Semina na Vikao vya awamu hii ni hatari kwa wenye vidonda vya tumbo

1468872661675.jpg


Ole wako uchukue Sambusa mbili!!
 
Hahahahahahaaaa mahindi ya kuchemsha na maji ya kunywa? Huku ni kukoseana heshima!
 
lakini ukipiga hesabu ya bei ya hindi moja ni Tsh 1000 na sambusa moja ni Tsh 1000. Sasa hapo ni aina ya kibwagizo au bei ya kibwagizo? Wacha muvi iendelee.

Hhhhhhaahhaaa sambusa moja hushibi ila hilo hindi moja ukipga na maji swaaaafi kabsa na unarud mzigoni
Hapa kazi tu
 
Niliwaambia wanunue karanga za jumla wakaange kubana matumizi..

Hawaoni kama mahindi na hiyo soda na maji ni gharama Sana?

Hiyo pesa tungetengeneza madawati mengi tu..

Nitaagiza atumbuliwe aliyeandaa bajeti..!!
 
Ndio hivyo mkuu. Mimi mwenyewe ni mtumishi wa umma kwa zaidi ya miaka kumi, nilianza enzi ya mzee wa malofa, hali ya vikao kwa sasa ni ngumu kumesa. Zamani ilikuwa ni mwendo wa mabagia, fulu menyu na li juisi kopo zima kwa kila mtu na bahasha nzito. Kwa sasa mwisho wa kikao unapewa asante ya mdomo. Ni maumivu hakunaga. Kwa sasa mimi vikao vingi natoa udhuru, sihudhurii kwani havina mvuto.

Unasikitisha sana kama haupendi kazi yako ondoka achia wengine watujengee nchi yetu, tena bora Mh. Magufuli aanze kuomba watu mnaotakiwa kuhudhuria mkikosa zaidi ya mara tatu mjieleze au kazi kwaheri.

Looo uvivu tu na labda hauna ujuzi na kazi yako. Unatia aibu kwa uliyoandika...beba pesa ukale unachotaka..

Orodha ya waliohudhuria inabidi ianzishwe kote serikalini
 
Vitu vingine ni kukomoana tuu. Hapo unakuta mtu na tai yake safi unapambana na mahindi ya kuchemsha mbele ya kamera
 
Mmeniacha wakuu wangu
Nacheka siyo kidogo..

Kwani hivyo vyakula vilikuwa forbiden kwenye menu za semina? Nadhani tunakuza soko la ndani
tatizo ni mambo mageni kwetu,mpaka tuje kuzoea itatuchukua miaka
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom