Sen: John Kennedy amwambia Mark Zuckerberg wa Facebook asitumie kiswahili kwenye user agreement

RGforever

JF-Expert Member
Apr 3, 2011
6,878
5,424
Nimefuatilia Kwa Muda Kama Masaa Manne hivi weekend hii kuhusu sakata la Kijana Wetu Mark la Kuvuja kwa Data zaidi ya Mil 87 za Watumiaji wake.

Na Alipoitwa kwenye Congress senate mmoja anaeitwa John Kennedy nimemuona kama Anauelewa mdogo sana Wa Mambo ya Internet na akafikia Hatua Akamwambia Mark atumie Lawyers wake waandike upywa User agrerment na Kwamba Asitumie Swahili language kwenye User Agreement zake za Facebook ili Mtu wa Kawaida Wa Marekani aweze Kuelewa..

Is Facebook Only in America?. Senator Mkubwa kiasi hicho unashindwa Kujiuliza Swali dogo kama Hili... They only care about America.

Nimekuwekea Linknhapo Chini.. Unaweza Ku-skip mpk kuanzia Dakika ya kwanza na Kuendelea
 
Na huku Jf tunaomba Melo aondoe English kwenye user agreement ili tuweze kwenda nao sawa hawa mabwigila siyo kila kitu lazma tulilie lie, ingekuwa ni nchi zinazo ongea kiswahili na wanajielewa ungekuta wamesha piga marufuku huo mtandao nchini mwao lakini sis wa dunia ya 4 hakuna namna
 
sijawahi kusoma kwenye hayo ma agreement kwanza yanakua marefu pili mengi hua kwa lugha ya kigeni tatu aina zooote za kwenye internet hua naona ni kama nacheza game tuu na hua siruhusu vitu vyangu vya maana kua humo wala sina siri wakitaka hu ni hack hakuna cha maana ninacho fanya humo yaani kifupi mimi na Internet ni 0.0%
 
Kitu ambacho watu weusi hatujui ni kuwa teknolojia au innovation yoyote huwa inagunduliwa kwa interest za wenyewe kwanza watu weupe.....na sisi huwa tunafuata au kutumia hiyo teknolojia au innovation kwa kufuata interest zao........

Wazungu wanagundua sana teknolojia kwa ajili ya kuwarahishia wao kwanza changamoto za mazingira yanayowazunguka........na huwa tunatumia baada ya kuvutiwa nayo
 
Alimaanisha nini

Alimaanisha kisitumike Kiingereza ambacho Mmarekani wa kawaida akisoma ni kama anasoma lugha ya kigeni.

Ukimwambia Mmarekani kitu ambacho hakielewi japo ni Kiingereza wao hupenda kusema “you might as well say it in Chinese” akimaanisha ulichokisema kwangu ni kama Kichina tu. Huyu Mbunge hapa ametumia neno Swahili katika mantiki hiyo.

Hakuna User Agreement ya Facebook ya Kiswahili.
 
Alimaanisha kisitumike Kiingereza ambacho Mmarekani wa kawaida akisoma ni kama anasoma lugha ya kigeni.

Ukimwambia Mmarekani kitu ambacho hakielewi wao hupenda kusema “you might as well say it in Chinese” akimaanisha ulichokisema kwangu ni kama Kichina tu. Huyu Mbunge hapa ametumia neno Swahili katika mantiki hiyo.

Hakuna User Agreement ya Apple ya Kiswahili.
Asante nimeelewa
 
Alimaanisha kisitumike Kiingereza ambacho Mmarekani wa kawaida akisoma ni kama anasoma lugha ya kigeni.

Ukimwambia Mmarekani kitu ambacho hakielewi wao hupenda kusema “you might as well say it in Chinese” akimaanisha ulichokisema kwangu ni kama Kichina tu. Huyu Mbunge hapa ametumia neno Swahili katika mantiki hiyo.

Hakuna User Agreement ya Facebook ya Kiswahili.
Nimefikilia sana hilo jambo, user agreement ya kiswahili? Hapo umedadavua vizuri sana.
 
Kiswahili ni Lugha iliyopitwa na wakati ni bora hapa Tz tubadilishe lugha tutumie English Only.
 
Alimaanisha kisitumike Kiingereza ambacho Mmarekani wa kawaida akisoma ni kama anasoma lugha ya kigeni.

Ukimwambia Mmarekani kitu ambacho hakielewi japo ni Kiingereza wao hupenda kusema “you might as well say it in Chinese” akimaanisha ulichokisema kwangu ni kama Kichina tu. Huyu Mbunge hapa ametumia neno Swahili katika mantiki hiyo.

Hakuna User Agreement ya Facebook ya Kiswahili.

Upo sahihi kabisa.
 
Back
Top Bottom