Uchaguzi 2020 Selemani Bungala (Bwege) asema Magufuli hakushinda kihalali. Atolea mfano wa aliyoshuhudia katika vituo viwili jimboni kwake

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,495
51,089
Aliyekuwa mbunge wa Kilwa kusini ndugu Selemani Bungala (Bwege) , amesema kuwa licha ya yeye kukosa Ubunge lakini Uchaguzi uliokuwa na matatizo zaidi ni wa Urais.

Amesema ameshuhudia yeye mwenyewe kwa macho yake katika vituo kadhaa katika jimbo lake ambapo kura halisi alizopata Magufuli zikibadirishwa na kuwekwa figure ambayo siyo halisi.

Amesema aliona kwa macho yake katika kituo kimoja Magufuli akipata kura 70 na Tundu Lissu kura 67 lakini za Magufuli ziliongezwa na kuwa nyingi zaidi ya hizo.
Na kwenye kituo kingine akasema Magufuli aliongezewa kura 150 ambazo siyo halali yake!

Selemani Bungala(Bwege) ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na kituo cha TV cha Kenya.

Kwa habari zaidi, msikilize ndugu Bwege hapa akihojiwa.

"Nyie watu wa Rufiji mna matatizo badala mchague Mbunge unachagua Bwege ,Bwege atawasaidia nini badala ya kuleta ubwege maana naona hapa hakuna alichofanya hata kujenga choo tu cha stand kwa pesa za jimbo ameshindwa "by JPM
 
Tunawataka mawakala wa Chadema walioshuhudia watupe hzo nakala, tuchukue kama sample tuone kama Lissu alishinda mbna tunaandikia mate na wino upo , mfano wa bwege unaonyesha still JPM aliwin 70/67 .....zingine ni bla bla
Hicho unachosema siyo hoja! , kwa sababu zilizoongezwa zimempa Magufuli overall advantage kwenye kura zote za majumuisho nchi nzima.
 
JPM anajua kabisa anaongoza watu ambao walimkataa!Halafu anajichekesha kinafiki,shame!
Bila Uchaguzi kuhujumiwa walikuwa wanapigwa pande zote za Muungano
Na Wapinzani wangechukua viti vingi vya Ubunge licha ya enguaengua ya akina Mahera ili kuipa advantage CCM.

Huwa ninakaa na kutafakari sana eti Hussein Mwinyi apate 76% na Maalim Seif apate 19%. Huu ni unyang'anyi usio na aibu!

Kama wameyafanya Zanzibar basi hawana sababu ya kutoyafanya Bara, maana ndiyo walewale!
 
Tunawataka mawakala wa Chadema walioshuhudia watupe hzo nakala, tuchukue kama sample tuone kama Lissu alishinda mbna tunaandikia mate na wino upo , mfano wa bwege unaonyesha still JPM aliwin 70/67 .....zingine ni bla bla

Hakuna mwenye tatizo na kushindwa, bali unashindwaje hapo ndio issue. Nimesema tena na tena kuwa wapiga kura kwenye uchaguzi huu hawakufika 10m, na katika hao Magufuli hajafikisha kura 5m, hata kama yeye ndio alikuwa mshindi. Hizo kura milioni 12+ ilikuwa ni kuhadaa umma ili kuficha aibu.
 
"Nyie watu wa Rufiji mna matatizo badala mchague Mbunge unachagua Bwege ,Bwege atawasaidia nini badala ya kuleta ubwege maana naona hapa hakuna alichofanya hata kujenga choo tu cha stand kwa pesa za jimbo ameshindwa "by JPM

Lugha za kitoto.
 
Hiyo siyo hoja, zilizoongezwa zimempa Magufuli overall advantage kwenye kura zote za majumuisho nchi nzima
Sio hoja kivip wewee, mnadai mawakala walifukuzwa , haya waliofanikiwa kushuhudia matokeo kwenye vituo hata kama wapo kumi , watupe nakala tujumlishe tuone kama Lissu alishinda na hyo ndo iwe sample ya matokeo yote , na hapo tutaamin kwel Lissu alishinda kura zikachakachuliwa ...sasa kuongea ongea Tu mara ooh niliona kwenye vituo vingi , mara oooh kimoja JPM 70 Kwa 67 , mara mabegi ya kura sjui , njia sahihi mawakala walikodoa from begining to the end na wakapewa nakala , watupe hayo tuoneee....

Mawakala wapo kimya na ndo Wana data nzuri, Kati ya watu waliosimamia uchaguz most ni walimu , watu ambao wanamhate Sana JPM but na wao wapo kimya cse wanajua JPM kashinda kiuhalali kabisa , ......
Nilikuwa na was was na matokeo ya ubunge wa mbowe , nimeongea na majamaa wa Hai wanadai jamaa kapigwa kiuhalali kabisa .....

Angalieni hzi laana mnazoliombea Taifa zitawarudia , mana mnajua mmeshindwa ila Kwa ukaidi mnatengeneza maneno ...
 
Aliyekuwa mbunge wa Kilwa kusini ndugu Selemani Bungala (Bwege) , amesema kuwa licha ya yeye kukosa Ubunge lakini Uchaguzi uliokuwa na matatizo zaidi ni wa Urais.

Amesema ameshuhudia yeye mwenyewe kwa macho yake katika vituo kadhaa katika jimbo lake ambapo kura halisi alizopata Magufuli zikibadirishwa na kuwekwa figure ambayo siyo halisi.

Amesema aliona kwa macho yake katika kituo kimoja Magufuli akipata kura 70 na Tundu Lissu kura 67 lakini za Magufuli ziliongezwa na kuwa nyingi zaidi ya hizo.
Na kwenye kituo kingine akasema Magufuli aliongezewa kura 150 ambazo siyo halali yake!

Selemani Bungala(Bwege) ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na kituo cha TV cha Kenya.

Kwa habari zaidi, msikilize ndugu Bwege hapa akihojiwa.

Attachments

  • VID-20201103-WA0000.mp4
    919.5 KB
Back
Top Bottom