Selfika na JF: Snap it. Show it

Kila tokeo la kimwili bila kujali kama ni chanya ama hasi asili yake ni roho ama rohoni... Hakuna kitu kisicho asili na roho ama nguvu isiyoonekana.... Hata huyu Mungu mkuu anayebishaniwa kila siku uwepo wake ni kinyume cha miungu ile ya kuchonga ile inayoonekana kwa macho..... Hata haya macho na masikio na sauti zetu... Kuna macho na masikio ya kuonekana, kuna sauti za kusikika na kuna macho masikio na sauti vya rohoni.... Havionekani havisikiki lakini vipo na ndio asili na chanzo cha ulimwengu unaoonekana

Maslahi ya kiroho ninini? Ni yapi?
Maslahi ya kiroho ni ukamilifu wa jambo lolote baya ama zuri kwenye ulimwengu wa nyama, ulimwengu unaoonekana kwa macho ya kawaida
Kutokamilika kwa jambo husika, maslahi ya kiroho huwa shakani na katika mtanziko mkubwa kutokana na kushindwa kufanya ukamilifu... Hapa sasa chanzo na sababu za kushindwa hutafutwa!!!!
Kila kitu, kila jambo huanza na wazo, wazo halionekani, halishikiki halisikiki.. Hiki linaishi rohoni.. Ndio penye chanzo chake... Wazo huzaliwa na kupangwa kati ya mtu na mwenyewe ndani ya nafsi zake tatu kabla ya kushirikisha nafsi ya nje, nafsi ya nne...
Wazo hata bila kupangwa ndani ya mwenyewe linaweza kuwasilishwa nje ya nafsi kwa njia ya sauti, michoro, maandishi na hata vitendo.... Baraza la nafsi lenye wajumbe nafsi tatu ndio huamua aina ya uwakilishi husika
Baraza nafsi tatu ndani ya nafsi ni lipi?
Nafsi ya kwanza ni nafsi roho... Mwenyekiti
Nafsi ya pili ni nafsi ufahamu... Katibu
Nafsi ya tatu ni nafsi wajumbe/hadhira... Muunganiko wa nafsi roho na nafsi ufahamu vinavyozaa utambulisho....
Asili ya wazo hutoka kwa wote katika muunganiko wa umoja, nafsi ufahamu akiwa ndio mzizi...
Hapa wazo hufanyiwa kazi na kukubaliwa na baraza la nafsi kwa sauti moja.... Kama kukiwa kuna kusitasita basi tambua kwenye kikao cha baraza la nafsi kuna mmoja hajakubaliana na wazo... Na shida itaanzia hapa kama kutakuwa na kufeli baada ya matokeo ya kimwili kuwa tasa au kuharibika....
Unapopanga jambo lakini ukawa kila wakati uko kwenye mtanziko wa kulifanya ama kutolifanya tambua baraza lako la ufahamu halijakubaliana kwa sauti moja....
Maslahi ya kiroho daima huzingatia na hudai mrejesho kwa kila tendo lililokamilika kwenye matokeo ya kimwili
Kama matokeo ni chanya baraza hushangilia na kupata faraja.... Lakini kama matokeo ni hasi basi lazima kitafutwe chanzo ama sababu yake....
Hapa kuna sababu nje ya baraza... Hizi si muhimu sana na maslahi ya kiroho huwa hayazingatiii sana.. Sababu ya kushindwa kama inatokana na maamuzi ndani ya baraza la nafsi, ama maamuzi yaliyokuwa yanakinzana ama kupishana hapa hali huwa mbaya na maslahi ya kiroho ndani ya mamlaka ya baraza la nafsi huamua kujiadhibu....
Ni adhabu gani hizo basi....
Majuto yenye kukosesha furaha na amani
Vilio mfululizo
Mawazo mpaka kuugua ama kushindwa kula nk
Kujidhuru mwili kwa vileo, madawa nk
Hisia za kutaka kulisambaratisha baraza na mamlaka yake kwa kuamua kujitoa uhai..
Nknk

Tuna tabia ya kuwacheka wengine wanaopitia hizi hali bila kutambua kuwa sio wao bali ni matokeo ya kushindwa kimwili yale yote yaliyopangwa na maslahi ya kiroho kupitia baraza la nafsi.....

Nimeeleweka?

Jr
 
Music time
20210618_222703.jpg
 
Ooooops Happy belated birthday to you swts. It shall always be well with you mdogo angu.

Psalm 20:4
May He grant you your heart’s desire and fulfill all your plans!

James 1:12
Blessed is the man who remains steadfast under trial, for when he has stood the test he will receive the crown of life, which God has promised to those who love him.

Numbers 6:24-26
The Lord bless you and keep you; the Lord make his face to shine upon you and be gracious to you; the Lord lift up his countenance upon you and give you peace.
 
Ooooops Happy belated birthday to you swts. It shall always be well with you mdogo angu.

Psalm 20:4
May He grant you your heart’s desire and fulfill all your plans!

James 1:12
Blessed is the man who remains steadfast under trial, for when he has stood the test he will receive the crown of life, which God has promised to those who love him.

Numbers 6:24-26
The Lord bless you and keep you; the Lord make his face to shine upon you and be gracious to you; the Lord lift up his countenance upon you and give you peace.
Amen Amen
Asante sana dada

Thanks for the verses
 
Back
Top Bottom