Uchaguzi 2020 Sengerema: Dkt. Magufuli aomba ridhaa kuongoza Muhula wa Pili. Asema wakichagua mwingine anaweza kuuza skrepa vyuma vya kujengea daraja

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
Leo Rais Magufuli anaendelea na kampeni mkoani Mwanza na yuko wilaya ya Sengerema, fuatana nami kukujuza yatakayojiri.

======



MAGUFULI: Wananchi wa Sengerema nawashukuru kwa makaribisho mazuri niliyoyapata hapa leo, Sengerema mmefunika, asanteni sana. Nilipopata makaribisho pale barabarani, nikafikiri ndipo kwenye mkutano, nikahutubia nikafikiria naishia huko huko.

Mimi Sengerema ni mwenyeji, katika maisha yangu nilivyoanza kufanya kazi, nilianzia Sengerema, nilifundisha Sengerema sekondari kwenye miaka ya 82-84 kwa hiyo Sengerema mimi ni mwenyeji. Maeneo yote ya Sengerema ninayafahamu, haikuwa hivi, kwenye miaka hiyo hata lami haikuwepo, ilikuwa ni barabara ya changarawe ambayo mara nyingi hata magari yalikuwa yanazama.

Upande wa barabara hii ya kwenda Nyakalilo ndio ilikuwa shida zaidi, kulikuwa na basi moja lilikuwa linaitwa digidigi, inawezekana mmeshasahau, linaweza kupita kwa wiki mara mbili na ndilo lilikuwa linategemewa, sehemu nyingine kulikuwa na mabasi ya African bus kwa hiyo maisha ya Sengerema ninayafahamu.

Tumekuja kuomba kura miradi yote iweze kukamilika, tumeweza kutenga mabilioni ili tatizo la maji liwe halipo wilaya hii ya Sengerema. Tumeendelea kutoa elimu bure, tumejenga madarasa 167, tumekarabati shule ya Sengerema sekondaro kwa bilioni 1.03 pamoja na vyuo vya maendeleo vya Wananchi.

Baadae tutakuja na mpango mkubwa wa kuimarisha bima ya afya kwa watanzania wote na hili limefafanuliwa vizuri katika kitabu cha ilani ya uchaguzi ukurasa wa 136, ndio maana tunaomba kura kwenu.

Fedha hizo zilipotolewa kwenye daraja hilo(Busisi) bilioni 700 si kidogo, hakuna mtu alietegemea tangu tupate uhuru, tangu dunia iumbwe tutatengeneza daraja hilo. Nyinyi wananchi wa Sengerema ndio mashahidi wa kwanza kwa sababu kazi ishaanza ndio maana nawaomba tena kura.

Mradi kama huo wa mabilioni 700, mkimleta mtu mwingine ambae hajui hata fedha atazitoa wapi, anaweza akatoa yale machuma akaenda kuuza skrepa. Ninawaambia ukweli na bahati nzuri ndugu zangu, uongozi haujaribiwi, huwezi ukajaribu uongozi katika miaka mitano.

Zipo nchi zilizojaribu kuujaribu uongozi, madhara yake mliyaona, uongozi haujaribiwi.

32E943F8-C7B3-4FB1-8BC3-21E3272E53F2.jpeg


Magufuli Misungwi.jpg

Mgombea Urais na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, DKT. Magufuli akiongea na kuagana na wananchi eneo la Misungwi mkoani Mwanza akiwa njiani kuelekea mkoa wa Geita leo Jumanne Septemba 8, 2020.​

NJIANI-BUKOKWA
MAGUFULI:
Yaani Bukokwa mmejaa hivi! Mheshimiwa Tizeba panda hapo uniombee kura, umuombee na mbunge na diwani.

TIZEBA: Magufuli oyeeee, Shigongo oyeee, niombe sana, mambo makubwa yaliyotokea Buchosa katika kipindi cha uongozi wake, neno moja tunaweza kulisema asante sana baba na wananchi hawa wanaziona nguzo, wanayaona mambo makubwa yaliyotokea.

Wananchi wa Buchosa mtakaomuunga mkono Shigongo nyoosha mkono, alafu wale wapambe wa Tizeba waliokuwa wananuna nuna ole wenu niwasikie mnanuna, ole wenu niwasikie mnanuna. Mimi nimefanya miaka 10, Shigongo nae aanze hii mitano aende kumi akibarikiwa na Mwenyezi Mungu, ndivyo ilivyo.

Kazi yetu sisi Mheshiwa Rais, wazalendo wa kweli ni kutii mamlaka. Maamuzi yakifanyika ya waannchi ndio mamlaka yenyewe, maamuzi yakifanyika ya wananchama ndio mamlaka yenyewe, kazi yetu ni kutii.

Magufuli Misungwiii.jpg
 
Hivi aliyesema Wote wanaoishi Mwanza ni Wasukuma ni nani? kama kuna Mmeru hawezi kuelewa anapoongea Kisukuma.
 
Leo Misungwi Mwanza mgombea ccm na Rais wa Tz, katamka akiwapongeza mbunge Mnyeti na Madiwani huko kupita bila kupingwa na kutoa angalizo yapo mapingamizi. Ni wakati muafaka NEC kutimiza wajibu wenu kwa kutoa maamuzi kurejesha HAKI na amani kwa umoja na ustawi wa taifa letu.
 
Too many problem solving discussions end up focusing all of the attention of all the people present on what happened in the past and who is to blame.
 
Back
Top Bottom