SEPPUKU , tamaduni ya kikatili toka Japan ya kale

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,060
40,723
‘Seppuku’ au ‘Harakiri’ inamaanisha “kukata tumbo kwa kisu”, hii ni aina ya tamaduni ya kujikafiri kwa kujikata na kulichana tumbo kwa kisu iliyokuwa ikifanyika Japan ya kale. Mila hii ya kikatili ilikuwa maalum tu kwa makamanda wa ki- ‘Samurai’ , lakini pia ilitumika ma wa –Japan wengine wa kawaida ili kurejesha heshima yao au ya familia na koo zao.

Mila hii ya ‘Seppuku’ iliyokuwa maalum kwa ma-‘Samurai’, iliweza kufanywa kwa hiari na makamanda ili aweze kufa kwa heshima na kuepuka kukamatwa na adui vitani pamoja na kuepuka kuteswa pale atakapokuwa mateka. Lakini pia ‘Seppuku’ iliweza kutumika kama adhabu ya kifo kwa ma-‘Samurai’ waliofanya makosa mazito sana au waliofanya matendo ya aibu yalioleta fedheha kubwa sana.

‘Sherehe’ ya kujipasua tumbo ambayo ni sehemu ya tamaduni katika utekelezaji wa adhabu ya ‘Seppuku’ huwa inafanyika mbele ya kadamnasi ya watazamaji, na huwa inahusisha kujichoma kisu kifupi maalum, ambacho kiasili kiliitwa ‘Tanto’, kwenye tumbo na kisha kukata tumbo kwa mtindo wa kulichana kutoka kushoto kuelekea kulia hadi viungo vya ndani ya tumbo vimwagike. Kama kisu kitazama ndani vya kutosha basi inaweza ikaukata mshipa mkubwa wa damu wa ‘aorta’ na kusababisha kifo cha haraka kutokana na kupoteza damu nyingi.

Kisa cha kwanza kurekodiwa cha ‘Seppuku’ kilitekelezwa na Minamoto no Yorimasa katika vita ya ‘Uji’ mnamo mwaka 1180. ‘Seppuku’ ilitumika na makamanda ili kuepuka kutekwa na adui na pia kuondoa aibu pamoja na mateso atakayoyapata pale atakapokuwa mateka. Ma- ‘Samurai’ pia waliweza kuamrishwa na wakuu wao kujikafiri kwa njia ya ‘Seppuku’. Baadae pia, makamanda walioleta aibu na fedheha waliruhusiwa kujiua wenyewe kwa mtindo wa ‘Seppuku’ badala ya kuuawa kwa njia nyingine za kawaida.

Njia ya ‘Seppuku’ iliyokuwa inatumiwa sana na wanaume ni ile ambayo baada ya kujichoma kisu na kulichana tumbo lake, mhusika aliinamisha shingo ili msaidizi wake aikate shingo yake kwa pigo moja tu kwa kutumia panga maalum.

Msaidizi alitarajiwa kuikata shingo kwa pigo moja tu la haraka, vinginevyo akishindwa inakuwa ni aibu kubwa sana kwake na kwa familia yake. Wale ambao hawakuwa sehemu ya watu wa ‘Samurai’ hawakupewa amri wala kutarajiwa kufanya ‘Seppuku’. Na hata ‘Samura’ waliruhusiwa kufanya ‘Seppuku’ kwa ruhusa tu.
images.jpeg.jpg


DON FRANCIS

================================
Update: 18/06/2021

 
Kuna movie inaitwa 44 Ronin(sina uhakika kama nimeipatia) ina mambo ya yanayofanana na unayoongelea, ndio seppuku au?.
 
Pia kuna movie niliiona kama Samurai akikamatwa na wabaya wake kama hana upanga. Basi hukaa chini kwa kukalia miguu na kufanya baadhi ya mazoezi, anakamata shingo yake na kuinyonga mara moja. Naye hukata roho sijuwi hii nayo ni SEPUKU.
 
Pia kuna movie niliiona kama Samurai akikamatwa na wabaya wake kama hana upanga.Basi hukaa chini kwa kukalia miguu na kufanya baadhi ya mazoezi, anakamata shingo yake na kuinyonga mara moja.Naye hukata roho sijuwi hii nayo ni SEPUKU.
Hapana, sio Seppuku hiyo.
 
Je, na ile ya kujikata vidole inaitwaje? si ndio hiyo seppuku? Nakumbuka ktk movie ya Randon Lee kuna yule jambazi kuu anaitwa tagawa alikosewa na moja wa watu wake, yule mkosaji akaamua kujikata kidole lakin tagawa hakuafiki adhabu hiyo tagawa akammaliza kwa kumchoma kisu cha chembe ya moyo.
 
Je, na ile ya kujikata vidole inaitwaje? si ndio hiyo seppuku? Nakumbuka ktk movie ya Randon Lee kuna yule jambazi kuu anaitwa tagawa alikosewa na moja wa watu wake, yule mkosaji akaamua kujikata kidole lakin tagawa hakuafiki adhabu hiyo tagawa akammaliza kwa kumchoma kisu cha chembe ya moyo.
Hiyo ni tamaduni ya kundi lingine kabisa la watu, huwa wanajiita 'YAKUZA' , ni aina flani ya ma gangster hivi.
 
Je, na ile ya kujikata vidole inaitwaje? si ndio hiyo seppuku? Nakumbuka ktk movie ya Randon Lee kuna yule jambazi kuu anaitwa tagawa alikosewa na moja wa watu wake, yule mkosaji akaamua kujikata kidole lakin tagawa hakuafiki adhabu hiyo tagawa akammaliza kwa kumchoma kisu cha chembe ya moyo.
Showdown in little tokyo, brandon lee vs dolf lindgren vs tia carere vs Gary hiroyuki tagawa na wengine kibao .

MÊmENtO HoMO
 
Back
Top Bottom