Semina elekezi ni muhimu kwa Mawaziri wa Rais Magufuli

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,087
6,568
Mzee wa msoga aka Jakaya aliona mbali pale alipokuwa anasisitiza ufanyaji wa semina elekezi kwa viongozi.

Japokuwa mambo yalienda kombo baada ya kuonekana kuna matumizi mabaya ya ofisi. Hasa baada ya ile iliyofanyika Ngurdoto kuonekana ilitumia pesa nyingi za umma bila sababu ya msingi.

Lakini JPM ameingia madarakani hatuoni semina elekezi kwa wateule wake. Badala yake tunashuhudia vimbwanga pale wanapoenda kukagua shughuli za serikali

Ni kweli wanaweza kuwa wapo sahihi kuwaaibisha wale wanaokosea kwa kufanya kazi kinyume na maadili, lakini kusimamia watumishi wa umma pia kuendane na misingi ya sheria na utu.

Maana tunakoenda huko mbele kuna watu watawaburuta mahakamani mawaziri wa JPM na itakuja kuleta kizaazaa.

Hivyo kama ishu ilikiwa ni gharama na ufisadi kukwepa semina elekezi,basi zifanyike sasa huku zikifanyika kwenye kumbi za serikali,na mawaziri kunywa maji na bajia lakini waweze kufanya kazi kwa misingi ya sheria bila kupayuka hovyo na kushikia watu miuno.
 
Huyu field marshall ndio kaliamsha
Ni kweli unavyosema na nakuunga mkono
Sema dooh.. watu wa awamu wanamaind sana mishiko, hasa yule mzee, anajengea tu kwao
Shame on them mataga
 
Back
Top Bottom