Selemani Zedi: CCM haijawahi kupata Rais anayetekeleza ilani kwa kasi kama Rais Samia

UGANDA

Member
Jul 24, 2017
59
125
"Jimbo la Bukene Kwenye Barabara tumepokea Zaidi ya Bilioni Moja na Milioni 500 ni ongezeko kubwa la Fedha halijawahi kutokea imeonyesha kabisa Rais huyu wa sasa Samia Suluhu Hassan ana dhamira ya dhati ya Kuboresha miundombinu yetu". Mbunge wa Jimbo la Bukene Seleman Zedi.

"Rais Samia amedhamiria kufuta kilio chetu cha ukosefu wa huduma za maji kabisa hapa Bukene ametuletea Fedha bilioni 2 ili kuyatoa Maji Pale Nzega zaidi ya Kilometa 40 hadi hapa, mradi huo utanufaisha vijiji zaidi ya 20 na vitongoji 100"
Mbunge wa Jimbo la Bukene Seleman Zedi

"Mwezi wa Novemba huu Miaka yote iliyopita tulikuwa tunakimbizana watoto wamefaulu tunachangishana mara kukamatana kupata Madarasa, lakini kwa mara ya kwanza Rais Samia ametupatia fedha kujenga Madarasa bila wananchi kutoa michango tunamshukuru sana" Mbunge Bukene Seleman Zedi

"Jimbo la Bukene Miaka iliyopita tulikuwa tunajitahidi kwenye Bajeti tunajenga madarasa 2 au 3 lakini mwaka huu Rais Samia ametupatia Madarasa 42 ya Sekondari zaidi ya Milioni 840 haijawahi kutokea! Ametupatia pia Milioni 220 kujenga Madarasa 11 kwenye Shule Shikizi"MBUNGE ZEDI

"Kasi ya Usambazaji wa umeme ni kubwa Jimboni Bukene Tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie Madarakani, mwezi wa saba tumepata Mkandarasi mpya mradi wa REA Awamu ya Tatu na kafikisha Nguzo vijiji kumi tayari, Pia Rais ametupa milioni 250 kuimarisha kituo cha Afya Itobo"MBUNGE ZEDI

"Rais Samia Suluhu Hassan ametupatia fedha milioni 600 kujenga Shule mpya ya kisasa ya Sekondari, Rais Samia anafanya makubwa hatujawahi kupata Mwenyekiti wa CCM anatekeleza Ilani ya Uchaguzi na miradi ya maendeleo kwa kasi kubwa kama Rais Samia"
Selemani Zedi

Mbunge wa Jimbo la Bukene Seleman Zedi ameyasema hayo leo Kwenye Ziara ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Shaka Hamdu Shaka ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM na uhai wa Chama Mashinani Jimboni Bukene, Wilayani Nzenga Mkoani Tabora.

IMG_20211123_144738_747.jpg
IMG_20211123_144738_674.jpg
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
53,563
2,000
MaCCM wote Akili zao hazina akili.
Magufuli alisema bila yeye na ukichaa wake, nchi haiwezi kwenda .
MaCCM yote yakainama na kumsujudia.
Leo yanakula matapishi. Bladefeken.
Kuna watu waajabu sn huko ndani
 
Dec 30, 2018
84
150
Mweee mweeee, ebu nyamazeni tupumue jamani khaaaaa😂😂😂😂, watu tunastress alafu jitu linakuja eti fulani anatekeleza ilani kwa kasi duuu.
 

Naipendatz

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
4,643
2,000
China pamoja na ucommunist wao rais wao anapingwa kwamengi na imepelekea kufikia pale..ccm hovyo kabisa
Unazungumzia China Ipi? Labda anapingwa na watu waliopo nje ya China, ila as long as upo ndani ya China ni kuufyata!! Unajua wanachomfanya tajiri wao namba moja kwa sasa?

Kosa lake kubwa ni kutoa maoni yanayopingana na Xi kuhusu sera zake mpya za uchumi anazozitekeleza China kwa sasa!! Hakuna mtu anainua mdomo kumkosoa Xi ndani ya China na akabaki salama
 

Peramiho yetu

JF-Expert Member
May 25, 2018
3,276
2,000
Msiwalaumu Sana hii n sababu ya nguvu ya mwenyekiti katika chama

Demokrasia ndan ya CCM n finyu Sana ukihoji au kwenda tofauti kutoboa kwenye CC ya Chama n ndoto

Hapo ndipo hata profesa anakuwa mpuuz fulan sababu ya Hilo

Kitila

Mwakyembe

Kabudi

Hawa wote n wasomi lakn ndan ya Chama KIBAJAJI na MSUKUMA ndio THINK TANK wa chama

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 

kiangola

Member
Apr 9, 2021
64
150
China pamoja na ucommunist wao rais wao anapingwa kwamengi na imepelekea kufikia pale..ccm hovyo kabisa

Kwa China hapana mkuu,hii system ya kutukuza Viongozi wakuu CCM wameicopy China.Na ilishika hatamu kipindi cha Hayati JPM,naona imeshawakolea watu.

Siku hizi mtu akipata nafasi hata ya kusikika Redioni au kuonekana kwenye Runinga basi lazima utasikia Pongezi kwa Mheshimiwa Raisi!
Hiyo ya kutaja Rais katoa Tsh kadhaa ni aina za mbinu katika kutengeza foothold ya kisiasa kwa muhusika!.

Ndio maana ya Propaganda.
 

Nipo huru

JF-Expert Member
Jul 20, 2021
1,316
2,000
Wafuasi wa jiwe wanakereka sana wakisikia Rais Samia akisifiwa wao wanataka watu waendelee kumsifu jiwe tu.
 

kina kirefu

JF-Expert Member
Dec 14, 2018
4,635
2,000
Kwa China hapana mkuu,hii system ya kutukuza Viongozi wakuu CCM wameicopy China.Na ilishika hatamu kipindi cha Hayati JPM,naona imeshawakolea watu.
Siku hizi mtu akipata nafasi hata ya kusikika Redioni au kuonekana kwenye Runinga basi lazima utasikia Pongezi kwa Mheshimiwa Raisi!
Hiyo ya kutaja Rais katoa Tsh kadhaa ni aina za mbinu katika kutengeza foothold ya kisiasa kwa muhusika!..
Ndio maana ya Propaganda.
Soma gazeti la chama communist party Tz Kama Uhuru hivi ,uone wanaisahisha serikali sio kusifia tuuuuuuuuu hatuwezi fika kokote nitakupa uongee na mwandishi habari wagazeti husika
 

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,055
2,000
"Jimbo la Bukene Kwenye Barabara tumepokea Zaidi ya Bilioni Moja na Milioni 500 ni ongezeko kubwa la Fedha halijawahi kutokea imeonyesha kabisa Rais huyu wa sasa Samia Suluhu Hassan ana dhamira ya dhati ya Kuboresha miundombinu yetu"...
Wapashe hao misukule ya mwendazake na Chadomo gang..

Mbunge yeyote wa ccm atayeanguka 2025 itakuwa ni upuuzi wake, ukweli ni kwamba mapesa mengi yamemwagwa kwenye Halmashauri hadi raha na ni kweli haijawahi tokea.

Kama yupo Rais amewahi toa pesa nyingi huko Halmashauri kushinda mama mtakeni na miweke figures hapa.

Kilio Cha barabara Vijijini kimemalizwa na Samia fasta👇

Screenshot_20211121-132004.png


Screenshot_20211121-132128.png
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom