Sensa yazua balaa; Sheikh Issa Ponda apingwa vikali kuzuia Waislamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sensa yazua balaa; Sheikh Issa Ponda apingwa vikali kuzuia Waislamu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 25, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  JUMAMOSI, AGOSTI 25, 2012 06:44 NA WAANDISHI WETU, DAR

  *Polisi yaahidi kupambana na vikundi korofi mitaani

  *Sheikh atimuliwa, watano wapandishwa kizimbani
  *DC akata mitaa usiku Tanga, Bukoba mambo mazito
  *Sheikh Issa Ponda apingwa vikali kuzuia Waislamu

  WAKATI Sensa ya watu na makazi, ikitarajiwa kufanyika kesho, imezua balaa katika maeneo mbalimbali nchini.

  Moja ya balaa hilo, ni kutimuliwa kazi kwa baadhi ya viongozi wa dini ya Kiislamu na wengine wakifikishwa mahakamani, kutokana na kuhamasisha waumini wao wasishiriki Sensa.

  Kutokana na hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini limesema limejipanga kuwashughulikia watu, vikundi na taasisi ambazo zimenuia kuharibu shughuli nzima ya Sensa nchini.

  Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaama jana, kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, Mkurugenzi wa Oparesheni na Mafunzo, Kamishina Paul Chagonja, alisema wamebaini kuna baadhi ya watu wamejipanga kuwabughudhi makarani na mawakala watakaosimamia Sensa.

  Alisema watu wenye mpango huo, wanapaswa kuacha mara moja kwani watajikuta wakihesabiwa wakiwa rumande.

  Alisema lengo kuu la Sensa, ni kujua idadi ya watu nchini pamoja na kukusanya taarifa zao muhimu kama vile umri, mahali wanapoishi, kiwango cha elimu, hali ya ajira, hali ya uzazi na vifo ikiwa yote ni kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

  "Kutokana na umuhimu na uzito wa suala la Sensa katika nchi yetu, jeshi la polisi linawaomba wananchi wote kushiriki kikamilifu pasipo wasiwasi ya aina yoyote ile, kwani tumejipanga kila kona kuhakikisha shughuli hii inakamilika kwa amani na utulivu.

  "Vile vile tunawatahadharisha wananchi, kikundi cha dini, taasisi au vyama vya siasa, hatutawavumilia hata kidogo watakaoonekana kuwashawishi watu wengine kutoshiriki katika shughuli ya sensa.

  …sasa intelejensia yetu imebaini kuna kundi limejipanga kuwaletea fujo makarani, mawakala na wasimamizi wa sensa, ili wasitimize wajibu wao, tunawatahadharisha kwamba, ni vema wakawa wa kwanza kuhesabiwa, vinginevyo watahesabiwa rumande baada ya kushurutishwa.

  "Tumesikia kiongozi mmoja anaongoza jumuiya fulani, akisema hawako tayari kuhesabiwa, sasa niwaambie yeye atakuwa wa kwanza kuhesabiwa, hivyo wananchi wasidanganyike na kauli zinazotolewa, pia tunawaomba wananchi kutoa ushirikiano pale watakapobaini kikundi, watu au taasisi ikiwa na mipango ya kuzuia ama kuleta fujo katika shughuli nzima ya sensa, ili hatua kali ziweze kuchukuliwa," alisema.

  Hata hivyo, Kamishina Chagonja alisema, shughuli ya Sensa ipo kwa mujibu wa sheria za nchi na ikiwa mtu atabainika kukataa kuhesabiwa atakwenda jela na kupigwa faini isiyopungia Sh 300,000.


  KINONDONI

  MANISPAA ya Kinondoni mjini Dar es Salaam, imewaomba msamaha na kukiri kuwa, kuna makosa yamefanywa kwa kuwatenga wenyeviti wa Serikali za Mitaa, wakati wa Sensa.

  Kutokana na hali hiyo, manispaa hiyo imeahidi kutoa sehemu ya fungu la fedha za manispaa hiyo, ili kuwalipa wenyeviti hao washiriki katika Sensa.

