Antony Fereji
Member
- Sep 29, 2016
- 46
- 63
Kulikuwa na taarifa za muda mrefu kuwa msainii wa reggae wa Afrika kusini, Senzo Mthethwa, ameuawa na marehemu Lucky Dube. Senzo aliyepakua album nne: "Nothing But Prayer", " Irene", "Worshiping Your Love", "Am Sorry", alisimama kuimba tangu mwaka 1999 baada ya kuugua na kupoteza sauti. Senzo aliugua mwaka 1999 alipoenda kufanya 'live show' nchini Malawi. Nilipo ongea na Senzo mwenyewe, mara ya kwanza aliniambia kuwa aliugua malaria kali nakupoteza sauti yake. Lakini baadae, baada ya kuzoeana, alidai kuwa alifanyiwa 'African sciece' na msanii wa reggae wa Malawi atwaye Banda.
Senzo anadai siku alipoingia Malawi alipata mapokezi makubwa ambayo hakuwahi kuyaona ktk maisha yake. Mapokezi hayo yalimfanya Banda akasirike nakuapa kufanya chochote ili kumfifisha Senzo, kwani yeye hakuwahi kuthaminiwa hivyo japo alikuwa msanii mkubwa wa reggae huko Malawi. Senzo alianza kuugua ghafla, akashindwa kufanya onyesho lake. Maisha yake tangu mwaka 1999 yamekuwa ya taabu sana, alipoteza sauti, alikuwa kama mtu asiye jitambua. Lakini Mungu si binadamu, Senzo alianza kupata nafuu tangu mwaka juzi. Anapigana kwa udi na uvumba kurudisha sauti yake, pia anampango wa kutoa album mpya na kuzitolea video nyimbo zake za zamani.
Senzo amekanusha kuwahi kufanya kazi na Lucky Dube. Amedai kuna mtu alikuwepo kwenye bendi ya Lucky Dube alifanana nae tu. Pia amesikitika sana baada ya taarifa kuenea kuwa aliuawa na Lucky Dube. Amedai hakuwahi kuwa na ugomvi na Lucky Dube, wala ugomvi na chuki sio fani yake.
Akiwa na miaka 46, je ataweza kuzitendea haki nyimbo zake za zamani kwa kuzifanyia video? He is a peace soldier.