Sensa yaingiwa na Giza kufanikiwa kwake majariwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sensa yaingiwa na Giza kufanikiwa kwake majariwa

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Return Of Undertaker, Aug 23, 2012.

 1. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,376
  Likes Received: 8,521
  Trophy Points: 280
  Zikiwa zimebaki siku tatu tu kabla ya kuanza rasmi zoezi la sensa ya watu na makazi, kumeibuka changamoto mbalimbali ikiwemo watu kusambaza vipeperushi vinavyozuia wananchi kushiriki sensa na katika baadhi ya maeneo makarani wakigoma kula kiapo kwa kuwa hawajalipwa posho ya kufanyakazi hiyo.

  Hii ni kwa mujibu wa uchunguzi wa NIPASHE katika mikoa mbalimbali nchini uliofanyika jana.

  Mkoani Tanga, kundi la watu wasiofahamika limesambaza vitabu na vipeperushi vinavyowataka wananchi kutoshiriki zoezi hilo.

  Mratibu wa sensa mkoa wa Tanga, Toni Mwanjota, aliiambia NIPASHE kwamba vitabu na vipeperushi hivyo vimekuwa vikitolewa kwa siri kubwa.

  "Tumesikia kuwa vipo vitabu na vipeperushi ambavyo vinatolewa na watu wasiopenda maendeleo ila vinatolewa kwa siri sana lakini tunavifanyia kazi," alisema.

  Hata hivyo, aliwataka wananchi kutambua kuwa ni kosa kisheria kufanya hujuma yeyote inayolenga kukwamisha sensa.

  Visiwani Zanzibar, Jumuiya za Kiislam Zanzibar zimetoa masharti kadhaa ambayo kama hayatatekelezwa, taasisi hizo zitaendelea kuwashawishi wafuasi wake kususia zoezi la sensa visiwani humo.

  Tamko hilo lilitolewa na kiongozi wa jumuiya hizo, Sheikh Mselem Ali Mselem, katika mkutano na waandishi wa habari uliotishwa kutoa msimamo juu ya ushiriki wa wananchi wa Zanzibar katika zoezi la sensa itakayofanyika nchini kuanzia Jumapili ijayo.

  Sheikh Mselem ambaye ni Amir wa mwavuli uitwao Umoja wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu Zanzibar, alisema taasisi hizo zinataka serikali itekeleze haki ya kisheria kwa wananchi kupewa vitambulisho vya Uzanzibari.

  Alisema pamoja na kuwapatia vitambulisho wote wanaostahili, serikali pia iwaamuru wote waliopewa vitambulisho hivyo kwa utashi wa kisiasa kuvirejesha.

  Sheikh Mselem alitaja sharti lingine ambalo taasisi hizo zinataka litekelezwe ni kuingizwa kwa kipengele cha dini katika dodoso za sensa hiyo.

  Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, amesema zoezi la sensa limekumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo kuibuka kwa

  kikundi cha watu wachache ambao ni waumini wa dini ya Kiislamu waliokuwa wakipinga zoezi hilo.

  "Hiki ni kikundi cha watu wachache wenye dhamira chafu ya kutaka kukwamisha zoezi hili, watu hao wanapatikana katika wilaya za Same, Mwanga, Hai na Moshi Manispaa, walikuwa wanajipatia kazi zisizo na mshahara kwa kupita na kuwahamasisha wananchi ili waweze kupinga zoezi la hilo," alisema.
   
 2. M

  Mbofu JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani waislam hamuwezi kujihesabu wenyewe hadi mhesabiwe na serikali? Mbona ni kitu rahisi sana! Mngesubiri zoez la taifa likafanyika then nanyi mkaendesha lenu, kwa kujuchukua idad ya watz mngejua mpo asilimia ngapi, simple,au mnataka kodi zetu ziwahesabu?
   
 3. m

  mamajack JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  serkali inayoelekea kushindwa daima haiwezi kusimamia jambo likafanikiwa.magamba wamelifanya zoezi la sensa kisiasa sana ndiyo maana ufanisi wa ihakika haupo.makalani kuweni makini huko mitaani msije mkachezea kipigo bure.

  angalia masuala yote haya matatu yanazid kuharibika na kupoteza maana.
  1.maoni ya katiba mpya tume imelewa pesa na wanafanya kulingana na maoni ya magamba
  2.vitambulisho vya ilaia ndo ovyo kabisa,
  3.sensa ndo msiba wa taifa.
   
 4. M

  Makupa JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Tabia ya cdm kuchochea migomo ndio mazara yake haya
   
 5. m

  mamajack JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  sasa seikali iliyoko madarakani inakubali kushinwa na chama ambacho hata kilichoko nje ya utawala.
  kwa hiyo unaniambia wananchi wanawaitii sana cdm kuliko serikali??????
  kama ndo hivyo basi cdm cha kubwa milele.
  hebu chukulia mfano wa mwanao,utashindwa kumdhibiti sababu ya majirani zako au ndugu,
  kweli nchi inaongozwa na watu wanaofikiri kwa kutumia nywele na sio akiri.
   
