Sera hii ndo imetufikisha hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sera hii ndo imetufikisha hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MpiganajiNambaMoja, Oct 27, 2008.

 1. M

  MpiganajiNambaMoja Member

  #1
  Oct 27, 2008
  Joined: Sep 20, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sisemi kama ni mbaya, lakini kwa jinsi inavyotekelezwa na serikali ya CCM kwa hakika hatutafika. Hii sera ya Kushirikisha sekta binafsi katika kufanya kazi ambazo zingetakiwa zinafanywe na serikali au wakala wa serikali wenyewe wanaiita Public Private Partnership (PPP) ndo chanzo cha ufisadi ulio kithiri. Sera hii ambayo ilipamba moto wakati wa serikali ya awamu ya 3 ikichochewa na wafadhili ikiwamo Bank ya Dunia ndo imezaa TICTS, RICHMOND, Meremeta n.k. Sababu kubwa ya kuanzisha sera hii ni uwezo mdogo wa serikali katika kutoa na kusimamia huduma mbalimbali kw ufasaha. Sera ilikuwa na lengo zuri lakini tatizo ni kwamba katika nchi yeyote yenye rushwa hii sera haitafanya kazi kama inavyokusudiwa. Hizo kampuni za kushirikiana na Serikali hazipatikana kihalali bali kwa rushwa.
   
Loading...