Kila la heri timu ya Taifa, Taifa Stars

CHADEMA

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
488
2,468
TAARIFA KWA UMMA

KILA LA HERI TIMU YA TAIFA, TAIFA STARS

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kupitia kwa Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe. Freeman Mbowe kimetuma salaam za kuitakia kila la heri Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu, Taifa Stars na kuwatia ari wachezaji na makocha wao wakiongozwa na Ndugu Emmanuel Amunike, wakati timu hiyo inaelekea kuanza mchezo wake wa kwanza katika Mashindano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2019) usiku wa leo, jijini Cairo, nchini Misri.

Kupitia ujumbe huo, Mwenyekiti Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Jimbo la Hai, ametoa wito kwa Watanzania wote bila kujali tofauti za itikadi zao, kushikamana kwa pamoja katika kuishangilia na kuitakia mafanikio Taifa Stars.

"Timu yetu ya Taifa leo usiku inaanza rasmi mashindano ya AfCON, Cairo, Misri. CHADEMA inawasihi Watanzania wote wa itikadi zote kushikamana katika kuitakia mafanikio timu yetu ya Taifa Stars. Michezo ni uchumi, afya, upendo, heshima, umoja na burudani. Tuitumie AFCON kujirekebisha," amesema Mwenyekiti Mbowe.

Timu ya Taifa Stars ambayo imepangwa Kundi C pamoja na timu za Senegal, Algeria na Kenya, itacheza mechi yake ya kwanza Jumapili, Juni 23, 2019 dhidi ya Timu ya Taifa ya Senegal, katika mchezo utakaopigwa June Stadium, jijini Cairo, nchini Misri, kuanzia saa 2 usiku.

Kila la heri Taifa Stars.
Kila la heri Watanzania.

Imetolewa leo Jumapili, Juni 23, 2019 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
 
1136625

Imekua ni siku iliyosubiriwa na Watanzania mbalimbali kuona timu yao ya Taifa (Taifa Stars) ikicheza mechi yake vs Senegal kwenye michuano ya AFCON 2019 ambapo mpaka mpira unaisha matokeo ni Senegal 2-0 Tanzania, magoli ya Senegal yamefungwa na Balde kwenye dakika ya 28 na goli la pili limefungwa kwenye dakika ya 64 na Diatta.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom