SELCOM kwa miaka 6 wamehujumu mapato ya Serikali kwa kiwango kikubwa

LAZIMA NISEME

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
240
267
Naanza kwa kutoa pole kwa Rais Magufuli, mama Samia, waziri mkuu na watanzania wazalendo wapenda maendeleo katika taifa letu, Mh Rais wakati Ukipambana kwa dhati kuhakikisha tunalipa kodi na serikali ipate mapato na kutimiza miradi ya maendeleo na kuboresha huduma kwa wananchi, hivi karibuni nilikusikia ukilalamikia kampuni zinazotoa huduma za malipo ukiitaja wazi wazi MAXCOM ama Max malipo na wengine kuhujumu mapato serikali kwa kutumia ujanja wa kitaalamu pitapita yangu nimekutana na hii Nyingine SELCOM, Mkuu sikia hii

Selcom wireles ni kampuni inayomilikiwa na Sameer Hirji (Mhindi), hawa ndio walikuwa wauzaji wa luku toka Tarehe 29/3/2009, walikuwa wauzaji kwa 75% ya wateja wote wa TANESCO hadi serikali/ TANESCO ilipoipiga stop kutokana na kugoma kufunga mashine za EFD kama sheria ya kodi ya 2010 VAT EFD Reg. ilivyowataka wafanye Mh. Simba Chawene akamwagwa hapa jamvini "Kufungiwa SELCOM: Simbachawene amekurupuka? JamiiForums ilikuwa na taarifa kabla ya mwekezaji!
Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ex Spy, Apr 30, 2015.

Sakata la wizi wa kutisha linaanzia hapa, TANESCO katika kutimiza Sheria ya kodi ya 2010 ilitangaza tenda namba PA/001/13/HQ/NO29 kupata wauzaji wa LUKU na moja ya vigezo ilikuwa muuzaji afunge mfumo wa EFD ilikuweka uwazi wa mapato ya mauzo yake, Selcom na Maxcom walishinda tenda hiyo na barua za awali zilitolewa Tarehe 18/9/2014 ikiwa na mkataba kurudishwa siku 30, Taarifa za kiuchunguzi zilibainika Selcom walirudisha Tarehe 29/1/2015 na walisaini mkataba tarehe 6/2/2015 na kuanza kazi bila kutimiza kigezo cha kuwa na mashine za EFD wakiendela kukwepa kulipa kodi stahiki na udanganyifu wa aina hiyo, wakianzisha kesi kupinga kufunga mashine hizo dhidi ya TANESCO, nani alikuwa nyuma ya hili?

Tarehe 10/02/2015 TRA ilikamilisha uchunguzi wake na kubaini udanganyifu huo ikaiandikia TANESCO barua yenye kumbukumbu na 30-4/106-138-471/EFD, TRA ikiitaka TANESCO kuhakikisha Selcom wanafunga mashine hizo nchi nzima kwa mujibu wa sheria

Tarehe 17/2/2015 TANESCO wakapokea barua toka kwa TRA Namba 30-4/100-183-471/EFD ikieleza kuwa TRA wamewapiga faini ya milioni 3 tu na wamewapa muda wa nyongeza kwa siku 45 kuweka mfumo huo duuu...

Tarehe 25/3/2015 TRA iliwaandikia Selcom kuwa inawaongeza tena muda wa kufunga na kutumia EFD hadi Juni 30 2015 na nakala ikapelekwa TANESCO

TRA ikafanya uchunguzi na Tarehe 23/4/2015 wakaandika barua kwa SELCOM yenye kumb. 30-4/SLC-TAN/EFD ikitamka bayana kwamba barua zote mbili ya tarehe 17/2/2015 na 25/3/2015 za kuwaongezea muda wafanye biashara bila EFD ni za KUGHUSHI na hazikutoka ofisi za TRA ikumbukwe kwa muda wote huo Shamba la bibi bila huruma lilikuwa likivunwa Natetema kwa hasira nchi yangu hii

Tarehe 28/4/2015 TANESCO kwa hasira nyingi wakawasimamisha wahindi hawa kuuza LUKU huku baadhi ya watendaji wa TRA kusimamishwa kazi na kuhamishwa

Bila aibu wala woga Wahindi hawa waka mwandikia Simba Chawene barua Pepe

From: Sameer Hirji [Email protected]
Sent: April 30, 2015 8:13 PM
To: 'gsimbachawene@parliament.go.tz'
Cc: 'Users protected'
Subject: Unjustified Suspension of Selcom LUKU Vending Channel
Importance: High



Honorable Minister Simbachawene,

It is with great disappointment and regret that we have to furnish you with the attached correspondence with TANESCO and TRA in regards to our LUKU vending agreement with TANESCO. We have been severely victimized for something, that to begin with, is not a Selcom responsibility to TRA. The fiscalization of LUKU transaction, under the EFD VAT regulation of 2011, is the sole responsibility of TANESCO, the product owner, and not the aggregator. Our connection to the LUKU vending system was disconnection on Tuesday without notice, and we are yet to receive any formal correspondence from TANESCO on their course of action.

Selcom is the largest vendor of LUKU services all four mobile financial service operators, namely Vodacom M-pesa, Tigo Pesa, Airtel Money and Zantel EzyPesa, 35 banks through mobile banking and over 11,000 retail point of sales terminals countrywide. We account for 75% of all LUKU traffic countrywide – our performance cannot be questioned. If TANESCO was being fair, the same pressure for fiscalization would have been applied to other aggregators such as NMB and CRDB who continue to vend while not having their LUKU transactions fiscalized – their channels were not blocked nor have they been pressurized to comply.

We have all witnessed the chaos and inconvenience that our undue suspension is causing the entire country. We seek your intervention and support to assist us in your capacity, while clearing any misinformation that may have filtered through to you, which may have prompted you to issue the below statement.

=Hapa wakaweka screenshot ya thread iliyo JF=

We still await TANESCO to restore our connection for LUKU vending vide the further extension granted to us by TRA earlier today (attached).

Yours faithfully,
Sameer Hirji
Executive Director



Mh RAIS WANGU DR. MAGUFULI! haya ni maswali machache najiuliza
Kabla ya Tarehe 28/4/2015 kurudi Nyuma hadi 2009 uwiano wa kulipa kodi kwa SELCOM, je udanganyifu ilioufanya kwa miaka yote hiyo katika mfano wa huduma moja tu LUKU hizi nyingine je? Ni kiasi gani cha kodi walilipa kwa muda huo nilipo uliza TRA kila mmoja alisikitika nikajibiwa inasikitisha sana mkubwa ni kiduchu mno

Je mwekezaji hadi anaghushi barua za taasisi nyeti ya serikali, nidharau iliyoje kwa nchi yangu huyu jamaa yupo na siamini kama hakuna hatua za kisheria hazikuchukuliwa siamini mkuu siamini

Mtumishi mmoja wa TANESCO anasema hao wahindi ni miungu watu TANESCO walikuwa wakiuza LUKU kabla ya kulipia kama inavyotakiwa,"Mbona data zipo kaka....Hapo ICT wameshika barabara walisababisha jamaa mtaalamu wetu aliye wabana kulipa kodi kaondoshwa hapa meneja mkuu si ndio aliwaungaunga 2009 wamehakikisha amerudi kaka JPM amulike hii SELCOM na Wengine closer wakibanwa hawa walahi hakopi wala hata omba msaada kwa mtu aweke tu utaratibu kisheria wizi wa mapato ya serikali utapungua hapa ni jicho kwa jicho vinginevyo kaka hakuna kitu timu ni kubwa mno na inaanzia hukohuko unafikiri kwa nini wanajeuri na nguvuuu???" Niliguna kwa hasira nikaachana nae, Nchi yetu italiwa hivi hadi lini

KATIKA HILI MH RAIS LAZIMA NISEME NIKO PAMOJA NAWE KATIKA JUHUDI KULIPA KODI NA KUDAI LISITI, Naambatanisha Vielelezo
 

Attachments

  • IMG_2770.jpg
    IMG_2770.jpg
    139.1 KB · Views: 111
  • IMG_2802.jpg
    IMG_2802.jpg
    154.4 KB · Views: 107
  • IMG_2804.jpg
    IMG_2804.jpg
    179.6 KB · Views: 124
  • IMG_2807.jpg
    IMG_2807.jpg
    147.9 KB · Views: 129
  • IMG_2809.jpg
    IMG_2809.jpg
    150.9 KB · Views: 112
Yaani inaelekea ma aggregators hawa Selcom na MaxMalipo wana issues linapo kuja suala ukusanyaji mapato - inaelekea Mabenki ndiyo hayana udanganyifu.

