Semina elekezi kwa mawaziri wapya May 8 2012/Jumanne

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,710
2,226
Mawaziri wapigwa 'stop'
Katika hatua nyingine mawaziri wote wamezuiwa kusafiri kikazi nje ya Jiji la Dar es Salaam kutokana na kile ambacho kinaelezwa kuwa ni maandalizi ya kukabidhi ofisi kwa mawaziri wapya ambao wanatarajiwa kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa.

Taarifa hizo zimekuja siku moja tu tangu Ikulu kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue kusema kuwa “Watanzania wasubiri Baraza bora la Mawaziri”.

Jana, taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari serikalini vililidokeza gazeti hili kuwa mawaziri wote sasa wamezuiwa kusafiri nje ya Dar es Salaam kutokana na kusubiri mchakato huo wa kukabidhiana ofisi.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, karibu mawaziri wote na naibu mawaziri walikuwepo jijini Dar es Salaam jana isipokuwa wachache ambao haikuthibitika mara moja kama walikuwapo au la.

Vyanzo hivyo viliongeza kwamba tayari Rais amekwishamaliza mchakato wa uteuzi na baraza jipya linatarajiwa kukutana na mkuu huyo wa nchi katika semina elekezi Jumanne ya Mei 8, mwaka huu.

Kwa wiki mbili mfulululizo sasa nchi imegubikwa na mjadala kwa watu wa kada tofauti kushinikiza kufanyika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri baada ya Bunge kutaka mawaziri wanane waliotajwa kwenye Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh wawajibike au wawajibishwe.

Mawaziri wanaotakiwa kuwajibishwa baada ya kushindwa kuwajibika ni Mustafa Mkulo (Fedha), Omary Nundu (Uchukuzi), Dk Hadji Mponda (Afya na Ustawi wa Jamii), Profesa Jumanne Maghembe (Kilimo, Chakula na Ushirika), Dk Cyril Chami (Viwanda na Biashara), George Mkuchika (Tamisemi), Ezekiel Maige (Maliasili na Utalii), William Ngeleja
(Nishati na Madini).
http://www.mwananchi.co.tz/componen.../22592-jk-apandisha-joto-uteuzi-mawaziri.html
MY TAKE;
So JK ana siku 4 kulitangaza na kuliapisha baraza jipya kabla ya semina elekezi!
Alafu kitengo cha mda wote huo hawa old minister wakiwa kwa transit si wanaweza poteza ushahidi wa kuwapeleka mahakani?Au ni strategy ya mkuu ili jamaa wasiende lupango mwisho wa siku kama dana dana za Yona na Mramba
 
Nadhani tulisubiri baraza jipy lenye ustadi wa kula bila kubainika na CAG.2shachoka na magamba
 
Aaache ubabashaji_achukue hatua ndio tutamwelewa.
 
Utakapotajiwa bajet ya iyo semina ndo utazimia!
Ifike wakati tuanze kuzitathmini izi semina kama zina matunda yoyote sio kwenda kula raha tuu na kufuja ela

Nashauri kila atakayepewa wizara akibiziwe na madudu ya mtangulizi wake kama yalivyotajwa na CAG na kamati za bunge na atoe mikakati namna ya kuhakikisha hayatokei hayo ie hayo madudu yawe sehemu ya KPI
 
Mawaziri wapigwa 'stop'

MY TAKE;
So JK ana siku 4 kulitangaza na kuliapisha baraza jipya kabla ya semina elekezi!
Alafu kitengo cha mda wote huo hawa old minister wakiwa kwa transit si wanaweza poteza ushahidi wa kuwapeleka mahakani?Au ni strategy ya mkuu ili jamaa wasiende lupango mwisho wa siku kama dana dana za Yona na Mramba

Kumbe sababu waijua halafu wajifanya kuuliza. Hapa wameambiwa hata kama tulikula wote, atakayeonekana kuchota ni weye, Chukua muda huu poteza ushahidi.
 
Nashauri wale ambao watarudi kwene baraza basi wasihudhurie hizo semina
 
hivi kwa nini wasifanye hizi semina online..au hawana akaunti za skype hawa???
 
Mawaziri wapigwa 'stop'

Katika hatua nyingine mawaziri wote wamezuiwa kusafiri kikazi nje ya
Jiji la Dar es Salaam kutokana na kile ambacho kinaelezwa kuwa ni
maandalizi ya kukabidhi ofisi kwa mawaziri wapya ambao wanatarajiwa
kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa.

Taarifa hizo zimekuja siku moja tu tangu Ikulu kupitia kwa Katibu Mkuu
Kiongozi, Ombeni Sefue kusema kuwa “Watanzania wasubiri Baraza bora la
Mawaziri”.

Jana, taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari serikalini
vililidokeza gazeti hili kuwa mawaziri wote sasa wamezuiwa kusafiri nje
ya Dar es Salaam kutokana na kusubiri mchakato huo wa kukabidhiana
ofisi.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, karibu mawaziri wote na naibu mawaziri
walikuwepo jijini Dar es Salaam jana isipokuwa wachache ambao
haikuthibitika mara moja kama walikuwapo au la.

Vyanzo hivyo viliongeza kwamba tayari Rais amekwishamaliza mchakato wa
uteuzi na baraza jipya linatarajiwa kukutana na mkuu huyo wa nchi
katika semina elekezi Jumanne ya Mei 8, mwaka huu.

Kwa wiki mbili mfulululizo sasa nchi imegubikwa na mjadala kwa watu wa
kada tofauti kushinikiza kufanyika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri
baada ya Bunge kutaka mawaziri wanane waliotajwa kwenye Ripoti ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh
wawajibike au wawajibishwe.

Mawaziri wanaotakiwa kuwajibishwa baada ya kushindwa kuwajibika ni
Mustafa Mkulo (Fedha), Omary Nundu (Uchukuzi), Dk Hadji Mponda (Afya na
Ustawi wa Jamii), Profesa Jumanne Maghembe (Kilimo, Chakula na
Ushirika), Dk Cyril Chami (Viwanda na Biashara), George Mkuchika
(Tamisemi), Ezekiel Maige (Maliasili na Utalii), William Ngeleja
(Nishati na Madini).
JK apandisha joto uteuzi mawaziri
MY
TAKE;

So JK ana siku 4 kulitangaza na kuliapisha baraza jipya kabla ya semina
elekezi!
Alafu kitengo cha mda wote huo hawa old minister wakiwa kwa transit si
wanaweza poteza ushahidi wa kuwapeleka mahakani?Au ni strategy ya mkuu
ili jamaa wasiende lupango mwisho wa siku kama dana dana za Yona na
Mramba
This yet another waste of public funds, semina elekezi Ngurdoto 1 na 2 zilizaa mchwa ndio hao wanatakiwa kufukuzwa so what makes any difference with another semina, usanii elekezi
 
Kumbe sababu waijua halafu wajifanya kuuliza. Hapa wameambiwa hata kama tulikula wote, atakayeonekana kuchota ni weye, Chukua muda huu poteza ushahidi.

Semina elekeziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii at the end of day yale yaleeeeeeeeeee, kama tunavyoaminishwa kuwa Baraza linalokuja litakuwa na ubora wa hali ya juuu sasa hiyo semina elekezi ya nini tena?
 
Semina elekezi inazaa matunda tulinayoyaona au vipi?
Hujakosea. Kwenye semina wanaelekezwa, pamoja na mambo mengine, kuwa akija mtendaji wa CCM kuomba pesa ya chama, shurti itafutwe toka kwenye fungu lolote serikalini. Ushahidi upo.
 
Back
Top Bottom