Semi Final 2, CECAFA: Zanzibar Heroes yaifunga Uganda goli 2 - 1! Sasa kukutana na Kenya katika mchezo wa fainali

Wahafidhina sijui kama ili wataaafiki kuvunja timu ya Tanganyika na tuwape Zanzibar nafasi hii
 
Mkuu zanzibar haina sifa ya kuwa mwanachama Fifa si ushabiki bali ni uhalisia.
Ndani ya fifa kuna mwanachama Tanzania ambayo Zaznibar inafahamika imo ndani ya Tanzania. Kwaiyo hapawezi kuwa na nafasi mbili kwa mwanachama mmoja.
Wales, Scotland, N.Irland wote ni wanachama kwasababu England hakujisajili fifa kama United Kindom. Wamejisajili kama ni England tu kwaiyo ndomana kila mtu akawa na nafasi yake ya kujiunga.

Kwaiyo ili zanzibar awe mwanachama Lakwanza Tanzania inatakiwa itoke ijisajili kama Tanganyika. Alafu ndo kuwe na Zanzibar na Tanganyika. hapo ndipo anaweza kutambulika.

Kaka maneno yako muafaka,kwani kwa kweli kama hawa watawala wa Zanzibar(Tanganyika) wangelikuwa na nia nzuri na na huu mungano wangeliwaiga wenzao Waingereza

Kwakweli muungano wa Tanganyika na Zanzibar hauna tafauti na muungano wa nchi ya Wales,Scotland,na England zilizounda Uk(United Kingdom) au Great Britain

kwa sababu michezo si siasa wenzetu waingereza wamejiunga kwenye FIFA kama nchi tafauti sio nchi moja

hii inasaidia kukuza michezo kwa nchi zilizoungana na zinazidisha ushindani wa michezo katika nchi zilizoungana

Lakini kwasababu Tanzania kila kitu kimewekwa kwenye siasa,hata michezo imewekwa kwenye siasa,hii inaifanya Zanzibar ikose fursa za kushiriki michezo ya kidunia

Serikali ya Mungano inabidi ifikirie upya katika kukuzisha michezo Tanzania,Inatakiwa Serikali ya mungano iwaige wenzao UK katika hili

Wales,Skotland,England wote wanatumia passport ya United Kingdom au Great Britain wanaposafiri,,(England, Wales, and Scotland considered as a unit. The name is also often used loosely to refer to the United Kingdom.)
 
Mkuu zanzibar haina sifa ya kuwa mwanachama Fifa si ushabiki bali ni uhalisia.
Ndani ya fifa kuna mwanachama Tanzania ambayo Zaznibar inafahamika imo ndani ya Tanzania. Kwaiyo hapawezi kuwa na nafasi mbili kwa mwanachama mmoja.
Wales, Scotland, N.Irland wote ni wanachama kwasababu England hakujisajili fifa kama United Kindom. Wamejisajili kama ni England tu kwaiyo ndomana kila mtu akawa na nafasi yake ya kujiunga.

Kwaiyo ili zanzibar awe mwanachama Lakwanza Tanzania inatakiwa itoke ijisajili kama Tanganyika. Alafu ndo kuwe na Zanzibar na Tanganyika. hapo ndipo anaweza kutambulika.

Na zaidi ya ayo, masuala ya michezo hayamo kabisa kwenye masuala ya muungano si kwenye mkataba wala kwenye katiba. Sasa inakuaje Tanzania iwakileshe kwenye michezo wakati haikutakiwa iwe ivo kila mmoja alitakaiwa ajiwakilishe kivake. Kujiunga uwanachama wa fifa kwa kutumia Tanzania ni makosa kisheria.
Lakini yote ayo kwa kupitia serekali ya SMZ utategemea nini? serekali ambayo ni balozi wa SMT zanzibar badala ya kua sarekali ya wananchi, huwezi kutegemea chochote kwao.
 
Kweli mswala ya michezo hayamo katika orodha ya mambo ya mungano,lakini hayo yanajulikana kwenye katiba ya ndani ya Tanzania sio nje ya Tanzania,Nje ya Tanzania Zanzibar ni sehemu ya Tanzania.

Ukweli wa mambo ni serikali ya Zanzibar inatakiwa iongee na wenzao wa Tanganyika kuhusu hili....waondoe siasa katika hili jambo la michezo kama walivyofanya waingereza...
 
Ni fact sio nawaombea hata viwango vya fifa kenya ni wa 84 je zanzibar ni wa ngapi?
Na Uganda ndo the first one kwa east afrika na zaid ni bingwa mtetezi wa hili kombe lakini wame poteza nafasi.
Ktk mpira lolote linaweza kutokezea regardless unacheza na nani
 
Kuna vijana wa kizanzibari hapa uk wanafika watatu tayari wapo katika club wanacheza game vizuri isitoshe wapo ambao wako katika mataarisho. Naamini siku za mbele zanzibar inaweza kuwa na timu ya uhakika zaidi
 
We jamaa huijui bendera ya znz? Ingia gugo utaikuta mkuu

800px-Flag_tz-sansibar_2005.png

Wewe Hivi Kwa akili Zako Hiyo ↑↑ inaitwa Bendera?
Umeona Wapi Bendera Kuwa Ndani Ya Bendera?
Huo Ni Uhuni tu Hapo Uliofanyika...

Hii Ndiyo iliyokuwa Bendera Halisi Ya Zanzibar baada ya Mapinduzi ya Mwaka 1964. ↓↓
..

FlagZanzMapinduzi1964.JPG

Lakini Bendera Hiyo Tanganyika wakishirikiana na CCM Wa Zanzibar Wameipiga Ban na Haitambuliki tena..

IMG_-hrqbk4.jpg

Hiyo ↑↑ Ndiyo Bendera Ya Kwanza Ya Wazanzibari Baada Ya Kupewa Uhuru Wao Kamili December 1963...
Ingawa Uhuru Huo ulidumu Mwezi mmoja tu na Kupinduliwa Mwaka 1964.
 
Na Uganda ndo the first one kwa east afrika na zaid ni bingwa mtetezi wa hili kombe lakini wame poteza nafasi.
Ktk mpira lolote linaweza kutokezea regardless unacheza na nani
Umenena kweli kabisa sasa kuna wengine hawataki coz zanzibar imecheza vizuri na imefika final basi moja kwa moja wanaipa ubingwa mpira hauko hivyo na ndio maana na mimi nikawa upande wakenya
 
Sasa sisi huku tumewatambua kwa vigezo gani

Hawajatambuliwa na Yoyote Wala Hakuna Kigenzo Cha Kisheria Kinachomfanya Zanzibar Ashiriki Mashindano Ya CECAFA.

CECAFA is an association of the football playing nations in East and Central Africa

Zanzibar sio Nation lakini Kwa Huruma tu za Kuombewa na Tanganyika Ndiyo Kagaiwa uanachama!
Lakini CECAFA haiitambui Zanzibar Kuwa Ni Nchi Na Ndiyo Maana Wanawapokea Wazanzibari Kupitia Passport za Tanzania na wala si Za Zanzibar.
 
Kwani Zanzibar wana Passport zao.....
 
Back
Top Bottom