Semina elekezi ya Chadema

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa, amepanga kufanya ziara nchi nzima kuwafunda madiwani wa chama hicho.

Mwaka huu, CHADEMA kimeshinda halmashauri 12 za Mwanza Mjini, Musoma Mjini, Karatu, Moshi Mjini, Ukerewe, Kigoma Mjini, Mbulu, Arusha, Moshi Vijijini, Hanang, Mbeya Mjini na Iringa Mjini.

Dk. Slaa alitangaza azma yake hiyo jana katika mkutano wake wa ndani wa madiwani wa halmashauri ya mji wa Musoma Mjini na baadhi ya wabunge wa mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Madiwani wa CHADEMA na CUF wamemteua diwani wa kata ya Nyamatare, Alex Kisusura, kuwa Meya wa Manispaa ya Musoma, huku Angela Lima diwani wa Kamnyonge, akiteuliwa kuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Musoma Mjini.

Tayari ameshatembelea halmashauri ya Jiji la Mwanza ambako aliwapatia madiwani mbinu mbalimbali za kuongoza halmashauri hiyo, na kufanikisha uteuzi wa Meya wa jiji hilo Bwana Josephat Manyerere.

Tunawatakia mafanikio mema Chadema katika harakati zenu za ukombozi.
 
Angeunganisha semina elekezi hizi na mikutano ya wananchi kila anakopita ingekuwa bomba sana - two in one, cost effective!

Taabu tu ni kwamba watawala wanaweza kumnyima vibali vya kufanya mikutano kwa sababu zisizo na mashiko
 
Wananchi waliompigia kura , tungependa tumsikie anasema nini, hata apite tu kutoa shukurani kwa wananchi.
Jinsi ilivyo sasa wanannchi hawajui kinachoendela, ni kama amewaacha "solemba". Inahitajika aseme na wapiga kura wake.
 
Good news kwa dr.slaa na chadema....wasisahau bundi zitto kabwe anawanyemelea
 
daaaah yaani Dr.Slaa utadhani mwalimu wangu wa fizikia wakati niko shule...very stratergic na moves zake
 
Plan nzuri ila angalizo watu kama kina Zitto kabwe lazima washughulikiwe mapema ili mipango iende kama ilivyopangwa.
 
Mwaka huu, CHADEMA kimeshinda halmashauri 12 za Mwanza Mjini, Musoma Mjini, Karatu, Moshi Mjini, Ukerewe, Kigoma Mjini, Mbulu, Arusha, Moshi Vijijini, Hanang, Mbeya Mjini na Iringa Mjini..

Masahihisho:

CCM imeshinda katika Jiji la Mbeya kwa kuwa na jumla ya Madiwani 28 dhidi ya 18 wa Chadema; na pia CCM imeshinda Iringa Mjini ikiwa na jumla ya Madiwani 20 dhidi ya 2 tu wa Chadema.
 
CHADEMA ni lazima waweke uongozi wa mfano kwa uongozi wa 'chumia tumbo' wa CCM. Kwa kuwa nyuma yao kuna wananchi, ni lazima watafanikiwa. Wawaache CCM ambao nyuma yao kuna chama chao, wanachi wakiwa wametupwa mbali.
 
Back
Top Bottom