Senene kuongezwa kwenye orodha ya vyakula vinavyotolewa kwenye ndege katika safari za kimataifa nchini Uganda.

Artificial intelligence

JF-Expert Member
Jan 28, 2021
1,262
2,191
Baada ya kusambaa kwa video inayomuonesha mchuuzi wa Senene aliyekuwa akiuza bidhaa zake ndani ya Ndege ya Shirika la Ndege la Uganda, Shirika hilo limesema linafikiria kuongeza Senene (Nsenene) katika orodha ya vyakula ndani ya ndege katika safari za kimataifa zinazofanywa na ndege zake.

Awali, video hiyo ilizua hisia tofauti kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, wengi wakijiuliza, mchuuzi huyo aliweza vipi kupenyeza na bidhaa hiyo katika uwanja wa ndege na kufanikiwa kuiza, huku wengine wakimpongeza kwa ‘ujasiri’ wake.

Shirika la Ndege la Uganda limekiri kuwa Wasafiri wa ndege hiyo, aina ya Airbus A330 iliyokuwa ikitoka Uwanja wa Entebbe kwenda Dubai Novemba 26, 2021, walionekana kufurahia bidhaa hiyo, na kuwa wamejifunza kutokana na tukio hilo. Shirika hilo limesema litatumia fursa hiyo kukuza utamaduni wa vyakula vya asili vya Uganda duniani.

ATCL hii ni FURSA kwenu ichangamukieni pia.

Chanzo; Jamii forum App

UGANDA: Shirika la Ndege la #Uganda limetangaza kuongeza Senene katika orodha ya Vyakula vinavyotolewa kwenye Ndege katika safari zake za Kimataifa

Hatua hiyo imekuja baada ya Wasafiri kufurahia Senene waliokuwa wanauzwa na mchuuzi ktk Ndege

Soma Uganda Airways kuongeza Senene katika orodha ya vyakula ndani ya ndege baada ya video ya mchuuzi kusambaa mitandaoni

#JFLeo https://t.co/WnGErA7mkC
Screenshot_20211128-131620-1.jpg
 
Ndiyo lazima wasimamishwe walifanya uzembe mkubwa sana, abiria hadi anapanda na senene na kuuza ndani ya ndege walikuwa wapi?, Kosa kubwa hilo japo imegeuka fursa, ila lazima wawajibishwe kwa huo uzembe, baada ya serikali kuchukua hatua hizo, imeona iwe fursa pia kwao kutangaza vyakula vya utamaduni wao.
 
Ndiyo lazima wasimamishwe walifanya uzembe mkubwa sana, abiria hadi anapanda na senene na kuuza ndani ya ndege walikuwa wapi?, Kosa kubwa hilo japo imegeuka fursa, ila lazima wawajibishwe kwa huo uzembe, baada ya serikali kuchukua hatua hizo, imeona iwe fursa pia kwao kutangaza vyakula vya utamaduni wao.

Kwa hiyo ni habari 2 tofauti
Moja ruksa na nyingine kufukuzwa
 
Back
Top Bottom