Mi nafikiri kuna haja ya kampuni haya mawili kunyanganywa huduma za kuuza LUKU - wasiwe wanaziachia kampuni mbili tu ndiyo zihusike na uuzaji wa LUKU - ukaribu wao na management ya Tanesco unatia shaka sana.

Mh. Simbachawene anaweza kueleza kwa undani nini kilimshtua kuhusu nyenendo za Selcom, kuna kitu pale si bure na wenzetu hawa Wahindi wakisha weka baadhi ya Viongozi mifukoni wanafanya wapendalo bila ya kuchukuliwa hatua zozote - makampuni haya yanapata faida kubwa sana Serikali inapashwa kufatulia kwa karibu sana sana nyenendo zao wanafanya ujanja mwingi sana wa kuikosesha mapato Serikali.
 
Nchi yoyote ikiwa na ubaguzi kwa wengine kulipa kodi na wengine wadilipe basi hapo ukusanyaji wa kodi mara zote ni kidogo sana.Watakaolipa kodi lazima ni wale wenye mitaji kidogo na kodi kutoka kwa wafanyakazi.

Suala la kodi lisimamiwe kwa haki iwe ni tycoon au mfanyabiashara wa kati na yeyote anayelipwa mishahara au pato lolote kutoka kampuni au serikali.

Kuwaweka wabunge kutolipa kodi katika mishahara yao huku walimu,manesi na wengine wenye vipato vidogo wanahenyeka na mzigo wa kodi unakuwa ni UBAGUZI wa ulipaji kodi na unashawishi pia watu kukwepa kodi.
 
Nchi yoyote ikiwa na ubaguzi kwa wengine kulipa kodi na wengine wadilipe basi hapo ukusanyaji wa kodi mara zote ni kidogo sana.Watakaolipa kodi lazima ni wale wenye mitaji kidogo na kodi kutoka kwa wafanyakazi.

Suala la kodi lisimamiwe kwa haki iwe ni tycoon au mfanyabiashara wa kati na yeyote anayelipwa mishahara au pato lolote kutoka kampuni au serikali.

Kuwaweka wabunge kutolipa kodi katika mishahara yao huku walimu,manesi na wengine wenye vipato vidogo wanahenyeka na mzigo wa kodi unakuwa ni UBAGUZI wa ulipaji kodi na unashawishi pia watu kukwepa kodi.
well said
 
Huu ni ufataani usio na mashiko.

Hapa celcom hawana hatia wala hakuna wizi waufanyao. Wao wakusanyaji tu wa mapato ya Tanesco na si walipaji pesa. Wanazolipwa wanakusanya kutokana na ankara za TANESCO. Hawawezi kukusanya zaidi au pungufu ya ankara hizo.

Kuleta ji habari refu lenye lengo la ufataani haimaanishi ni ukweli.

Nnamashaka mleta mada ni jipu lililotumbuliwa kabla ya ujio wa mtumbuaji majipu na maumivu bado hayajapona.

Wasioweza kufikiri tu ndiyo wataona umeleta cha maana.
 
Wabunge wanalipwa fedha halali ambazo nafikiri utakuwa zaidi ya mil.1 lakini hazikatwi kodi.Wangekuwa mfano bora na wajisikie uchungu wa ulipaji kodi ili wasimamie vyema wengine walipe kodi na matumizi ya serikali pia eayasimamie ipasavyo.

Serikali imepokea hoja ya kuwa wanawasaidia wananchi kwenye majimbo yao,je hiyo ni moja ya shughuli zao za kibunge? Kuna wengine pia huwa wanakuwa mstari wa mbele sana kutoa misaada kwenye matatizo ya kijamii,je nao hawana haki ya kusamehewa kodi.

