Sema chochote kuhusu Ben Carson

Michael Chairman

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
922
581
Nafurahishwa na wale wanaotumia uwezo wao wote kufanikisha jambo wanalotaka
huyu naye ni miongoni mwao kati ya wale wanaotumia uwezo wao wote kufanikisha jambo wanalotaka anaitwa Ben Carson , aliyekuwa mgombea wa urais kwenye chama cha Repulican aliyeonesha ushindani mkubwa na ukosoaji wa nguvu wa sera za mgombea wa urais Donald Trump ambaye sasa ni Rais mteule wa marekani lakini mwishoni akashindwa na kuamua kumuunga mkono Donald Trump na sasa anayo matumaini makubwa kuwepo kwenye serikali ya Donald Trump.
kupitia ukurasa huu sema chochote kuhusu Ben carson na usisahau kuwa yeye ndiye mwandishi wa vitabu pendwa vya "mikono itendayo maajabu " na cha sasa kijulikanacho kama "Lenga juu"
 
Nasema chochote:

Daktari Benjamin S. Carson (amezaliwa tar. 18 Septemba 1951) ni daktari na mtaalamu wa Nyurolojia, na pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Nyurolojia kwa watoto katika hospitali ya Johns Hopkins huko nchini Marekani. Alitunukiwa na raisi medali ya uhuru mwaka 2008

Historia ya elimu
Benjamin Solomon Carso alizaliwa katika eneo la Detroit katika jimbo la Michigan. Mama yake, Sonya Carson, aliacha shule akiwa katika daraja la tatu na kuolewa na Robert Solomon Carson, aliyekuwa mchungaji mzee zaidi katika eneo la Tennesee, wakati mama yake Ben akiwa na umri wa miaka kumi na tatu tu. Wakati Carson akiwa na umri wa miaka nane tu, wazazi wake waliachana. Mama Carson aliachwa kuwalea Benjamin na kaka yake Curtis, yeye mwenyewe. Alifanya kazi katika sehemu mbaili au hata tatu kwa mara moja ili aweze kuwatosheleza watoto wake wawili. .[1] Mwanzoni Carson alikuwa na maisha magumu shuleni. ,[2] hali iliyopelekea kuwa wa mwisho mara kadhaa katika darasa lake. Alikuwa akiitwa majina mbalimbali kutokana na hali hiyo, hivyo ikapelekea kukua kwa hasira kali ndani yake. Akiwa amedhanmiria kubadilisha maisha ya mtoto wake, mama yake Carson akazuia muda wake wa kuangalia runinga na kumzuia kutoka nje kila siku hadi pale atakapokuwa amemaliza kazi zake za shule kila siku. Mama yake Carson alimtaka Kusoma vitabu viwili kutoka maktaba na kuandika taarifa juu ya vibu hivyo kila wiki, bila kujali elimu yake ndogo, hata hivyo hakuweza kusoma vitu ambavyo vilikuwa vmeandikwa. Lakini mapema, Carson alimshangaza mwalimu wake na wanafunzi wenzake kufuatana na maendeleo yake. Anakumbuka “Ni wakati ule ndipo nilipogundua kuwa sikuwa mpumbavu” anagundua baadae. Carson anaendelea kuwashangaza wanafunzi wenzake na ndani ya mwaka mmoja alikuwa na ujuzi na kuwa katika nafasi ya juu katika darasa lake.[1]

Baada ya kugundua kuwa alitaka kuwa daktari wa magonjwa ya akili, Carson alimaliza shule na matokeo mazuri yenye heshima na hivyo alijunga na chuo kikuu cha Yale ambapo alipata shahada yake ya kwanza katika maswala ya saikolojia ya akili. Pschology. Baada ya kutoka Yale, aliendelea na shule ya udaktari ya michigan, ambapo hapo ndipo nia yakeya kuwa daktari wa magonjwa ya akili ilipobadilika na na kuwa daktari wa mishipa. Uwezo wake mkubwa wa kuona na uwezo wake wa kufikiri haraka ulimemfanya awe daktari wa upasuaji mzuri zaidi Baada ya kumaliza shule yake ya udaktari, alikuwa daktari wa mishipa msaidizi katika hospitali ya Johns Hopkins katika jimbo la Baltimore. Akiwa na umri wa miaka 33, alikuwa profesa wa hospitali na pia mkurugenzi wa idara ya upasuaji mishipa ya watoto

Kazi zake za mapema
Mwezi wa tisa mwaka 1987, Carson alifanya upasuaji wa kutenganisha mapacha wenye umri wa miezi saba, waliokuwa wameungana katika sehemu ya kichwa. Carson alikuwa ndiye kiongozi wa upasuaji huo mgumu, Mwaka 1997, Carson pamoja na timu yake, walienda Afrika ya Kusini, kuwatenganisha Lukas na Joseph Banda kutoka Zambia. Watoto wote wawili waliweza kuishi baada ya upasuaji na hakuna hata mmoja wao aliyepata uharibifu wa ubongo. Watoto hao wa Banda walikuwa ni watoto wa kwanza walioungana kwa upande wa juu wa vichwa vyao kuweza kuishi baada ya upasuaji. Upasuaji huo ulifanyika kwa saa 28. Mwaka 2003, Carson alikuwa moja kati ya madaktari waliofanya upasuaji wa watu wazima waliokuwa wameungana katika sehemu ya vichwa, Ladan na Laleh Bijan. Lakini wote hawakuweza kuishi baada ya upasuaji. Alipoulizwa kwa nini alikubali kufanya upasuaji wa kubahatisha kiasi hicho alisema, ndugu hao walikwa wamekubali bora wafe kuliko kuendelea kuishi wakiwa wameungana.

