Sera mbadala ya elimu: Serikali anzisheni bima ya elimu

Sijakuelewa unaposema pesa itumike kama security for loan!Sijawahi ona hii,labda unaweza nifafanulia kidogo hapo!

Suala la pili,kama kila mzazi atamchangia mtoto wake na mtoto atapata elimu kulingana na mchango wa baba,vipi kama baba akikata uzi njiani?Tuseme mzazi amefariki akiwa amechangia mwaka mmoja tu,hizi gharama anabeba nani?

NB:Changamoto kubwa za gharama za masomo zipo elimu ya juu na si msingi mpaka sekondari!

Mimi nakumbuka nilisoma shule za serikali mwanzo mwisho!Gharama yangu kwa miaka 6 yaani form 1 mpaka 6 ilikuwa sh 420,000/-!Hiyo ndiyo karo mzee wangu alilipa kwa miaka 6,yaani 70,000 kama karo kwa mwaka tena boarding school!
Lakini nilipoingia chuo,ada pekee kwa mwaka ilikuwa 1.5M,bado accomodation ,examination fee,chakula,stationary,field vyote hivi kwa mwaka vilikuwa vinachukua kama mil 3!So kwa mwaka wa masomo mil 4.5 ilikuwa lazima iwepo!

Hapo utaona changamoto kubwa ilipo!
kwenye security for loan, namaanisha loan from bodi ya mikopo ya elimu ya juu. itafanyikaje? kama mzazi kachangia pesa zake kwenye bima ya elimu na mzazi akastaafu ama kupoteza maisha kabla mtoto hajamaliza elimu yake ya msingi na upili, pesa za kwenye bima zitatumika kugharamia elimu yake kwa upande wa msingi na sekondari kwa shule za sekondari za serikali ambazo kimsingi zitatosha kabisa kugharamia .

kama mzazi amefariki serikali inabidi kucover gharama za elimu ya mwanafunzi huyu na akifika chuo awe preferred kwenye mikopo ya elimu ya juu.

tatizo linakuja elimu ya juu , kiasi cha pesa kwenye bima yako kinaweza kisitoshe serikali inaweza kutumia bima yako kukupa mkopo wa elimu ya juu kwa kuwa bima ni uwekezaji wa kudumu kwa hiyo serikali itakuwa inakata pesa zake walizokupa taratibu kwenye bima yako mpaka mkopo wako uishe na kama itashindikana basi wanakata na sehemu ya mshahara wako
 
So uchangiaji huu uwe wa pamoja,sivyo?Yaani hakuna aliyetoa kingi wala kidogo!Kwa maana hiyo huu unakuwa mfuko wa pamoja,angalizo tu ni kuwa je itawezekana?Kila mzazi,mwenye watoto 6 na mwenye mtoto mmoja ataweza kumlipia mwanaye?

Nikupe mfano rahisi!
Kwa elimu ya juu,wastani wa gharama za mwanafunzi ni kati ya mil 3-mil 5 kulingana na faculty!Tuchukulie 4m kama mean,kwa miaka mitatu ni mil 12,na wale miaka 4 ni mil 16!Tusema una watoto 3,kila mmoja kwa maana hiyo kwa elimu ya juu uchangie mil 36!Wangapi wataweza?

Sidhani kama tunaelewana,wote tukilipa 2% ya tunacho earn,regardless wewe ni mkulima au mfanysbiashara au mfanyakazi then yes we can ALL afford kuwasomesha vijana WOTE,,,mkuu sikuelewi hivi umefikiria tu kuwa na watoto sita,je umefikiria kuna familia nyingine au niseme watu wengine hawatabahatika kuwa na watoto??
 
kwenye security for loan, namaanisha loan from bodi ya mikopo ya elimu ya juu. itafanyikaje? kama mzazi kachangia pesa zake kwenye bima ya elimu na mzazi akastaafu ama kupoteza maisha kabla mtoto hajamaliza elimu yake ya msingi na upili, pesa za kwenye bima zitatumika kugharamia elimu yake kwa upande wa msingi na sekondari kwa shule za sekondari za serikali ambazo kimsingi zitatosha kabisa kugharamia .

kama mzazi amefariki serikali inabidi kucover gharama za elimu ya mwanafunzi huyu na akifika chuo awe preferred kwenye mikopo ya elimu ya juu.