Uwe mfanyakazi mdogo,wa kati na mkubwa pia na wafanyabiashara vivyo hivyo,tulipe kodi kwa maendeleo ya nchi yetu bila kujali hali ya mtu maana huduma tunazitegemea wote.Na serikali iwaangalie hawa watu wa jamii ya ya Wahindi,ni wezi,wakwepa kodi na ni wadanganyifu sana.Wanafanya biashara sana huku wakificha fedha zao Canada na India huku wakiebdelea kuishi kwenye nyumba za NHC miaka nenda rudi maana wanajua wakishtukiwa wao ni kukimbia bila kupoteza mali nyingi.
 
Huu ni ufataani usio na mashiko.

Hapa Selcom hawana hatia wala hakuna wizi waufanyao. Wao wakusanyaji tu wa mapato ya Tanesco na si walipaji pesa. Wanazolipwa wanakusanya kutokana na ankara za TANESCO. Hawawezi kukusanya zaidi au pungufu ya ankara hizo.

Kuleta ji habari refu lenye lengo la ufataani haimaanishi ni ukweli.

Nnamashaka mleta mada ni jipu lililotumbuliwa kabla ya ujio wa mtumbuaji majipu na maumivu bado hayajapona.

Wasioweza kufikiri tu ndiyo wataona umeleta cha maana.
CELCOM imekuwa ikiuza umeme wa Sh. bilioni 1.0 hadi bilioni 2.0 kwa siku kwa wakati huo,kinacholalamikiwa ni kutotumia mashine za EFD wakati huo na kukwepa kulipa kodi stahiki inapokaribia mwisho wa mwezi mauzo hufika hadi Sh. bilioni 4.0 kwa siku.
 
Sasa Kama tumefika huku kwasababu ya wazee alafu umeapa kuwalinda nothing tena kipindi hichi ndiyo watapiga maana midomo ya watu imezibwa Na mamwela wameongezwa rupia..
 
CELCOM imekuwa ikiuza umeme wa Sh. bilioni 1.0 hadi bilioni 2.0 kwa siku kwa wakati huo,kinacholalamikiwa ni kutotumia mashine za EFD wakati huo na kukwepa kulipa kodi stahiki inapokaribia mwisho wa mwezi mauzo hufika hadi Sh. bilioni 4.0 kwa siku.

Wacha porojo na uongo.

CELCOM hata wauze billioni kumi kwa siku, ankara zao au za TANESCO?

CELCOM ni cashier tu, unaenda wewe kulipa kwao kabla hujatumia umeme kwa unafuu wako. Hawahusiki na pesa ngapi utalipa na ukilipa wao wanakupa ankara inayoainisha makato yote.

Wewe unamatatizo binafsi, ulitumbuliwa mapema.

Huna kesi hapa, ni ufataani tu.
 
Mama heri ya idd ? Mbona hatualikani

Wacha porojo na uongo.

CELCOM hata wauze billioni kumi kwa siku, ankara zao au za TANESCO?

CELCOM ni cashier tu, unaenda wewe kulipa kwao kabla hujatumia umeme kwa unafuu wako. Hawahusiki na pesa ngapi utalipa na ukilipa wao wanakupa ankara inayoainisha makato yote.

Wewe unamatatizo binafsi, ulitumbuliwa mapema.

Huna kesi hapa, ni ufataani tu.
 
Hakuna mhindi mwenye nia nzuri na nchi tuombe wahusika wachukue hatua za kisheria kuanzia TRA hadi CELCOM.
Kina mramba walikuwa wahindi leo mzee wngu kitillya mzee wngu chenge kule mama tibaijuka pale kati baba yngu iddy simba wameuza uda kwa Mil 200 tu walikuwa wahindi tatizo la Nchi yetu ni viongozi wa CCM na serikali yao imeshindwa kujari maisha ya watanzania wenzao japo sipendi kejeri na matamshi ya kukera toka kwa kijana wngu Trump mgombea urais wa marekani lkn ukweli utabaki ukweli tu japo unauma Afrika tunaitaji kutawaliwa tna maana tumeshindwa kujitawala
 
Back
Top Bottom