  Akizungumza jana na wenyeviti mitaa 171 mjini Dar es Salaam,

  Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda alisema, hakuridhishwa na kitendo walichofanyiwa wenyeviti hao.

  "Binafsi nimekerwa, ninafahamu tulipoangukia kwani ninyi ndiyo watu muhimu mnaojua mipaka ya mtaa, hivyo kitendo cha kutowashirikisha katika Sensa siyo cha kiungwana.

  "Wenyeviti ni watu walio karibu na jamii na wanafahamu nyendo zao pamoja na sehemu wanazolala, hivyo kutowashirikisha kunaweza kuchangia kuharibika kwa uendeshaji wa Sensa na kwa kutambua umuhimu wenu, ofisi yangu itawawezesha Sh 50,000.

  Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Kwembe, James Nyanda, alisema kama wenyeviti wasiposhiriki Sensa, kutakuwa na matatizo kwani jiografia ya Wilaya ya Kinondoni, ina matatizo ya mipaka na wanaoifahamu kwa undani ni wenyeviti.


  SHEIKH PONDA APINGWA

  Baadhi ya Waislamu, wamegawanyika huku baadhi yao wakiunga mkono Sensa.

  Hali hiyo, imetokana na kundi la wahadhiri ambalo lilikuwa likiunga mkono msimamo wa Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, kupingana na tamko lililotolewa na katibu wao Sheikh Ponda Issa Ponda.

  Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Islamic Peace, Sheikh Sadiki Godigodi, alisema kutokana na kutambua umuhimu wa Sensa, Waislamu na wananchi wote kwa ujumla ni lazima washiriki kikamilifu.

  "Viongozi wa Jumuiya na Taasisi mbalimbali, tumeamua kujitoa kwa umoja wetu…wanaoshawishi Waislamu wagomee Sensa, hawana jambo lolote la maana, tukigoma tunarudisha nyuma maendeleo ya taifa letu nyuma.

  Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, amepinga hatua hiyo na kusema Serikali imeshindwa kuweka mazingira rafiki ya Sensa ya Watu na makazi nchini.

  "Mfumo wa Sensa Tanzania, hauwezeshi madhumuni ya Sensa kufikiwa na ili sensa iweze kufikiwa ni lazima watu wote waweze kuhesabiwa sio kama inavyotaka kufanya sasa kwa kutoa vitisho dhidi ya Waislamu.


  TANGA

  Habari kutoka mkoani Tanga, zinasema watu watano wakiwemo walimu watatu wa elimu ya dini ya Kiislamu katika shule za sekondari mkoani hapa, jana wamefikiswa mahakamani kwa kosa la kuhamasisha wananchi na kusambaza vipeperushi vya kuhamasisha wananchi washiriki Sensa.

  Akisoma mashitaka yanayowakabili watuhumiwa mbele ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Tanga, Maira Kasonge, Wakili wa Serikali, Rachel Magambo alisema, watuhumiwa wanakabiliwa na makosa mawili ya kula njama na kuhamasisha wananchi wasishiriki Sensa.

  Alidai watuhumiwa hao, walitenda kosa hilo Agosti 22, mwaka huu katika Kijiji cha Mtibwani kilichoko wilayani Mkinga.

  Alidai wakiwa msikitini, waliwahamasisha waumini wa dini ya Kiislamu kutoshiriki Sensa, kwa kuwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume cha maelekezo.

  Wakili Magambo, alidai shtaka la pili linalowakabili ni kutotii sheria halali ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu, kwa kusambaza vitabu na vipeperushi vya kuhamasisha wananchi kutoshiriki Sensa.

  Wakili Magambo, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Chambuso Rajabu, Kasim Amar Mbaraka na Hamad Ayub, ambao ni walimu wa elimu ya dini ya Kiislamu kwa shule za sekondari, wengine ni Fadhili Chambo na Husein Mbwana ambaye ni dereva.

  Hata hivyo, baada ya kusomewa mashtaka, mtuhumiwa wa kwanza Rajabu alipohojiwa kuhusu shtaka linalomkabili alisoma aya za qurani, badala ya kukana na kukubali, jambo lililomfanya Hakimu Kasonge kumsihi mtuhumiwa kusikiliza na kujibu anachohojiwa.

