Sensa ya watu na mifugo wilayani Ngorongoro

Monasha

JF-Expert Member
Apr 2, 2011
561
422
Nawasalimu wote wana JF,

Wakati naayaandika haya, wakazi wa Ngorongoro wanajiandaa kwa Sensa ya watu na mifugo inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni. Ikumbukwe kwamba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliiagiza mamlaka hiyo kufanya zoezi la sensa alipoitembelea mnamo December 6 mwaka 2016.

Aliagiza mamlaka hiyo ya hifadhi ya Ngorongoro na serikali ya mkoani humo kufanya zoezi la sensa ya watu na mifugo ili kutambua idadi halisi ya wenyeji wanaotakiwa kuishi kisheria katika eneo hilo ambalo sasa kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wageni kuwa limeelemewa na idadi ya watu,mifugo na makazi.

Haya yanafanyika kwa kisingizio cha kuwaondoa wavamizi yaani watu amabo siyo wenyeji wa hapo ambao wamekuwa wakiishi kinyume na taratibu za hifadhi. Serikali inaenda mbali zaidi kwa kutaka wenyeje wawe na kadi maalum (special card) ya kuingia kwenye eneo la hifadhi.

Ujio wa hili zoezi limezua gumzo kubwa sana miongoni mwa wakazi wa Ngorongoro kwani imewajengea hofu kubwa sana. Watu hawajui nini kitatokea baada ya zoezi, nani atatimuliwa na kwenda kutafuta makazi mapya.

Wengi mtakubaliana na mimi kwamba wakazi wa Ngorongoro ndio watanzania wanaoishi katika mazingira magumu kupita kiasi, ndiyo maisha ni magumu kwa watanzania lakini watanzania wa Ngorongoro wana maisha magumu zaidi.

Kunyimwa kilimo, maendeleo ya namna yoyote ile ikiwemo kuanzisha biashara katika eneo unaloishi ni moja ya dalili kwamba huyo mtu ana mazingira magumu sana. Uongozi wa NCAA umekuwa ukijikita sana kwa mamboya uhifadhi huku ikiwasahau wenyeje na kuwaacha wateseke, ndo kusema akufukuzae hakuambii toka. Leo hii serikali inasahau kwamba moja ya sifa Ngorongoro ni kuwa kuna maisha ya binadamu na wanyama pamoja kitu ambacho ni tofauti na hifadhi zingine duniani. Serikali inashindwa kuja mpango dhabiti wa kuwaendeleza wenyeji hawa badala yake kumekuwa ni mlolongo wa unyanyasaji tu.

Hivi unafanya sensa halafu ukute hamna wahamiaji, nini kitafata kama siyo kuwaondoa wenyeji kwa lazima? Bila shaka kama serikali inataka zoezi hili liende salama na kwa mafanikio, ingeendesha kwanza semina juu ya hili zoezi na pia ingekuwa ni nafasi kwao kujibu maswali lukuki toka kwa wakazi wa Ngorongoro badala ya kuamka tu na kuanza zoezi la sensa. Wakienda hivi watakosa ushirikiano na mwisho wa siku hizo Milioni 400 za zoezi lenyewe zitakuwa zinapotea bure tu.

Tuendelee kujifunza mengi toka kwa serikali yetu sikivu.
 
Acha lifanyike tu maana kuna sintofaham kubwa hasa kwa suala la umiliki wa mifugo katika eneo hilo.
 
Back
Top Bottom