Seneta wa Marekani akiri kuwa kuendelea kuisaidia Ukraine hakusaidii na ni hatari kwa Usalama wa Marekani

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
May 31, 2018
8,638
16,566
Rand Paul, seneta wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican amemlaumu Joe Biden kwa kuendelea kuipa Ukraine misaada ya kila namna ya kijeshi na kuonya kuwa, kitendo hicho kinahatarisha usalama wa kitaifa wa Marekani.

Seneta huyo ameandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa, mimi nimekula kiapo cha kulinda katiba ya Marekani si katiba ya nchi nyingine yoyote.

Amesema: "Baraza la Congress linaendelea na juhudi zake za kupasisha muswada wa matumizi ya fedha za taifa - muswada ambao nina yakini hakuna yeyote aliyeusoma - na nina uhakika kuwa hakuna udhibiti wowote wa matumizi ya fedha za taifa."

Baraza la Wawakilishi la Marekani hivi karibuni limepasisha msaada wa takriban dola bilioni 40 kwa Ukraine na kupeleka muswada huo kwa Baraza la Sanate la nchi hiyo. Iwapo muswada huo utapasishwa na Baraza la Sanate, kitakachobakia ni kutiwa saini tu na Joe Biden ili uwe sheria.

Kama muswada huo utakuwa sheria, utaifanya Marekani ivunje rekodi katika misaada yake kwa Ukraine. Itakuwa imeipa nchi hiyo ya Ulaya Mashariki msaada wa karibu dola bilioni 60 katika kipindi cha muda mfupi tu.

Matumizi hayo ya kiholela ya fedha za taifa huko Marekani yanafanyika katika hali ambayo, mgogoro wa kupanda bei ya mafuta unaendelea kuvunja rekodi nchini humo na hivi sasa bei ya bidhaa hiyo muhimu imevunja rekodi ya historia ya Marekani baada ya kupanda tena.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Jumuiya ya Wenye Magari ya Marekani imesema kuwa, bei ya mafuta inazidi kuvunja rekodi siku baada ya siku nchini humo.

Ijapokuwa bei ya mafuta imepungua kwa asilimia 7 katika soko la dunia tangu mwezi Machi, lakini bei ya bidhaa hiyo muhimu imepanda kwa asilimia 9.4 huko Marekani. Marekani imeomba msaada kwa Brazil lakini imekataliwa.
 
Pro Putin mnalia sana kipindi hiki na kule Donbas mmekimbizwa hapa Sweden and Finland wanajiunga NATO zinakuwa nchi 32 kumbuka Sweden and Finland wanapakana na Russia kwa 1440km

USSR
Distance ndogo sana hiyo.... Lazima wakina PUT IN waweweseke.
 
Hata uje na ngonjera gani haibadilishi ukweli wa mambo huko, tunaendeendeleza dozi
Ungekuwa unaendeleza dose usingekuja na thread za kulia lia kama hii,unakwenda kwa Beberu Mkuu unaokoteza vihabari unavileta hapa vya kukufanya upate ahueni ya moyo. Msaada utakwenda Ukraine kwa wingi tu,Russia kaeni kwa kutulia
 
Sisi tunafanya kwa vitendo
Ungekuwa unaendeleza dose usingekuja na thread za kulia lia kama hii,unakwenda kwa Beberu Mkuu unaokoteza vihabari unavileta hapa vya kukufanya upate ahueni ya moyo. Msaada utakwenda Ukraine kwa wingi tu,Russia kaeni kwa kutulia
Sisi hatuyaelewi hayo maneno yenu , Hawa maofisa wa marekani tuliowadaka watatusaidia kujenga miji ya Ukraine iliojotangazia uhuru wake, watajenga miji hio kama vile madaraja, school, vituo vya mabasi, viwanda, mols, masoko, barabara nk bila ya malipo, na hawa uzuri wake hamna prisoner change kwa sababu wametoka nje ya Ukraine
20220516_091634.jpg
 
... Seneta mjinga huyo! Congress imefikia maamuzi ya kuisaidia Ukraine yeye ni nani mtu mmoja apingane na Congress?
 
... Seneta mjinga huyo! Congress imefikia maamuzi ya kuisaidia Ukraine yeye ni nani mtu mmoja apingane na Congress?
Kwamba ww ni mwerevu, mwenye nchi yake haumii unaumia ww huku mtongani , asee huwaga mnaniwacha hoi
 
Back
Top Bottom