Sera mbovu kwa fao la kujitoa kwa vijana

Witmak255

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
3,264
5,403
Nina mpango wa kuachana na utumishi wa umma hivi karibuni baada ya kuitumikia serikali Kama mhandisi wa mifumo ya computer kwa miaka5 Sasa Leo nilienda ofisi za NSSF Kinondoni ( nilikuwa mwanachama huku kabla ya mifuko kuunganishwa) kujua namna ya kupata pesa zangu baada ya kuresign kazi,
Nilikuta watu wapo wengi hasa vijana na watu wa makamo kwa namba Ni wachache kuliko vijana. Ilibidi nifuate utaratibu ili ifike zamu yangu nihudumiwe huku napiga stori na vijana wenzangu kuhusu majibu wanayopewa na wahudumu, juma Ni kijana aliyeacha kazi ya ulinzi KK baada ya kufanya miaka3 na ushee na anasema ana 2m+ kwenye mfuko wa nssf na anahitaji achukue ili aende kuanzisha biashara ya dagaa kwao mwanza but kufika pale wahudumu wamemwambia kwa sababu kaacha kazi inaonekana Hana uhitaji na pesa hivyo asubiri afike miaka55 au akipata kazi nyingine aunganishe michango yake alipoishia," very sad" Hawa jamaa wameua malengo na ndoto za juma jamaa anaongea kwa huzuni mpka una mhurumia, kila aliyekuwa pale nje ya ofisi ukimtizama wote wanaonesha sura za kinyonge, nikamsogelea mama mmoja mtu mzima Sana nikamsalimia.
Nikamdadisi alichoambiwa huko ndani, "ananiambia mwanangu nimestaafu tangu 2016 mwezi wa8 mpka Sasa sijapewa MAFAO yangu, kila siku nikija wananizungusha na hapa nilipo sijala, mfukoni nilikuwa na buku3 na kwa vile nilikuwa na pesa tigopesa haukuwa shida nikampa mama kale.
Ikafika zangu yangu nikaenda pale ndani nikawaelezea, wakaniambia "wewe mtumishi wa umma unaacha kazi wewe ndo huna shida na pesa kabisa na kwa taratibu za Sasa inabidi uje baada ya kufikisha miaka 55", just imagine now Nina 28 yaani miaka 27ijayo ndo niifatilie 10mill. Sikuona haja ya kujibishana nao kwa sababu nshakamilisha taratibu za kujilipua nje ya nchi zisije kutibuka bure maana unaweza kuwajibu vibaya ukajikuta uko central?
Ni kwa Nini Hawa watunga Sera wanatuwekea limitations kwenye pesa zetu ikiwa wao wakistaafu wanachukua zote?, Hizi Sera za hii mifuko Zina ustawi kwa maisha ya vijana, au ndo tunalazimisha kufanya kazi hata Kama hazilipi mpaka mda wa kustaafu?

Kama wastaafu walivyocharuka kikokotoo Chao kikarudishwa, vijana na nyie pigeni kelele kwenye hili fao la kujitoa Hawa jamaa wanataka kuuawa malengo yetu.
 
Hili ndio tatizo la kuwa na watetetea matumbo wengi ndani ya chama. Hawa kazi yao ni kuitikia NDIOooooo hata kwenye BIG NO.
 
Hizi ni Sera kipumbavu sana
Kwa kifupi insmfanya Kijana wa kitanzania awe na akili ya kuajiliwa hadi mwaka.
Ndo maana Mimi sitaki Kazi ya kuajiliwa ni bora niendelee kuchoma maandazi na kachori

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asichojua Magufuli ni kuwa hiyo sheria itasababisha mambo mawili kwa wakati mmoja.
1. Serikali na mashirika ya umma yatashindwa kushawishi best talents kuajiriwa na wao; na
2. Mifuko ya pension itakosa contributions toka private sector (nikitaka kum-retain a talented personnel nitaingia nae contract ambayo hatalazimika yeye wala mimi kuchangia nssf).

Management sio maguvu ni mostly akili na maarifa.
 
Asichojua Magufuli ni kuwa hiyo sheria itasababisha mambo mawili kwa wakati mmoja.
1. Serikali na mashirika ya umma yatashindwa kushawishi best talents kuajiriwa na wao; na
2. Mifuko ya pension itakosa contributions toka private sector (nikitaka kum-retain a talented personnel nitaingia nae contract ambayo hatalazimika yeye wala mimi kuchangia nssf).

Management sio maguvu ni mostly akili na maarifa.
Kuyajua hayo yanahitaji uwe kipanga.
 
maana kama mfumo unalalamikiwa na watu basi haufai na pia kwann umzuie hela ya mtu eti mpk afikishe miaka 55 je akifa kabla ya huo umri.??
kuna haja ya watanzania kuamka kupinga vitu km hivi.ht wajukuu watakuja kutuona mabogasi kbsaa
 
Back
Top Bottom