tatizo linakuja elimu ya juu , kiasi cha pesa kwenye bima yako kinaweza kisitoshe serikali inaweza kutumia bima yako kukupa mkopo wa elimu ya juu kwa kuwa bima ni uwekezaji wa kudumu kwa hiyo serikali itakuwa inakata pesa zake walizokupa taratibu kwenye bima yako mpaka mkopo wako uishe na kama itashindikana basi wanakata na sehemu ya mshahara wako
Utaratibu wa sasa,bado watu wanakopeshwa na kuja kulipa mkopo kupitia mishahara au biashara zao wanapokuwa wamesajiliwa kama walipa kodi TRA!
Sasa tofauti inakuwa wapi kama bado mtu anakopeshwa kwa ajili ya elimu ya juu?Huko ndiko kwenye changamoto,huku kwingine asilimia kubwa ya watanzania wanamudu!
Ukiangalia hata nchi za watu,college ndio sehemu yenye changamoto ya gharama ya elimu!
Utekelezaji wa education fund hiyo utakuwa hauna maana kama sehemu yenye kikwazo haijaguswa!
Na niseme,kumpa mzazi mzigo wa kuchangia gharama za elimu ya juu kwa mtoto kwa kumkata mshahara itakuwa kumuongezea maumivu!
Baba mwenye watoto wanne utamkata asilimia 20,bado achangie 20% Nssf,akatwe kodi kwenye mshahara,akatwe NHIF ya watoto wanne,hapo anabaki na nini??????
 
Sidhani kama tunaelewana,wote tukilipa 2% ya tunacho earn,regardless wewe ni mkulima au mfanysbiashara au mfanyakazi then yes we can ALL afford kuwasomesha vijana WOTE,,,mkuu sikuelewi hivi umefikiria tu kuwa na watoto sita,je umefikiria kuna familia nyingine au niseme watu wengine hawatabahatika kuwa na watoto??
So hii kila mtu atachangia regardless ana mtoto au la?
Tuseme unapata mil 1!Asilimia 2 ni sawa na 20,000!
20,000×12=240,000(mwaka)
240,000×30=7.2 Milion(miaka 30 ya utumishi)

Hapo nimechukulia mshahara wa kiwango cha juu!
Sasa kama kila mzazi atazaa mtoto mmoja na kuchangia kiwango hicho,pesa hiyo haitoshi kumsomesha mtoto elimu ya juu!
Mil 7.2 ni ndogo kwa elimu ya juu!
Kwa muda mfupi mambo yataonekana shwari,in the long run mifuko hii itakauka na tutashikana uchawi!
 
Utaratibu wa sasa,bado watu wanakopeshwa na kuja kulipa mkopo kupitia mishahara au biashara zao wanapokuwa wamesajiliwa kama walipa kodi TRA!
Sasa tofauti inakuwa wapi kama bado mtu anakopeshwa kwa ajili ya elimu ya juu?Huko ndiko kwenye changamoto,huku kwingine asilimia kubwa ya watanzania wanamudu!
Ukiangalia hata nchi za watu,college ndio sehemu yenye changamoto ya gharama ya elimu!
Utekelezaji wa education fund hiyo utakuwa hauna maana kama sehemu yenye kikwazo haijaguswa!
Na niseme,kumpa mzazi mzigo wa kuchangia gharama za elimu ya juu kwa mtoto kwa kumkata mshahara itakuwa kumuongezea maumivu!
Baba mwenye watoto wanne utamkata asilimia 20,bado achangie 20% Nssf,akatwe kodi kwenye mshahara,akatwe NHIF ya watoto wanne,hapo anabaki na nini??????
bima ya elimu ya mtoto ndio itatumika kama security for higher education loan na kama kwenye bima yake kutakuwa na pesa ndogo ya kushindwa kulipa gharama za elimu ya juu, serikali itampa mkopo na bima yake itatumika kama security na kwa kuwa bima ya elimu itakuwa ni ya kudumu kwa maana anaweza kutumia mtoto na mjukuu basi unakuwa ni kama uwekezaji na katika uwekezaji mwekezaji anategemea faida basi mwenye bima akipata faida yake serikali itaichukua hiyo faida kama njia ya kurudisha mkopo wa elimu ya juu
 
So hii kila mtu atachangia regardless ana mtoto au la?
Tuseme unapata mil 1!Asilimia 2 ni sawa na 20,000!
20,000×12=240,000(mwaka)
240,000×30=7.2 Milion(miaka 30 ya utumishi)

Hapo nimechukulia mshahara wa kiwango cha juu!
Sasa kama kila mzazi atazaa mtoto mmoja na kuchangia kiwango hicho,pesa hiyo haitoshi kumsomesha mtoto elimu ya juu!
Mil 7.2 ni ndogo kwa elimu ya juu!
Kwa muda mfupi mambo yataonekana shwari,in the long run mifuko hii itakauka na tutashikana uchawi!
hao watoto watatumia bima kuombea mikopo na kwa kuwa serikali itakuwa imetumia pesa za bima.kwenye uwekezaji wenye faida zaidi basi waombaji mkopo wataweza kupatiwa mkopo kwa asilimia kubwa na kupelekea changamoto ya ukosefu wa mikopo ya elimu ya juu kutatuliwa zaidi
 
