Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 302
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa, amepanga kufanya ziara nchi nzima kuwafunda madiwani wa chama hicho.
Mwaka huu, CHADEMA kimeshinda halmashauri 12 za Mwanza Mjini, Musoma Mjini, Karatu, Moshi Mjini, Ukerewe, Kigoma Mjini, Mbulu, Arusha, Moshi Vijijini, Hanang, Mbeya Mjini na Iringa Mjini.
Dk. Slaa alitangaza azma yake hiyo jana katika mkutano wake wa ndani wa madiwani wa halmashauri ya mji wa Musoma Mjini na baadhi ya wabunge wa mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Madiwani wa CHADEMA na CUF wamemteua diwani wa kata ya Nyamatare, Alex Kisusura, kuwa Meya wa Manispaa ya Musoma, huku Angela Lima diwani wa Kamnyonge, akiteuliwa kuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Musoma Mjini.
Tayari ameshatembelea halmashauri ya Jiji la Mwanza ambako aliwapatia madiwani mbinu mbalimbali za kuongoza halmashauri hiyo, na kufanikisha uteuzi wa Meya wa jiji hilo Bwana Josephat Manyerere.
Tunawatakia mafanikio mema Chadema katika harakati zenu za ukombozi.