Sengerema ukame unawamaliza, waomba msaada toka Serikalini

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Wakazi wa maeneo ya NYAKASASA na ISENYI katika kisiwa cha KOME wilayani SENGEREMA mkoani MWANZA wameiomba serikali kuwapelekea chakula cha bei nafuu ili wakabiliane na tatizo la ukame linalowakabili.

Wakazi hao wametoa ombi hilo kwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. CHARLES TIZEBA alipowatembelea kusikiliza kero zinazowakabili.

Akijibu hoja za wananchi Dkt.TIZEBA amewaambia serikali inafanya utaratibu kwa maeneo yote nchini kujua athari za ukame ili kupeleka chakula cha bei nafuu kwa wananchi.
 
Mheshimiwa sana na mgombea urais William Mganga Ngeleja mbunge wa sengera mbona kimyaa
 
Huo utafiti unahitaji catalyst. Ni kiasi tu cha Lowassa kutoa tamko moja tu. Mtaona watakavyokimbiziwa chakula.
 
Njaa hakuna, anaejua kuwa kuna njaa ktk familia ni mimi, anaetakiwa kutangaza kuwa kuna njaa ni mimi. Bora kifo hujui unakufa lini kuliko kujua kuwa kuna miaka 9 ya mateso mbele.
 
Haa Serikali Ya Viwanda Haitambui Njaa
Nakumbuka Serikali Haitambui Uchawi Pia
 
Back
Top Bottom