Uchaguzi 2020 Selemani Bungala (Bwege) asema Magufuli hakushinda kihalali. Atolea mfano wa aliyoshuhudia katika vituo viwili jimboni kwake

Aliyekuwa mbunge wa Kilwa kusini ndugu Selemani Bungala (Bwege) , amesema kuwa licha ya yeye kukosa Ubunge lakini Uchaguzi uliokuwa na matatizo zaidi ni wa Urais.

Amesema ameshuhudia yeye mwenyewe kwa macho yake katika vituo kadhaa katika jimbo lake ambapo kura halisi alizopata Magufuli zikibadirishwa na kuwekwa figure ambayo siyo halisi.

Amesema aliona kwa macho yake katika kituo kimoja Magufuli akipata kura 70 na Tundu Lissu kura 67 lakini za Magufuli ziliongezwa na kuwa nyingi zaidi ya hizo.
Na kwenye kituo kingine akasema Magufuli aliongezewa kura 150 ambazo siyo halali yake!

Selemani Bungala(Bwege) ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na kituo cha TV cha Kenya.

Kwa habari zaidi, msikilize ndugu Bwege hapa akihojiwa.

Yaani ameona kwa macho yake...!! Kwa hiyo akawaacha waendelee kubadili, na hao jamaa wala hawakumuogopa Bwege, kweli huyu ni Bwege
 
Sidhani kama unajua ulichoandika na ukweli ktk 'box la kura' ulivyokuwa! Ila watu kama nyie mpo wengi wenye akili fupi.
Kama mna ushahidi wa kura kuibiwa au matokeo kuchakachuliwa pelekeni mahakamani ni za humu nchini au za kikanda.Ha ha haa mpigwa Hai na nje ya Hai,Mmepigwa pemba na nje ya pemba haha haaa wananchi wamewatupa mkono

Hata mkiungana matusi kututukana wanachi tumeamua tayari
 
Tunawataka Mawakala wa CHADEMA walioshuhudia watupe hizo Nakala, tuchukue kama sample tuone kama Lissu alishinda mbona tunaandikia mate na wino upo, mfano wa Bwege unaonyesha still JPM aliwin 70/67 .....zingine ni bla bla
Wakikupa hizo nakala naacha kuchangia humu. Na nitafurahi kama na Wakala wa Chadema aliyekuwepo kwenye kituo nilichokuwa Msimamizi Mkuu nae ataleta Nakala niliyompa na kueleza "wizi" uliofanyika. Na akifanya hivyo, NAACHA KAZI NA KUWA MWANACHADEMA!!!
 
Wewe unatoka sayari gani? 90% ya mawakala hawakuruhusiwa kushudia zoezi la kura kupigwa wala kuhesabiwa.Nawalioruhusiwa wengi waliondolewa kabla ya zoezi kwisha lastly hakunamahali waitoa nakala za matokeo zikiwana signature za wasimamizi.
Unaongea nn we jamaa , hapa nilipo vituo Saba vilikuwepo na mawakala wa Chadema walikuwepo , walishuhudia show nzima mpak mwisho , na nakala wakachukua, matokeo yalikuwa ni disaster Kwa Lissu kituo ambacho aliscore kura nyingi ni kura 43 dhidi ya 78 za JPM ....
Tatizo inafkia hatua za kuombeana laana Kwa Mungu , na mnataka kutuaminisha kuwa Lissu alishinda ila akaibiwa kura kitu ambacho sio kweli.... Ameshindwa kiuhalali kabisa , labda chuki zake tuu ndo zinamfanya aende ughaibuni kuomba nchi iwekewe vikwazo.... Nilikuwa na waswas na matokeo ya mbowe kumbe na yeye wananchi wamemtupa kiuhali kabisa , lakn utashangaa watu wanataka kutuaminisha ujinga na chuki zisizokuwa na sababu.....
 
Mmmh..
Aliyekuwa mbunge wa Kilwa kusini ndugu Selemani Bungala (Bwege) , amesema kuwa licha ya yeye kukosa Ubunge lakini Uchaguzi uliokuwa na matatizo zaidi ni wa Urais.

Amesema ameshuhudia yeye mwenyewe kwa macho yake katika vituo kadhaa katika jimbo lake ambapo kura halisi alizopata Magufuli zikibadirishwa na kuwekwa figure ambayo siyo halisi.

Amesema aliona kwa macho yake katika kituo kimoja Magufuli akipata kura 70 na Tundu Lissu kura 67 lakini za Magufuli ziliongezwa na kuwa nyingi zaidi ya hizo.
Na kwenye kituo kingine akasema Magufuli aliongezewa kura 150 ambazo siyo halali yake!

Selemani Bungala(Bwege) ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na kituo cha TV cha Kenya.

Kwa habari zaidi, msikilize ndugu Bwege hapa akihojiwa.

Tunawataka Mawakala wa CHADEMA walioshuhudia watupe hizo Nakala, tuchukue kama sample tuone kama Lissu alishinda mbona tunaandikia mate na wino upo, mfano wa Bwege unaonyesha still JPM aliwin 70/67 .....zingine ni bla bla
Kwani nakala zilitolewa?
 
ᴹᵃᵗᵒᵏᵉᵒ ʸᵃ ʷⁱᶻⁱ ⁿᵃ ᵘᵖᵒʳᵃʲⁱ ʷᵃ ᵈᵉᵐᵒᵏʳᵃˢⁱᵃ ᵏᵃᵗⁱᵏᵃ ᶜʰᵃᵍᵘᶻⁱ ᶻᵉᵗᵘ ⁿᵃ ʰᵃˢᵃ ʰᵘᵘ ʷᵃ ᴿᵃⁱˢ ⁿᵃ ʷᵃᵇᵘⁿᵍᵉ²⁰²⁰ ᵘᵗᵃᵏᵘʲᵃ ᵏᵘᵒⁿᵉˢʰᵃ ᵐᵃᵗᵒᵏᵉᵒ ʸᵃ ᵏᵘᵗⁱˢʰᵃ ˢᵃⁿᵃ ᵏᵃᵗⁱᵏᵃ ᵐⁱᵃᵏᵃ ʰⁱⁱ ᵐⁱᵗᵃⁿᵒ.
 
Back
Top Bottom