Senegali waandamana kupinga Mgao wa Umeme.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Senegali waandamana kupinga Mgao wa Umeme....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mzee wa njaa, Jun 28, 2011.

 1. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
 2. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  mimi naona niwawekee kabisa msipate shida.
  Senegal waandamana kupinga mgao wa umeme
  Maandamano yamezuka katika mji mkuu wa Senegal, Dakar na katika jiji la kusini la Mbour kutokana na ukosefu wa umeme. Jijini Dakar, majengo kadhaa ya serikali yalichomwa moto, zikiwemo ofisi za shirika la umeme la serikali - Senelec.
  [​IMG] Maandamano Dakar


  Majeshi ya usalama katika mji wa Mbour yalipiga mabomu ya machozi kutawanya maelfu ya waandamanaji.
  Tatizo la ukataji umeme, ambao umedumu kwa saa 48 katika maeneo kadhaa, limekuja wiki moja tu baada ya kutokea maandamano dhidi ya rais.
  "Mamia ya vijana walivamia ofisi za Senelec na kuzichoma moto," amesema mkazi mmmoja wa Dakar, Ismail Diop akikaririwa na Reuters.
  Chupa zilizovunjwa, mabaki ya majengo na matairi yaliyochomwa moto vimetapakaa mitaani, amesema mkazi huyo.

  Mjini Mbour, karibu kilomita 80 kusini mashariki mwa Dakar, ofisi za shirika la umeme pia zilishambuliwa. watu walioshuhudia walisema ofisi za Senelec zilivunjwa na magari yaliyoegeshwa nje kushambuliwa pia.
  Senelec imeshindwa kutoa huduma ya umeme ya kuridhisha kwa miaka mingi.
  Wiki iliyopita, kulikuwa na maandamano mjini Dakar, yaliyotokana na pendekezo la rais Abdoulaye Wade kutaka kubadilisha katiba.
  Maandamano hayo yalikuwa ya kiwango ambacho hakijawahi kuonekana katika kipindi cha miaka 11 ya utawala wa Bw Wade.

  Gharama za maisha
  Rais huyo alitaka kupunguza kiwango cha asilimia kinachohitajia kushinda urais kutoka asilimia 50 hadi 25 ili kuepuka duru ya pili katika uchaguzi.
  Wakosoaji wamesema marekebisho hayo ya katiba yamelenga kuhakikisha Rais Wade, ambaye ana umri wa miaka 85, anachaguliwa tena mwakani.
  Bw Wade alingia madarakani katika uchaguzi wa kidemokrasia, lakini sasa anakabiliwa na ongezeko la hasira kutoka kwa wananchi kutokana na matatizo ya umeme ya kila siku na kupanda kwa gharama za maisha.
   
 3. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kwa hili la watu kuandamana kutokana na ukosefu wa umeme linashangaza sana kwa nchi ya Senegal kwani serikali ya rais Abdulwaye Wade inasifika kwa kuwawajibisha watendaji.

  Miaka kadha iliyopita Rais huyo alimtimua waziri wake mkuu na baraza lake lote la mawaziri kutokana na serikali kuchelewa kupeleka vikosi vya uokoaji wa meli moja ya nchi iliyozama ufukweni mwa Senegal ambapo watu wapato 1,500 walipoteza maisha.

  Linganisha hiyo na hapa kwetu ambapo zaidi ya watu 1,000 walizama ktk ziwa Victoria mwaka 1996 ambapo hakuna mtendaji yoyote mkuu wa serikali aliwajibishwa. Mwaka 2004 wato 300 walikufa ktk ajali ya treni karibu na Dodoma kutokana na uzembe na hakuna katika watendaji wakuu wa serikali aliyewajibishwa
   
 5. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,250
  Likes Received: 823
  Trophy Points: 280
  Its time to wake up!! Tuamueni kulisahau kabisa hili shirika mtaji wa wanasiasa (Tanesco), hatuwezi kuwa karne ya 21 harafu hatuna huduma ya umeme.
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Nchi hii: halafu ghafla january Makamba anakuja na spin yake eti Tanesco ni swafi!!!!
   
 7. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 15,806
  Likes Received: 8,630
  Trophy Points: 280
  they say ‘the world is spining around’ i see & i say the world is upside down!!
   
 8. notmar

  notmar Member

  #8
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  wakati mgao wa umeme unaendelea tena bila ratiba maalum serikali imepandisha bei ya mafuta ya taa!
   
 9. M

  Mwambao Member

  #9
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni rahisi sana kuwaonganisha wasenegal lakini si wabongo maana sisi wabongo tumegawanyika toka miaka ya ukoloni.
   
 10. peck

  peck JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 205
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  chadema wamechochea. wanatafuta umaarufu.
   
Loading...