Semina ya Mwakasege jana KKKT Mbezi Beach na vioja vyake

Onyix

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
682
788
Habari wakuu,

Moja kwa moja nianze na mada husika hapo juu.. jana ilikuwa ni semina ya Mwl. Mwakasege kwa wanaume wote pale mbezi beach KKKT. Nami nilikuwepo kwenye hiyo semina na kuna mambo niliona na nilifanya kiujitafiti flani hivi.

Kwanza nilifika pale kwenye semina mida ya saa nne hivi nikitokea kwangu ingawa muda wa seminar ilikua sa tatu asubuhi. Hii ilichagizwa na mkesha wa jana sehemu mbalimbali za starehe tukiwa na marafiki ambao hatujaonana muda kidogo toka tumalize A' level enzi hizo.

Turudi kwenye mada, baada ya kufika pale kwanza nilikua na hangover ya ajabu nilivyo fika geti la kanisa nikamuona dada mmoja mlinzi nikamuuliza ndani ya kanisa kuna duka hata nipate energy drink nikate usingizi na mning'inio akasema hakuna duka labda nisogee mbele mkono wangu wa kushoto kuna Baa na Duka wanauza vinywaji hapo.

Basi nikasogea pale kufika nakuta waumini kibao na Biblia zao wanakata hangover kwa maji baridi, soda, supu na mtori. Nilijua nitajikuta peke yangu kumbe kuna wenzangu kibao wenye matatizo kama yangu, basi tukajumuika pale kwa pamoja kutafuta energy ya kwenda kumeza neno la mwalimu.

Wakati tukifanya yetu pale nikaangalia sura za wanaume pale karibu wote walikua wanaonyesha jana yake walitwagwa kwa nyundo ya ulevi yani wapo nyang'a nyang'a, wakati tunapiga story kila mtu akawa anaelezea chanzo cha yeye kuja leo eneo la tukio (Seminar).

Nikakugundu pia wengi wetu sio upako ulio tuleta wala utashi bali ni "external force behind us" jamaa wa kwanza akasema toka tangazo la hiyo semina limetoka, mke wake kamkomalia akiamka akilala mke kamganda lazima aende, mwingine anasema mimi mke wangu kanileta mpaka getini kahakikisha nimeingia ndani kama anampeleka mtoto wa chekechekea shule.

Mwingine anasema leo nimenunuliwa daftari na peni ili niandike kitakachoongelewa nisirudi mikono mitupu na mke wangu anasubri nikirudi nyumbami nimfundishe nilichojifunza, mwingine alisingizia eti hana hela anaenda kutafuta pesa. Mke wake kazama kwenye mkoba kampa laki anasema hela hiyo hapo kwaiyo hakuna sababu.

Mwingine kanuniwa kama hataki kwenda in short sababu zilikua nyingi sana sana, mimi niliambiwa tu kama sitaenda kwenye semina nibaki huko huko na huyo anaenipiga biti ni mchumba tu sasa hao wenye wake kabisa si do hatari.

Kwa kajiutafiti kangu haka nikagundua wanawake week hii wamefanya mapinduzi ya [HASHTAG]#Mangekimambi[/HASHTAG] maana wanaume tulijaa barabara ya hapo Mbezi kama zoezi la utayari la wale ndugu zetu waoga.

Ndani ya Semina sasa kila mtu na maji baridi na ikimuona amelala hakuna kumshtua unajua upako unaingia na roho mtakatifu anatenda kitu ndani yake sasa kwa sababu wameambiwa waandike, akishtuka tu usingizini anakuomba note book a copy vifungu vilivyo mpita wakati pepo la usingizi lilipo mchukua.

In short jana niliona mengi ila kubwa zaidi nawashukuru wamama na wadada kwa kazi kubwa mliyoifanya the turn up was good, nyomi lilikua la kufa mtu japo nusu yake walikua na weekend fever.

Asanteni
 
Hatari sana hii, inabid kuwe na muendelezo wa ili tufike atua wanaume tuzoee
 
Tueleze na content ya semina ambao hatukwenda tujifunze japo kidogo.
SOMO: UTUZWAJI WA UZAO WA KIUME KTK JAMII KIBIBLIA
1524986868723.jpg
 
Habari wakuu
Moja kwa moja nianze na mada husika hapo juu.. jana ilikuwa ni seminar ya Mwl. Mwakasege kwa wanaume wote pale mbezi beach KKKT. Nami nilikuwepo kwenye hiyo seminar na kuna mambo niliona na nilifanya kiujitafiti flani hivi.