  Hata hivyo, washtakiwa wote walikana mashtaka yao na wako nje kwa dhamani ya Sh milioni moja. Kesi hiyo, itatajwa tena Septemba 6, mwaka huu.

  Mara baada ya kesi hiyo kuahirishwa washtakiwa wakiwa na wafuasi wao nje ya mahakama, waliandamana kwa kusema takbiri na kauli ya "Waislamu hatutashiriki Sensa."


  MBEYA

  Kutoka Mbeya, Mwandishi Wetu, anaripoti kuwa Baraza la Masheikh wa Mkoa huo, kwa kauli moja limemsimamisha uongozi Sheikh wa Wilaya ya Mbarali, Yassin Bambala kwa tuhuma za kuwashawishi Waislamu kususia Sensa.

  Tamko hilo, lilitolewa jana na Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Mkoa wa Mbeya, Sheikh Juma Killa baada ya kuridhika na uwamuzi wa baraza hilo.

  Alisema Sheikh Bambala, amekuwa akishiriki na kuhudhuria vikao vya baadhi ya Waislamu wanaopinga Sensa, kufanyika kwa kuwataka wasijitokeze siku ya kuhesabiwa.

  Alisema, baraza limebaini wapo baadhi ya viongozi wamekuwa wakifanya kampeni za chini chini, kwa kuungana na taasisi nyingine wasishiriki.

  "Hawa walifanya hivi wakati wanafahamu fika, msimamo wa BAKWATA na Kiongozi Mkuu wa Waislamu (Mufti), kuhusu kuhakikisha Waislamu wanashiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi," alisema Sheikh Killa.

  Alisema, wahusika hao wamekiuka maagizo ya pamoja ya Waislamu kwani awali masheikh wa ngazi za wilaya na wale wa mikoa nchini, waliitwa na Mufti mjini Dodoma kwenye kikao cha Tume ya Dini na kupeana msimamo wa pamoja kuhusiana na zoezi la Sensa na wakakubali kurudi kwenye maeneo kuwahamasisha Waislamu wenzao kushiriki Sensa.

  Alisema baadhi ya masheikh, akiwemo Sheikh Bambala baada ya kurudi kutoka Dodoma, walianza kufanya kazi tofauti na makubaliano ya pamoja yaliyofikiwa.


  DC NYUMBA KWA NYUMBA

  MKUU wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu ametoa kali ya mwaka baada ya kuhamasisha Sensa ya watu na makazi kwa aina yake, baada ya kupita nyumba kwa nyumba usiku.

  DC Mgalu amekuwa akipita katika maeneo mbalimbali yakiwemo masoko na kuwaambia wafanyabiashara, wajitokeze kwa wingi Agosti 26, mwaka huu ili wahesabiwe.

  Mbali ya masoko, amekuwa akipita mitaa mbalimbali kwa miguu na kuwasimamisha watu mbalimbali.

  Akiwa katika Soko Kuu la Wilaya juzi, alionekana wazi wazi akisisitiza umuhimu wa Sensa kwa kila mtu.

  Mgalu aliwaomba wafanyabiashara hao kuwa itakapofika siku ya kuhesabiwa sensa, wasitoke nyumbani mpaka wahesabiwe.


  MADIWANI

  MADIWANI katika Halmashauri ya Jiji la Tanga, wametakiwa kuwa mstari wa mbele kuhamasisha wananchi wao kushiriki kikamilifu Sensa.

  Wito huo, ulitolewa juzi wakati wa semina ya madiwani hao na mwezeshaji kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Taifa, Nicholaus Moshi iliyohudhuriwa na madiwani kutoka kata 24.

  Alisema wakati wa mchakato huo, ni lazima viongozi hao kwa kushirikiana na viongozi wengine pamoja na wananchi kutoa ushirikiano kwa makarani wote, ambao watapita kwenye maeneo yao ili kufanya mchakato huo uweze kupata mafanikio.

  Alisema watu wote, walioandaa vipeperushi vya kupotosha mchakato huo, watachukuliwa hatua za kisheria, bila kificho.