Utaratibu wa sasa,bado watu wanakopeshwa na kuja kulipa mkopo kupitia mishahara au biashara zao wanapokuwa wamesajiliwa kama walipa kodi TRA!
Sasa tofauti inakuwa wapi kama bado mtu anakopeshwa kwa ajili ya elimu ya juu?Huko ndiko kwenye changamoto,huku kwingine asilimia kubwa ya watanzania wanamudu!
Ukiangalia hata nchi za watu,college ndio sehemu yenye changamoto ya gharama ya elimu!
Utekelezaji wa education fund hiyo utakuwa hauna maana kama sehemu yenye kikwazo haijaguswa!
Na niseme,kumpa mzazi mzigo wa kuchangia gharama za elimu ya juu kwa mtoto kwa kumkata mshahara itakuwa kumuongezea maumivu!
Baba mwenye watoto wanne utamkata asilimia 20,bado achangie 20% Nssf,akatwe kodi kwenye mshahara,akatwe NHIF ya watoto wanne,hapo anabaki na nini??????
mzazi hakatwi kwenye mshahara wake kwa ajili ya mkopo mtoto wake, mtoto atakuja kukatwa baadae kabisa. tumeona ni namna gani serikali inakopesha watu lakini hawalipi mikopo, bima itatumika kutatulia matatizo ya mikopo kama haya kwa sababu uwekezaji kwenye bima utafanyika hatakama mlengwa atakuwa amekufa
 
So hii kila mtu atachangia regardless ana mtoto au la?
Tuseme unapata mil 1!Asilimia 2 ni sawa na 20,000!
20,000×12=240,000(mwaka)
240,000×30=7.2 Milion(miaka 30 ya utumishi)

Hapo nimechukulia mshahara wa kiwango cha juu!
Sasa kama kila mzazi atazaa mtoto mmoja na kuchangia kiwango hicho,pesa hiyo haitoshi kumsomesha mtoto elimu ya juu!
Mil 7.2 ni ndogo kwa elimu ya juu!
Kwa muda mfupi mambo yataonekana shwari,in the long run mifuko hii itakauka na tutashikana uchawi!

Uko sahihi mkuu 7.2 ni ndogo,

I guess tuchangie 2% kila household ila kiwango kinachobaki serikali ijazie,,,

Au la,

Fees zote kuanzia primary,secondary,chuo ziwe calculated,then igawanywe kwa watu wote,hio 2% ni yangu,labda tukishacalculate kila kitu inawezekana tukatakiwa kulipa each 4%!,,,
 
Ugomvi utaanzia hapo. Kwa nini nilazimishwe kuchangia bima ya elimu kwa mtoto hewa?

Kodi wanikate kwenye mshahara, na bima ya elimu wakati sina mtoto?

Serikali itakuwa imewachoka wafanyakazi to the maximum.
Nilikua sijasoma vizuri ina maana anapendekeza mfanyakazi tena ambaye hajaongezewa mshahara wake akatwe tena? Huyu mtu ana akili timamu kichwani?
 
Ndo hivyo mkuu.
Kuna watu wana utani wa ngumi mkuu.
Yaani mshara miaka mitatu haujaongezwa, makato kibao halafu kuna mtu anafikiria kuniongezea makato!

Lengo la elimu bure ni kuwasaidia hata wale wasioweza kulipiwa na wazazi/walezi nao wapate elimu.

Ukimlazimisha achangie bima ya elimu sijui atazitoa wapi hizo pesa.
 
Watakaofaidika ni wanao na vitukuu vyako ...kutokua na familia sasa hivi au bachelor kusikuhadae!
Naamini humaanishi unachokisema.
Wapeni watu elimu wajue umuhimu wa kuweka akiba benk hata kabla ya kuwa na familia. Habari ya kuwachangisha hata wasio na wa kusoma ni uonevuv na wizi. Ada analipa mzazi/mlezi, sio kila mtu.
 
Uko sahihi mkuu 7.2 ni ndogo,

I guess tuchangie 2% kila household ila kiwango kinachobaki serikali ijazie,,,

Au la,

Fees zote kuanzia primary,secondary,chuo ziwe calculated,then igawanywe kwa watu wote,hio 2% ni yangu,labda tukishacalculate kila kitu inawezekana tukatakiwa kulipa each 4%!,,,
Hamuitakii mema serikali itakayokuwepo
 
Nimesoma kilichoandikwa na kuelewa!Ndio maana nakuuliza,unafahamu maana ya Bima??Kwa mujibu wa uliyoandika ni wazi hujui maana ya Bima!
Insurance is a means of protection from financial loss. It is a form of risk management, primarily used to hedge against the risk of a contingent or uncertain loss.