Kwanza nilifika pale kwenye seminar mida ya nne hv nikitokea kwangu ingawa muda wa seminar ilikua sa tatu asubh.. hii ilichagizwa na mkesha wa jana sehemu mbalimbali za starehe tukiwa na marafiki ambao hatujaonana muda kidogo toka tumalize A' level enzi hizo. Turudi kwenye mada, baada ya kufika pale kwanza nilikua na hangover ya ajabu nilivyo fika geti la kanisa nikamuona dada mmoja mlinzi nikamuuliza ndani ya kanisa kuna duka hata nipate energy drink nikate usingizi na mning'inio.. akasema hakuna duka labda nisogee mbele mkono wangu wa kushoto kuna Baa na Duka wanauza vinywaji hapo.

Basi nikasogea pale kufika nakuta waumini kibao na biblia zao wanakata hangover kwa maji baridi, soda, supu na mtori.. nilijua ntajikuta peke yangu kumbe kuna wenzangu kibao wenye matatizo kama yangu, basi tukajumuika pale kwa pamoja kutafuta energy ya kwenda kumeza neno la mwalimu.

Wakati tukifanya yetu pale nikaangalia sura za wanaume pale karibu wote walikua wanaonyesha jana yake walitwagwa kwa nyundo ya ulevi yani wapo nyang'a nyang'a, wakati tunapiga story kila mtu akawa anaelezea chanzo cha yeye kuja leo eneo la tukio (Seminar).

Nikakugundu pia wengi wetu sio upako ulio tuleta wala utashi bali ni "external force behind us" jamaa wa kwanza akasema toka tangazo la hiyo seminar limetoka, wife wake kamkomalia akiamka akilala wife kamganda lazima aende, mwingine anasema mimi wife kamilete mpaka getini kahakikisha nimeingia ndani.. kama anampeleka mtoto wa chekechekea shule.

Mwingine anasema leo nimenunuliwa daftar na peni ili niandike kitakacho ongelewa nisirudi mikono mitupu na wife anasubri nikirudi home nimfundishe nilichojifunza, mwingine alisingizia eti hana hela anaenda kutaguta pesa.. wife ake kazama kwenye mkoba kampa laki anasema hela hyo hapo kwaiyo hakuna sababu.

Mwingine anuniwa kama hataki kwenda in short sababu zilikua nyingi sana sana..mimi niliambiwa tu kama sitaenda kwenye seminar nibaki huko huko.. na uyo anae nipiga biti ni mchumba tu.. sasa hao wenye wake kabisa si do hatari..

Kwa kajiutafiti kangu haka nikagundua wanawake week hii wamefanya mapinduzi ya [HASHTAG]#Mangekimambi[/HASHTAG] maana wanaume tulijaa barabara ya hapo Mbezi kama zoezi la utayari la wale ndugu zetu waoga.

Ndani ya Seminar sasa kila mtu na maji baridiiiii na ikimuona amelala hakuna kumshtua unajua upako unaingia na roho mtakatifu anatenda kitu ndani yake.. sasa kwa sababu wameambiwa waandike, akishtuka tu usingizini anakuomba note book a copy vifungu vilivyo mpita wakati pepo la usingizi lilipo mchukua..

In short jana niliona mengi ila kubwa zaidi nawashukuru Wamama na Wadada kwa kazi kubwa mliyoifanya the turn up was good.. nyomi lilikua la kufa mtu japo nusu yake walikua na weekend fever.. Asanteni
jamaa huwa anapoteza muda wake, sema anawakusanyia sadaka mno, anapata hela nyingi sana za sadaka ila matunda zero. huwezi kumfundisha semina mtu ambaye hajaokoka, ndio maana wanajaagaa akiondoka wanarudi kwenye maisha yao ya zamani wanasubiria yeye alete tena semina wajae tena wamletee sadaka. hamna kitu hapo. kwa wanaoelewa wameelewa, wasioelewa mtasubiri sana.
 
jamaa huwa anapoteza muda wake, sema anawakusanyia sadaka mno, anapata hela nyingi sana za sadaka ila matunda zero. huwezi kumfundisha semina mtu ambaye hajaokoka, ndio maana wanajaagaa akiondoka wanarudi kwenye maisha yao ya zamani wanasubiria yeye alete tena semina wajae tena wamletee sadaka. hamna kitu hapo. kwa wanaoelewa wameelewa, wasioelewa mtasubiri sana.
Baada ya kila semina huwa anawaita watu kuokoka... wenye uhitaji huo.. na hapo hawezi mlazimisha mtu kuokoka hiyo na hiari na nafsi ya mtu... na ukiwa katika wokovu sio kwamba huwezi anguka tena dhambini... ndo maana unatakiwa uwe karibu na Mungu wako na ujiepushe na mazingira yatayo kupelekea kwenye dhambi... hata Bwana wetu YESU katika safari yake ya wokovu wetu alianguka mara 3 hii ina maana sana kiroho
 
Back
Top Bottom