Sensa:serikali ya visasi,kinyongo,fitina,majungu nk yawanyima wangi kusimamia sensa

matongo manawa

JF-Expert Member
Apr 6, 2011
336
79
Serikali imefanya kioja kingine kwa kuwapiga chini walimu kusimamia zoezi la sensa
tofauti na sensa ziliopita ambapo walimu ndo walikuwa wadau namba moja.
Taarifa za ndani zinathibitisha kuwa hila hii wamefanyiwa walimu ili kukomolewa
kutokana na kugoma.

Swali:Mgomo wa walimu si ulikuwa unaratibiwa na CWT?
Sasa kwanini waadhibiwe walimu??

Wito:walimu mmegeuzwa na serikali hii km jalala na kwavile wao wameamua hivyo
Shikamaneni kwa kugomea sensa nasi wanafunzi wenu tutawaunga mkono.
Pili CWT wapozeni walimu hata elfu hamsini kila mmoja kutoka michango yao
ili kuwapa moyo mana ktk hali ya kawaida wanaweza wasishiriki mgomo
kwakuogopa serikali ya visasi kuwabania kwenye issue km za uchaguzi.

Hali halisi:nafasi za sensa zimegeuka mtaji kwa watendaji wa kata wanauza majina
Moja laki moja.
Ushauri:serikali iache visasi na mtimanyongo kwa walimu kwani wameonesha utii
wa sheria pale mahakama chini yajaji wa voda fasta kuharamisha mgomo
waalimu walisitisha mgomo.
 
Ni waalimu tu wanaojua kufanya kazi ya sensa?Acha kulalamika ndugu yangu!Hiyo sensa ilikuwa inahitaji watu wangapi?Waombaji ni wangapi?Ulitaka walioomba wote wapate?Mwalimu tayari ana ajira!Waonaje na wasiokuwa waalimu wakafanya kazi hiyo kwa muda wakajikimu kimaisha?
 
wagalatia aya sasa nafasi hzo. MI FWEDHA YA UFISADI AKA SENSA KITUKO. CDM MPO WAPI KUKUBALI SENSA IENDELEE WHEN IMESHAPOTEZA MAANA! HAESABIWI MUJAHIDINA HATA MMOJA
 
Ni waalimu tu wanaojua kufanya kazi ya sensa?Acha kulalamika ndugu yangu!Hiyo sensa ilikuwa inahitaji watu wangapi?Waombaji ni wangapi?Ulitaka walioomba wote wapate?Mwalimu tayari ana ajira!Waonaje na wasiokuwa waalimu wakafanya kazi hiyo kwa muda wakajikimu kimaisha?

Mzee mpiganaji jaribu kutafakali kidogo usiamini sana majibu wanayoyatoa wanasiasa kama majibu aliyoyatoa Mtoto wa Mkulima jana bungeni akijibu swali kuhusu walimu na sensa! Ukweli ni kuwa maaamuzi ya kuwaengua walimu kwenye sensa yamefanyika kwa ajili ya kuwakomoa baada ya mgomo walioufanya. Mpango wa awali wa serikali ulikuwa ni kuwatumia walimu kwa kazi ya sensa na ndio maana walitoa maelekezo ya kubadilisha mihula ya masomo na shule zifungwe Agosti badala ya Juni kama ilivyokawaida ili walimu watapokuwa kwenye kazi ya sensa watoto wasikose masomo.

Jaribu kujiuliza swali dogo tu wewe unayejiita mpiganaji! Kama kazi hii ya sensa ilikuwa ni kwa ajili ya watu wote watakaoomba ni kwa nini shule zimefungwa agosti badala ya juni!!? na je kuna ofisi nyingine yoyote ya serikali ambayo itafungwa kupisha zoezi la sensa!!? Walimu wanaonewa sana nchi hii!!! NAshukuru Mungu Mimi sio mmoja wao! Labda ningeua mtu kwa manyanyaso haya!
 
ni vizuri walimu kunyimwa kusimamia hilo zoezi la sensa na kulinda profession yao badala ya kutumiwa kama TP
 
Ni waalimu tu wanaojua kufanya kazi ya sensa?Acha kulalamika ndugu yangu!Hiyo sensa ilikuwa inahitaji watu wangapi?Waombaji ni wangapi?Ulitaka walioomba wote wapate?Mwalimu tayari ana ajira!Waonaje na wasiokuwa waalimu wakafanya kazi hiyo kwa muda wakajikimu kimaisha?

Ndugu yangu naomba nikuambie,toka awali waalimu walielezwa kuwa wao watatumika katika sensa,ratiba ya kufungwa mashule ilibadilrishwa kwa sababu tu waalimu watakuwa kwenye zoezi la sensa.Kawaida shule zote huwa zinafungwa mwezi wa sita lakini kwa sababu walipanga mwanzo kuwa waalimu watatumika kwenye sensa shule zimefungwa sasa hivi.Kituko kilichotokea ambacho ni dhahiri kabisa kuwa kinahusiana na mgomo wa waalimu uliopita ni kwamba waalimu wameachwa kwenye zoezi la sensa.Nilikuwa manispaa ya kinondoni hakuna mwalimu hata mmoja hasa wa sekondari aliyechukuliwa kwenye zoezi hilo.Nasikitika sana kuona nchi inayumba vibaya sana,sijui kwa nini watendaji hawalioni hili?,kweli sikio la kufa halisikii dawa.

Walimu vigeu geu.. ni mwamini nani kwani.....mwishowe ananigeukia,..walimu vigeugeu... Ukiigomea serikali igomee vyote sio mara kufundisha no ila sensa nipe. Katika kutetea haki adui namba moja huwa ni NJAA. Malalamiko ya walimu kukosa sensa kutoka kwa mwajili yuleyule waliemkorofisha juzi yanadhihilisha hilo. Waingereza angewaambia walimu kuwa; YOU OUGHT TO HAVE KNOWN BETTER. Poleni walimu hayo ndo madhara ya ujasiri bandia na wa kuiga.
 
hahahahaha..walimu ni dhahili wanatapatapa.mlijua mkigoma kipindi km hichi cha sensa madai yenu yatasikilizwa kwa kua mmeshikilia zoezi.hii serikali janja nyie.mlikolala nyie ndio ilikoamka.naona weng wenu mnalia, kugoma mmegoma na sensa mmekosa.by the way waswahili wanakamsemo kao wanadai kufa kufaana.nyie mmekufa mmetufaa cc majobless.tunakula mpunga wa sensa saf kabisa.
 
Poleni waalimu. Ila naamini kuna madudu yatafanyika na serikali itajua baadae umuhimu wa kutumia waajiliwa ktk sensa. Mwaka huu hadi bar maids inclusive ili mradi anajua kuandika.
 
Back
Top Bottom