Selfika na JF: Snap it. Show it

Hivi wasukuma na ugali ni mapacha nini

Kwa sasa maembe tu, tunashushia na maji tukisubiri dinner
Bila ugali kwa kweli mambo hayaendi. Si ajabu hata hiyo dinner ikawa ni ubwabwa tu. Endeleeni tu bageshi
Screenshot_20211207-103246_Instagram.jpg
 
Sema nakukubali huwa una busara sana. Sijawahi ona mahali unatukana mtu humu hata akikukwaza vipi huwa unajitahidi kumjibu kistaarabu tu.

Kwa comment yake hiyo nina uhakika angelikuwa ni mtu mwingine asingeweza kuvumilia angelipuka kwa matusi na mjadala ndiyo ungekuwa mkubwa zaidi.

Binafsi huwa najifunza sana kuwa na that type of attitude na nikifanikiwa hilo naamini nitakuwa mtu mwingine kabisa. I hope hii ndiyo attitude uko nayo hata in real life.
Oooh! Thanks mai furendi...

Na uzee wote huu kuanza tena kutukanana na wajukuu humu dah! Wengine huchukulia kama ni udhaifu hata huku mtaani lakini kuna faida nyingi sana kisaikolojia kuwa calm. Hupati mahomoni haya ya stress hovyo hovyo na roho yako inabakia kuwa nyeupe.

Isitoshe niko mahali yaani social life imeharibiwa sana na Korona. Kwa hivyo JF hapa ndiyo kijiwe changu cha kahawa kuja kutaniana na kucheka. Sasa niache tena kucheka na kufurahi niingie kwenye kutukanana? Hapana. Ndo maana nilikimbia hata jukwaa la siasa japo mara moja moja nikitamani kuyakoga matusi naendaga huko kuchokoza watu tu .

Yeah! It costs us nothing to treat everyone with respect hata kama hatujuani. Actually that's a reflection and a true measure of a man's integrity and self awareness. Kuna mambo mengi ambayo, kama binadamu, hatuwezi kuya-control. Nguvu zetu, hata hivyo, zimo katika namna tunavyo-respond.

Asante sana Karma
 
Back
Top Bottom