.

  Alitoa mifano ya baadhi ya watu walioanzisha magazeti wakati wakigombea ubunge, lakini wakashindwa na watu ambao hawakuwa na hata chombo kimoja cha habari.

  Pia alizungumzia baadhi ya kampuni zinazozalisha bidhaa na hazimiliki chombo chochote cha habari, lakini zikaweza kufanya vizuri kuliko bidhaa kama hiyo inayozalishwa na wafanyabiashara wenye vyombo vya habari.

  Naye kiongozi wa chama cha siasa cha NLD, Emmanuel Makaidi alisema ni vyema serikali ingewapongeza wafanyabiashara wenye vyombo vingi vya habari badala ya kutafuta mbinu za kuwabana kwa kuwa wamesaidia kukuza demokrasia.
  Badala yake, Makaidi alisema sera inatakiwa idhibiti wanasiasa na viongozi wa serikalini kumiliki vyombo vya habari.


  MFANYABIASHARA maarufu wa jijini Dar es salaam, Reginald Mengi amedai kuwa alibanwa na vyombo vya dola baada ya kutangaza hadharani majina ya watu watano wanaotuhumiwa kwa vitendo vya ufisadi, akiwabatiza jina la mafisadi papa.

  Mengi, ambaye anamiliki vyombo tofauti vya habari, alibainisha hayo jana wakati akitoa mchango wake juu ya sera mpya ya habari kwenye mkutano wa wadau wa habari ulioitishwa na Idara ya Habari (Maelezo) kwenye Ukumbi wa Karimjee.

  "Baada ya kutangaza majina ya watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi, niliitwa na (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa), Takukuru na kuambiwa kwa nini nisichukuliwe hatua kwa kitendo changu," alisema Mengi.

  "Niliitwa pia na Maelezo na kuambiwa kwa nini nisichukuliwe hatua; niliitwa na (Mamlaka ya Mawasiliano) TCRA. Kote huko niliulizwa kwa nini nisichukuliwe hatua."

  Mengi pia alisema kuwa alielezwa kwenye taarifa yake ya kutaja watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi kulikuwa na chembechembe za ubaguzi wa rangi na kutakiwa kutoa maelezo.
  "Siku hiyo ndipo nilipojua kuwa kumbe ufisadi una rangi," alisema Mengi.

  Mwananchi
   
 2. M

  Mmongolilomo Senior Member

  #2
  May 29, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Pole Mengi dunia ndivyo ilivyo na sisi ndio watu wake
   
 3. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Katika mjadala huo, moja ya masuala makubwa yaliyotawala ni kipengele namba 2.3.2 ambacho kinataka mtu mmoja asimiliki vyombo vingi vya habari, sera iliyotafsiriwa na wajumbe kuwa inamlenga mtu mmoja tu

  Kawaida ninavyofahamu ni kuwa hii sera ya habari si kwa ajili ya watu habari peke yao bali inatengenezwa ili kukidhi mahitaji ya jamii nzima.

  Ni kweli kabisa vipengele vingine vitaonekana haviwafurahishi watu wa habari lakini ni muhimu viwepo kwa ajili ya kuwalinda kundi jingine la watu. Watu wa habari wasiangalie jambo hili kwa upande wa maslahi yao bali wajue kuwe ni suala la kitaifa na linatakiwa liwaguse watu wote.

  Sababu ambazo hadi sasa watu wa habari wanazozitoa hazina nguvu kwani hakuna hata moja inayoonesha kuwa wanataka pia kulinda haki za watu wote. Sera haijakataza kutokuwepo kwa TV, Radio, au magazeti bali inataka kuwe na mgawanyo ambao hautaleta athari kwa wananchi endapo mmiliki atakuwa na nia mbaya dhidi ya jamii. Ikumbukwe kuwa uandishi wa habari unaweza kutumiwa kama silaha nyingine yeyote na kuleta madhara makubwa kama hakutakuwa na sera nzuri.

  Ni vema tukaweka tamaa nyuma na kuweka mustakabali wa nchi hii kwa miaka mingi ijayo.
   
 4. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mzee Mengi usife moyo. Dunia ni tambarare ila mabonde na milima yamo rohoni kwa watu.
   
Loading...