So kama jambo fulani litatokea kama suala la Elimu,basi hapo inaondoa maana halisi ya Bima!Bima ni kama gumble,lazima kuwe na uwezekano wa jambo lililokatiwa Bima kutotokea,na mara nyingi chances za occurances huwa hazitabiriki!
Nakuunga mkono.Kwa hili wazo la jamaa kampuni ya bima itapata hasata
 
kama hauna mtoto kabisa wa umri wa kusoma basi zinzweza kutumika kwa ajili ya elimu ya wajukuu zako. uwekezaji katika bima ya elimu uwe ni wa kudumu, kama mtoto akimaliza elimu yake na bima yake bado ina pesa inaweza kutumika kwa mjukuu na wanafuata
Hapa ndo umeharibu.Je bima ya afya inamtibu mjukuu baada ya mtumishi kustaafu?
 
Bado kichwa chako ni kizito kuelewa maana ya Bima!
Ngoja nikufungue uweze kuelewa,usipoelewa hapa basi tena!Wazo lako tuseme ianzishwe NEIF yaani national education insurance fund kama ilivyo kwa NHIF!
Sasa kila mwaka mzazi atakuwa anamchangia mtoto % fulani kwa ajili ya bima ya elimu!Siku zote Bima inakuwa na principle moja,uchangiaji wako haulingani na huduma utakayopata once utakapohitaji kutumia Bima yako!Mfano kwenye NHIF,unaweza ukawa umechangia 50,000 kwa mwaka ila ndani ya mwaka huo huo ukatibiwa kwa zaidi ya mil 2!Au unaweza usitibiwe kabisa maana hujaugua!
Insurance Fund huwa ni mfuko wa pamoja,na hutegemea kupata faida pale ambapo wanachama wake hawataitumia bima hiyo,mfano wasipougua,wasipopata ajali na nyumba zao zisipoungua kwa moto!

Tuje kwenye NEIF,hapa ili mfuko upate faida inabidi watoto wengi wanaochangiwa na wazazi wao Bima hiyo wafe au wasipende kusoma!Lakini kama lengo ni watoto wote wapate elimu basi Bima haiwezi kucover!Uhitaji utakuwa mkubwa kuliko mchango wa wanachama!Bima ndivyo inacyooperate,mnachangia kiasi fulani halafu atakayepata tatizo Bima ndio itamsaidia,lakini tuseme hata 50% ya wachangiaje wakipata matatizo au wakitumia Bima basi mfuko hauwezi kuwasaidia wote,pesa hiatatosha!

Ndio maana nasema,kwenye Elimi huwezi kuweka Bima,badala yake unaweza weka mfumo mwingine wa kumhakikishia mtoto elimu na si Bima!
Duniani kote hakuna kitu kinaitwa Bima ya elimu!!!lakini kuna education funds mbalimbali lakini sio Bima!
 
hao watoto watatumia bima kuombea mikopo na kwa kuwa serikali itakuwa imetumia pesa za bima.kwenye uwekezaji wenye faida zaidi basi waombaji mkopo wataweza kupatiwa mkopo kwa asilimia kubwa na kupelekea changamoto ya ukosefu wa mikopo ya elimu ya juu kutatuliwa zaidi
Vipi huo uwekezaji usipoleta faida
 
Kila mwaka madudu yanayoibuliwa na C.A.G yangepatiwa ufumbuzi hii hoja mbovu na ya wizi isingeibuka.

Nakumbushia 1.5 Trilioni hazijulikani matumizi yake.

Rasimu ya katiba ya warioba ndio dawa ya kuwashughulikia mafisadi wa kodi zetu na rasilimali zetu kwa FAIDA ya wote.
 
Nilikua sijasoma vizuri ina maana anapendekeza mfanyakazi tena ambaye hajaongezewa mshahara wake akatwe tena? Huyu mtu ana akili timamu kichwani?
akili ninayo na ndio maana nimetoa wazo ambalo litadumu kwa muda mrefu na itapunguza changamoto kubwa ya kielemu ambayo watanzania. kunaweza kukawa na cost sharing kati ya serikali na mchangiaji na hii itasaidia kupunguza gharama. hebu jaribu kufikiria siku ukifariki mtoto wako atasomaje? kwa nini asiwe na bima ya elimu itakayomwezesha kusoma vizuri?
 
Back
Top Bottom