Semeni yote kuhusu Lissu lakini kuna ambao kwao ni zaidi ya mtetezi

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,797
71,216
6cdf7048c43c85f0c87467728dd799bc.jpg


Niwaambie nini kuhusu Tundu Lissu?
Sina la kusema

Kwa ufupi

Nilifungwa jela miaka 30 na viboko 12! Nikiwa kada wa CCM na mjumbe wa mkutano Mkuu wa CCM. Kwa kusema neno moja tu watu tunaozunguka mgodi tuingie ubia na kampuni ya uwekezaji nikiwa mwenyekiti wa kijiji cha Kewanja,( CCM ) na mstaafu wa Jeshi la Wananchi
Amri ya Benjamin mkapa Rais ikaja kwamba huyo anayefundisha watu ashughulikiwe

Nikafungwa miaka 30! Familia yangu haikuwa na uwezo wa kuja Mahakami ila Tundu Lissu akajitolea akawa Wakili wangu bila kumpa cent hata moja. Akanitetea nikashinda kesi

LISSU KWANGU NI ZAIDI YA MTETEZI

AUGUSTINO NESTORY SASSI
KUTOKA NYAMONGO
Senior council 1984- 2010
Mwkt wa Kijiji. 1982-2001
Nimeona mengi namuomba MUNGU AMTETE LISSU

My take;
Kuna watu wamemwita Lissu msaliti na majina kedekede, lakini ona ushuhuda wa huyu Mzee kada wa ccm ulivyo. Alisaidiwa bila kujali yeye ni CCM lakini kama Mtanzania mnyonge. Lakini Kuna watu wanabomolewa Nyumba zao kwa vile tuu hawakuwapa kura.

Je mzalendo ni nani hapo?
Nadhani ni mpango wa Mungu Ku spare maisha ya Lissu ili 2020 aje awapiganie wananchi wote bila kujali haya mavyama
 
..na hicho ndicho kinachowapa shida CCM na kufikia chama kizima kumpiga vita Tundu Lissu.

..waTz wanajua kwamba mtetezi wa kweli wa rasilimali zao ni Tundu Lissu na wanaharakati wenzake, na siyo John Pombe Magufuli.

..ukweli huo unawapa shida kubwa CCM na ndiyo unaosababisha Tundu Lissu aandamwe na kupigwa vita.
 
Mungu amjalie Mh: Tundu Lissu afya njema, nguvu ya mwili na akili, na amzidishie hekima na busara daima siku zote, huku akimuimarisha katika usafi wa nafsi na roho daima. Amjalie maisha marefu pamoja na kumkamilisha katika afya ya utimamu wa mwili, arejee Tz kulikomboa Taifa hili mama linaloangamia chini ya mikono ya kakundi ka watu wachache, wajiitao wakombozi wa wanyonge, na kujivisha ngozi za kondoo, wakati wao binafsi ni WANYONGAJI, WAKOLONI NA MBWA MWITU WENYE NJAA KALI WALIJIDHATITI KUWANYONGA NA KUWALA HAO WANYONGE WAKIWA HAI. Eee Mungu wetu mwenye haki na upendo, rehema, na usiye na visasi kwa watu wako, tunusulu na janga la shetani huyu (VAZI MPYA LA MFALME). Amina.
 
Huyu ndiye kipenzi cha wanyonge, amesoma akaelemika.
Elimu yake ni lulu kwa taifa, kwa taaluma yake wanyonge wafurahia.

Waoga waliomuogopa, kwa kuwa hawakuwa na hoja walishindwa vibaya mbele ya hoja zake imara na zinazochoma mioyo. Walipumbazika kutumia risasi wakidhani kimya kizito na giza nene kingetawala, Mungu si athumani, kwa mkono wake alitenda, giza limefunikwa na nuru, nuru yaangaza, na imeleta uzima na ushindi tele.

Twakushukuru Mwenyenzi Mungu kumlinda Lisu, Mjaze afya tele, mpe nguvu tele, umbariki kwa maarifa na hekima tele.
 
Hatukosei kabisa Mkuu tunaposema Lissu the Great ni hazina kubwa ya Taifa. Mwenyezi Mungu kasikia sala zetu (Wakristo, Waislamu na wale wa dini nyingine) kuhusu mwenzetu mtetezi wa maslahi ya Taifa na wanyonge nchini tulipomuombea kumuomba amponye pamoja na risasi 38 kuingia mwilini mwake. Mwenyezi Mungu ni mkubwa na leo hii ametupa matumaini makubwa kuhusu afya ya Lissu the Great ukilinganisha na siku ile aliyoshambuliwa ambapo wengi tulikuwa na hofu kubwa kama ataweza kumaliza hata masaa 24 akiwa hai. Tuombe.

 
Tundu Lissu is a true hero, achana Na Yule Msukuma mshamba Fid Q anayejidai ni mtetezi wa masikini Na wanyonge wakati ndiye anayefanya maisha yao yawe magumu Kila kukicha
Umegonga mulemule Bujibuji.
Mshamba na mlimbukeni huyu lingosha. "Et
Tundu Lissu is a true hero, achana Na Yule Msukuma mshamba Fid Q anayejidai ni mtetezi wa masikini Na wanyonge wakati ndiye anayefanya maisha yao yawe magumu Kila kukicha
Umegonga mulemule Bujibuji. Mungu amlinde Tundu Lissu na mabaya yote na kila atakayejaribu kumdhuru adhurike yeye.
Nchi inaendeshwa na washamba na malimbukeni. "Eti wa Dar anawabomolesha na wa Mwz wasibomoleshwe". Huyu ndo mzalendo. Kulaleek...aache umazwazwa.
 
ccm tunatamani sana lissu aje huku.huyu mtu Ni tishio
Na ninakuhakikishia kwa ccm hii ya sasa isiyojali RAIA, yenye uonevu na dhuluma pia wasema uongo Lissu hata mumuahidi kumpatia hazina yote ya nchi hawezi hats siku moja kukubali kujiunga nanyi.
Wanaomjua watakubaliana na hili.
 
Back
Top Bottom