Seneta wa zamani wa Haiti akamatwa Jamaica kwa mauaji ya Rais

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Polisi nchini Haiti imesema seneta wa zamani ambaye ni mshukiwa mkuu katika mauaji ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Jovenal Moise ametiwa mbaroni nchini Jamaica.

Msemaji wa jeshi la polisi Gary Desrosiers [Derosieri] ameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba John Joel Joseph yuko chini ya ulinzi katika mahabusi. Hakuna taarifa zaidi zilizopatikana kuhusu kukamatwa kwake.

Wakati hayo yakijiri kamanda wa jeshi la polisi nchini Jamaica Stephanne Lindsay ameliambia shirika la habari hilo hilo kwamba watu wengine wamekamatwa pamoja na Joseph na maafisa wanajaribu kubaini ikiwa ni jamaa wa familia.

Kamanda huyo amethibirisha watu hao walikamatwa Jumamosi alfajiri lakini akakataa kutoa taarifa zaidi. Watu waliokuwa na silaha waliyavamia makazi binafsi ya rais Moise katika vilima vya mji wa Port-au-Prince Julai saba mwaka uliopita na kumuuwa kwa risasi.

DW Swahili
 
Mamlaka nchini Jamaica imemkamata Seneta wa zamani wa Haiti Bw. John Joel Joseph kama mshukiwa namba moja wa mauaji ya Rais wa zamani wa Haiti Jovenel Moise.

Rais Moise aliuawa tarehe 7 Julai Mwaka jana na watu wenye silaha waliovamia nyumbani kwake katika mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince

Mara baada ya mauaji hayo, Kiongozi mmoja wa juu wa Polisi nchini humo alitoa taarifa kuwa Bw. Joseph ndiye aliyewapatia silaha majambazi hao na pia alifanya nao mikutano kadhaa. Bw. Joseph alikamatwa juzi.
 
Back
Top Bottom