Sera mpya ya Elimu yasubiri idhini ya Baraza la Mawaziri

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,357
8,062
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema mabadiliko makubwa kwenye elimu yanakuja.

Alisema Rais Samia alitaka Wizara ya Elimu kufanya mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 ambayo ilitungwa wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne.

“Sera iliyopo haijatekelezwa ambayo ilifanyiwa mapitio, elimu ya msingi mpaka darasa la sita, sekondari miaka minne ili mwanafunzi akae shuleni miaka 10,” alisema na kuongeza:

“Mabadiliko kwenye elimu yanakuja na yajayo yanafurahisha, tutapitisha kwenye Baraza la Mawaziri ili tupate kibali.”
 
Ndio Maisha yalivyo mkuu

Aliye madarakani ndio anang'aa hata ndo ungekuwa wewe namba moja WA inchi ungepata maujiko
ila huu ni utamaduni mbovu wa waafrika. Ni aina ya plaigarism.

Hata makazini tuna hayo mambo, mfanyakazi anafanya jambo zuri halafu mkuu wake wa kitengo anaenda kusema kwa bosi kuwa yeye ndio kafanya hiko kitu ili apate ujiko wote, ila mfanyakazi akiharibu lawama zote zinaenda kwa huyo mfanyakazi.

Nilifanya kazi na wazungu nikagundua wao hawana hiko kitu...yani hata utoe mchango mdogo kiasi gani lazima aku'acknowledge kwa mabosi kuwa hiki kitu fulani alichangia.
 
Sera aliyoanzisha magufuli saivi inaitwa sera ya samia na pongezi zote zinaennda kwa samia...jaman🙆
Sera ipi hiyo mkuu aliyoianzisha jpm na kupewa samia?!!! Ipo hapo kwenye mada au unayo tu mwenyewe? maana kwenye mada naona imesemwa kabisa sera ya 2014 ambayo ilianzishwa wakati wa serikali ya awamu ya nne ndiyo samia kaagiza ipitiwe.

Lakini, tukiamua kuwa wakweli, mbona flyovers kwa sasa nchi nzima inatangazwa kuwa ni kazi ya jpm wakati KWA MACHO YANGU nilishuhudia ile ya tazara ikipimwa wakati wa jk?!!!! Dah, hiyo siku ya hukumu kutakuwa na kazi kubwa sana na mishangao ya watu!!
 
Baby Class
Middle Class
Pre Unit
Primary
Secondary
High School
University

Jumla miaka 20-23
 
Back
Top Bottom