 6. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Kushindwa kuwa zoezi hili ni dhahili kabisa kwa sababu nyingi tu:
  1. Makarani wamechukuliwa kwa kujuana na wasimamizi wa sensa amabo wengi ni sisiemu, unamkuta karani hajui lugha ya kisukuma anapangiwa kwenda kufanya kazi maeneo ya Igwambiti - Buhongwa Mwanza; kwa vyovyote vile karani huyu hataweza kuwasiliana na wananchi hao ambao kiswahili kwao ni kama kiarabu.
  2. Wabunge walipewa pesa kwa ajili ya kuhamasisha sensa, tuambizane ni wabunge wangapi wameonekana mitaani / majimboni kwao wakifanya kazi hiyo?
  3. Wenyeviti wa mitaa hawajashirikishwa hata kidogo; tutegemee nini iwapo makarani wataingia mitaani na kuomba ushirikiano kwa wenyeviti hao amabo hawajapewa hata hela ya soda?
  4. Tunavyojua sensa madhumuni yake ni kujua idadi ya wananchi ili serikali iweze kuwahudumia; ni lini serikali ya sisiemu ikawahudumia wananchi wa Tanzania badala ya kuwaibia hata kile kidogo walichonacho?
  5. Wewe unayesoma haya una lipi la kuongezea? .......
   
 7. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  msitupie waislamu peke yao ,wao kama wananchi wengine wanayo haki ya kukataa ,mbona kuna wakulima wafugaji walimu nao pia wamesikika kutishia kushiriki zoezi hilo ?
   
 8. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #8
  Aug 23, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Uzalendo wa wananchi uko kwenye all time low tangu uhuru sasa ni sisi dhidi yao, kila walifanyalo ni baya lililokuwa disguised kwenye masuala yenye tija kwa Taifa. Hawako sincere, nitakosea nikisema wanatuhesabu ili wafunge hesabu mapema come 2015 #justsayin
   
 9. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Nimekusoma baby! Ila nia yao ni kutuhesabu hili watutumie kuombea misaada then wagawane!
   
 10. mnyanyaswaji

  mnyanyaswaji JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2012
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 469
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Pumba unazungumza. Je, km wakijihesabu wakaja na takwimu zao jamii itazikubali? Miez michache iliyopita kila mtu alikuja na takwimu zake za uongo.

  Mmfano kanisa Catholic na TBC1 na zote uongo mpaka kupelekea kuomba msamaha. All in all serikali ndo msimamizi wa institutes zote so yatakiwa awe na records sahihi.

  SUali linakuja, kama serikali inakana je, nani msimamizi? Wahuni tu wanaoropoka ropoka na hatuwaamini. Kajipange upya.
   
 11. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Inasemekana kuwa yule atakayehesabiwa ndie atakayepata vile vitambulisho vya mtanzania,itakuwa very strictly wakati wakuhakiki upya ukuhesabiwa !hamna kitambulisho na vile vya wapiga kura navyo vitasitishwa rasmi sasa kazi kwenu amueni kuhesabiwa au kutohesabiwa na kitambulisho cha mtanzania ndio kitasaidia kila mahali,na hapo ndipo itakapowakamata wote waliokataa kuhesabiwa!!!!!!!!!!

  mimi simo kabisa
   
 12. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  mbona hiyo sijasikia je waliopo nje ya TZ hawaitaji kuwa na vyeti vya utambulisho
   
 13. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  only in tanzania! pathetic!
   
 14. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Upuuzi mtupu!
   
 15. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #15
  Aug 23, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Upuuzi wa serikali ya dhaifu huu, majungu majunguuuuu
   
 16. sister

  sister JF-Expert Member

  #16
  Aug 23, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,027
  Likes Received: 3,933
  Trophy Points: 280
  sensa ya mwaka huu ni pasua kichwa mpaka ipite tutasikia mengi.
   
 17. H

  Hute JF-Expert Member

  #17
  Aug 23, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,053
  Likes Received: 3,920
  Trophy Points: 280
  kuishi na wanafunzi au wasomi wa chuo kikuu cha morogoro MU ni zaidi ya kubebe gunia la mawe....ni shida sana...sasa kwanini wanakataa kuhesabiwa?sababu waliyotoa ni ndogo sana hadi huamini kama kichwani zimewatosha.
   
 18. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #18
  Aug 23, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Hapo ndipo upeo wako wa kufikiri ulipofikia anyway lets go, the day will come we will have real dream
   
 19. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #19
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,371
  Likes Received: 19,597
  Trophy Points: 280
  kikwete kwenye uchaguzi si alishasema kuwa nchi ina udini? Ama mmesahau?ila hii ya sasa ni muslim against muslim ama against Pinda
   
 20. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #20
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Jino la pembe si dawa ya pengo, walisema waswahili!
  Hawa watu wameshindwa kuongoza nchi then wanaanza kubuni mambo ya ajabu...
  Wekeni ndani watuhumiwa wa ufisadi wote, prior to legal actions, muone kama Wanaogomea sensa wataendelea kufanya hivyo!
   
Loading...