  Awali Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego aliwataka viongozi hao kuweka kando suala ya udini na ukabila, ili kufanikisha mchakato huo.

  Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Tanga, Omari Nundu aliwataka madiwani kuhakikisha wanasimamia kikamilifu mchakato wa Sensa ya watu na kuacha ushabiki wa kisiasa.


  BUKOBA

  Habari kutoka Bukoba, zinasema Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Ziporah Pangani ameahidi kumchulika hatua kali mtu yoyote, bila kumuangalia usoni ambaye atajaribu kukwamisha Sensa.

  Alitoa kauli hiyo, wakati wa kikao chake na viongozi wa madhehebu ya dini, viongozi wa vyama vya siasa na baadhi ya waandishi wa habari.

  Aliwaambia washiriki wa kikao hicho, hasa viongozi wa dini na viongozi wa vyama vya siasa, wahamasishe wafuasi wao ili wakubali kuhesabiwa.

  Alisema Serikali haitakubaliana na wale wanaodaiwa kusambaza vipeperushi ya kuwazuia watu, wasishiriki Sensa watachukuliwa hatua kali.

  Alisema maandalizi yote yamekamilika na kwamba Sensa itafanyika kwa amani kabisa.

  Na Amina Omari, Oscar Asenga (Tanga), Audax Mutiganzi (Bukoba) na Pendo Fundisha (Mbeya), Benjamin Masese, Bakari Kimwanga, Christina Galuhanga na Sebastian Mparazo (Dar).

   
 2. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Rais Kikwete ameagiza kwamba wale wote watakaokwamisha zoezi la sensa wachukuliwe hatua za kisheria. Ole wake mtu yule atakayebainika kukwamisha sensa!
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ukianza kula nyama za watu hutaacha alisema Nyerere sasa hii zambi imeanza kuwatafuna CCM
   
 4. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,094
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Yeyote anayepinga sensa kwa sababu yeyote SIKUBALIANI NAE KATU.NI UJINGA MKUBWA SAANA KUSUSIA SENSA...Nina hasira.
   
 5. k

  khamsa Senior Member

  #5
  Aug 25, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 155
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  habari za ukweli zitapatikana kuanzia kesho inshaallah.
   
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  Aug 25, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mufti wa Tanzania ameshaonya dhidi ya kaffir yeyote anayekwamisha sensa
   
 7. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #7
  Aug 25, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,094
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  natamani wote wanapinga sensa wachapwe viboko..nonsense
   
 8. Hute

  Hute JF-Expert Member

  #8
  Aug 25, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,062
  Likes Received: 3,928
  Trophy Points: 280
  hivi kwanini ponda asirudishwe kwao burundi? hawa maforena wanasumbua sana tz.
   
 9. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #9
  Aug 25, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Rais KiKwete anaingia katika historia ya kuwa rais wa kwanza duniani aliyeshindwa hata kusimamia sensa ya watu wake. Udhaifu huu wa Kikwete kushindwa hata kusImamia sensa unaweza kuhusishwa na masuala ya kidini huku wengine watafikiria mfumo kristo ndio unasababisha viongozi shupavu watoke dini nyingine tu
   
 10. U

  UNO Senior Member

  #10
  Aug 25, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wameachiwa kufanya wanavyotaka sasa matokeo yake ni haya. Wametukana sana dini nyingine, hasa kupitia redio imaan, hakuna kiongozi aliyekemea. Wakachonganisha saana wananchi walio na imani tofauti, hakuna aliyesema kitu na leo wamediriki hata kutangaza wazi kwamba watu wasishiriki sensa; tena kwenye redio imaan; lakini bado mpaka leo hakuna aliyeulizwa........Haya ndio matokeo; msishangae; nendeni nyumba kwa nyumba mkawaombe......
   
 11. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #11
  Aug 25, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hii ndiyo inatakiwa...kama unaua nyani...
   
 12. m

  miti Senior Member

  #12
  Aug 25, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  khafiri yeye anayekubali kuhesabiwa
   
 13. m

  miti Senior Member

  #13
  Aug 25, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  uanze kurudishwa kwanza wewe kwenu msumbiji we vipi? kazi kuomba uraia kwenye nchi za wenzio tu lione kwanza kama chizi vile!
   