Maisha binafsi
Carson amepokea tuzo mbalimbali katika miaka mbalimbali, kama vile, Shahada za heshima za Udaktari 40, pia ni mwanachama katika chama cha American Academy of Achievement, Horatio Alger Association of Distinguished Americans, Alpha Omega Alpha Honor Medical Society Ushirikiano wa yele, (Bodi ya wakurugenzi wa Chuo kikuu cha Yale) na mashirika mengine mengi. Pia ni mwanzilishi na mkurugenzi wa The Carson Scholar Fund, ambayo huwasaidia wanafunzi kutoka katika historia tofauti tofauti walio na vipaji maalumu katika masomo. Mwaka 2007, Carson alijumuishwa katika Chuo kikuu cha Indiana Wesley, katika Society of World Changes na kupokea nishani ya heshima ya udaktari alipokuwa akiongea katika Chuo hicho. Aliporudi, alirudi na rafiki yake alyeitwa Tony Dungy ambaye naye alikumuishwa katika jamii. Tarehe 19 mwezi wa 9 mwaka 2008, Carson alopokea nishani ya raisi ya uhuru kutoka kwa Raisi George W. Bush

Utaalamu na magonjwa
Carson ameandika vitabu vitatu vilivoongoza katika mauzo na vilivyochapishwa na Zondervan shirika la kimataifa la uchapaji la kikristo, Vinavoitwa : Gifted Hands (Mikono Yenye Vipawa: Hadithi Ya Ben Carson) , The Big Picture, na Think BigKitabu cha kwanza cha Historia ya maisha ya mtu, na vitabu vingine viwili ni kuhusu filosofia ya maisha yake hususani katika mafanikia yake yanayoenda sambamba na imani yake kwa Mungu.Carson ni Mkristu katika dhehebu la sabato.

Mwaka 2002, Carson aliamuriwa kusitisha kuonekana katika maeneo yenye imati wa watu, baada ya kupata matatizo ya kiafya ya kwake mwenyewe. Mwezi wa sita alikutwa na dalili za kuwa na Saratani ya Kibofu cha mkojo, lakini kwa bahati nzuri, saratani hiyo ikiliweza kukutwa katikamuda muafaka. Lakini pamoja na hayo, Carson alibadilisha mfumo wake wa maisha, Bado anafanya upasuaji kwa zaidi ya watoto mia tatu (300) kwa mwaka lakini amekuwa akijaribu kupunguza muda wake.Carson amekuwa akifanya kazi kuanzia saa 7:00 asubuhi na kumaliza saa 8:00 usiku, lakini tangu agundulike kuwa na saratani amekuwa akifanya kazi na kuondoka saa 6:15, jioni. Hii inampa muda zaidi wa kukaa na mke na watoto wake watatu (3)

Makala ya video kuhusu maisha ya Carson inyoitwa Gifted Hands:Kitabu kinachohusu, hadithi ya Ben Carson kilitolewa na Zondervan mwaka 1992, hali iliyopelekea mwaka 2009, filamu ya Televishen iilitolewa ikiwa na Jina hilo hilo, katika TNT tarehe 07/02/2009, na kushinda tuzo ya Academi ya Gooding jr ikiongozwa na Kimberly Elise akimwelezea mama yake.
 
Ben Carson hakumkosoa trump, bli alikuwa mmoja kati ya republican wachache kumsuport tka alivyoidhinishwa na chama. ukososji wake ulikuwa wakt wa kampen ndn ya chama.
 
Ina maana alivyoomuunga mkono alikuwa hajielewi?..unaufahamu msimammo wake sasa hivi?
Kha,kasema hawezi kuingia serikalini kwa kuwa anataka kuwa na mawazo huru,hataki kuwa na ideas za kupelekeshwa pelekeshwa.
 
Kha,kasema hawezi kuingia serikalini kwa kuwa anataka kuwa na mawazo huru,hataki kuwa na ideas za kupelekeshwa pelekeshwa.
Hivi umefuatilia latest news yake pamoja na kudai hivyo?
 
What I can say about this handsome Ben C. is......
1. I love him pure love
2. He is strong (in many ways)
3. With the hand of his mother, he prove many that they were wrong and he was capable.
4. He courage others not to give up, just put an effort.
5. I will always love him (Kasie is born to love).
6. Wherever I see Ben C. I remember my once friend Tized
 
Namfagilia Ben Carson...napenda sana kitabu chake cha THINK BIG ambacho ni muongozo kwa wanafunzi hasa watokao ktk familia za kimasikini.
 
Back
Top Bottom