Nchi yetu imefikia hatua sera ya nchi inaweza kutungwa ili kutatua matatizo ya familia ya waziri. Inasadikiwa Mungai alikuwa na watoto walioshindwa Sayansi ya sekondari, akaamua kuyaunganisha masomo.
Bodi ya mikopo ya elimu ya juu ilipigwa shinikizo kwa mwaka mmoja kuwapa mikopo wanafunzi wasome digrii za masters ili watoto wa waziri wapate nafasi. Baada ya mwaka mmoja wakasema hapana!
Bodi hiyo hiyo iliyolenga watoto wasio na uwezo vyuo vya serikali, ikasema sasa ni walioshinda sayansi, kiongozi mmoja akaona watoto wake wameachwa nje akasema hapana! Wote ni watanzania wapewe mikopo bila kujali ni University ya serikali au hapana.
Sasa Waziri huyu kaja na sera mpya. Ukiiangalia utadhani kuna kitu, lakini inakuja kuwabagua watoto wa maskini na matajili watakaosoma private schools.
Miaka 6 sawa lakini hawasemi 7 iliharibu nini? Umri wa kuanza umeshushwa na sera lakini hawasemi akianza na miaka 7 kuna shida gani na kwa nini ilikuwa 7?
Watoto wa waziri watasoma private je, watoto wa mwanakijiji kule chini atapata wapi sekondari ya kubeba watoto wote walioko primary? Sasa hivi kuna sekondari ambazo kwa miaka 20 hazijawahi kupata mwalimu wa hisabati! Yaani sera irekebishe ubora wa elimu kizembe kiasi hiki?
Nasikitika kuona kwamba waziri wa elimu ni profesa. Au ni wale wanaoamini anajua sana kiasi kwamba wengine hawamuelewi? Kichwa cha mwendawazimu.