 14. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #14
  Aug 25, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,884
  Likes Received: 2,833
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo kwenye red una ushahidi?

  Sasa kama ni Mrundi kwa nini Serekali hii Dhaifu inamlea?
   
 15. A

  Aikaotana Senior Member

  #15
  Aug 25, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  muislamu hawezi kumpinga Sheikh Ponda kuhusu sensa, fanyeni sensa hiyo
   
 16. B

  Bahati Risiki JF-Expert Member

  #16
  Aug 26, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwani Kikwete anahesabu watu amewasadia nini? Shule ni za kata bila mwalimu wala kifaa. Hospital ndiyo kama tunavyoona. Barabara ndiyo lami za danganya toto. Hakuna system ambayo inaangalia wazee, vilema, wagonjwa, nk. Sasa unahesabuje watu ambao hawafaidi chochote kutokana na raslimali za taifa?
  Hii serikali haiko serious na kuboresha chochote cha umma wa watanzania. Ni matumbo yao na basi. Kwani wanashindwa kujihesabu wao wenyewe na ufisadi wao? Kuwatishia watanzania na vijisensa visivyo na tija sii sawa. Kwanza tumia raslimali za taifa kujenga shule bora, hospitali za kisasa na zenye madaktari na vifaa vya kazi. Jenga barabara bora kuanzia mjini hadi vijijini ili wakulima waweze kusafirisha mazao yao kwenda sokoni. Weka system zinazoeleweka tangu mtoto anapozaliwa. Ukifanya hayo watanzania watakuheshimu na wataona faida ya kuhesabiwa. Sasa unatutishia tu wakati tunajua hakuna faida ila kwa mafisadi. Unafikiri hii nchi ni ya wajinga wale uliojua? Punguzeni kelele fanyeni kazi na muache madanyatoto yenu eti kuhesabiwa. Ninahesabiwa leo kesho ninaenda hospitali hata kidonge cha maumivu hakuna. Kikwete acha upuuzi wa kuwaibia watanzania na kuwanyanyasa for nothing.
   
 17. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #17
  Aug 26, 2012
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Kamwambie huyo mhariri wa gazeti la mtanzania na kesho tena aweke kichwa cha habari kama hicho front page,ili jamii ipime nani muongo. Mimi ninavyojua imepingwa serikali nasiyo ponda. Nchi nzima waislam hawashiriki sensa. Sasa hapo nani kapingwa? Acheni propaganda ivo mnamuangusha kikwete.
   
 18. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #18
  Aug 26, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,812
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  Huyu Ponda anastahili apelekwe Mabwepande apewe haki yake baada ya sensa aachwe huko akiweza kurudi sawa akishindwa nayo poa tu, huyu asipoangaliwa sana atakuja kuingiza nchi kwenye machafuko ya kidini!!
   
 19. C

  Chiya Chibi JF-Expert Member

  #19
  Aug 26, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 485
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Huyo Shekh Ponda ajipange, sensa ikimalizika tu ndo atagundua kuwa serikal ina mkono mrefu unaoweza kumfikisha mtu Mwabepande. Kwahiyo ndg na jamaa zake andaen hela za kumpeleka mwenzenu South Africa. Simuombei hivyo, lakin ni vema mkajiandaa hasa nyie mnaomuunga mkono bila kutafakar kwa kulinganisha hoja zake na sheria za nchi plus Bakwata na utawala uliopo.

  Kubalini kuhesabiwa, na mzipange upya hoja zenu, kuanza upya sio ujinga. Kama kweli serikali inawaonea na kuwapendelea wakristo tafuten uthibitisho ambao utaifanye serikali iamin maneno yenu, tena msichelewe mana waislam wenzenu ndo wapo madarakan (Ikulu) na bado miaka 3 tu.
   
 20. MZIMU

  MZIMU JF-Expert Member

  #20
  Aug 26, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 4,080
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  mufti wa bakwata yeye ndie kafiri. Anauza imani yake kwa ajili ya dunia. laanatul llah alaihi.
   
Loading...