Seneti nchini Marekani limepiga kura kuendelea na mchakato wa mashitaka dhidi ya Rais wa zamani Donald Trump, likisema mchakato huo ni wa kikatiba

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Baraza la Seneti lilipiga kura 56 kwa 44 za kuendelea na kesi dhidi ya Trump, likizipinga hoja za mawakili wake kwamba Rais hawezi kushtakiwa pindi anapomaliza muda wake.

Maseneta ambao waliapishwa kama wazee wa baraza, walipitia picha za vidio za wafuasi wa Trump wakipambana na polisi, kuvamia kumbi za bunge na kupeperusha bendera za Trump. Pia kuliwasilishwa vidio za Trump mwenyewe akiwahimiza wafuasi wake kabla ya uvamizi kuwa wapambane hadi tone la mwisho kupinga kushindwa kwake kwenye uchaguzi wa Novemba 3.

Kiongozi mkuu wa mashitaka hayo Jammie Raskin aliwaeleza maseneta kwamba kesi hiyo itawasilisha "ukweli mgumu" dhidi ya Trump. "Rais Trump ametuma mawakili wake hapa leo kujaribu kuzuia Bunge la Seneti kusikia ukweli wa kesi hii. Wanataka kuzima kesi kabla hata ya ushahidi wowote kutolewa. Hoja yao ni kwamba ikiwa unafanya makosa ya kushitakiwa katika wiki zako za mwisho mamlakani, basi unafanya ukiwa na kinga ya kikatiba na unanusurika".
 
Unapopewa malimao na adui wewe yatengenezee juisi tamu ya lemonade.

Hapa Trump atakomaa na hii kesi mpaka 2024 maana inampa sana publicity.

Channel ya white house leo Biden alikuwa na watazamaji wachache sana kwasababu wengi wapo kucheki impeachment ambayo haitakuja kuwezekana (zinahitajika kura 67 kati ya 100)
 
ukweli ni kuwa hawataweza pata 2 ya 3
Mkuu kwa ushahidi mpya wa cct camera ulioonyeshwa leo, ki ukweli cjui kama atachomoka!!kumbe ilikuwa ni balaa!!hata hao wenzake (republican), waliponea tundu la sindano!!nadhani kwa hizo video mpya zilioonyeshwa leo hii zitawabidirisha wengi sana ki mtizamo!!na kumuona trump ni kiumbe ambaye hafai kabisa kwa ulimwengu uliostarabika!!yaani hata hao wanaomtetea sijui unakuwa na ujasiri gani, kwa ushahidi huu!!ila askari wa ulaya kweli ni askari na sio roboti, ki ukweli kama ni kule porto rico, wale waandamanaji, yangetokea mauji ya haraiki!!!!hata kama wakiamua kutanguliza u chama mbele, historia itawahukumu !!na kama wangemkuta makamu wa rais ofisini alikuwa anauawa!!
 
Askari walivumilia tu kwa sababu majority ya walioingia kule capitol hill ni wazungu,angalia jinsi hao hao askari walivyokua wanaua weusi kwny BLM.
 
Back
Top Bottom