Selasini: Aliyekuwa mgombea Ubunge (via Kura ya maoni CCM), Stephen Morimi Magoiga kuwa Jaji ni sahihi?

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Naona aliyekuwa Mgombea Ubunge kupitia Kura ya maoni CCM na baadae akateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu Bwana Stephen Morimi Magoiga ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Kwa tafsiri pana ni kuwa kada wa CCM ameteuliwa kuwa Jaji.

Question everything, Doubt everyone? (Uhuru wa mahakama unazidi kuingiliwa. Sijui tunajenga Taifa la aina gani. Inasemekana hata ndugu wako ktk uteuzi huo kibao. Si wangeweza kupewa upendeleo wa namna nyingine tofauti na kupelekwa kwenye taasisi hii nyeti inayohitaji watumishi wake kutokuwa na egemeo upande wowote?)
 
Je,ana sifa za kuwa Jaji..Je kwenye uteuzi wake katiba imekiukwa?....
Tena nyie kina SELASINI tungewapa nchi mngejazaa UKOO MZIMA MAJAJI....kama ubunge viti maalumu tu UKABILA UMETAMALAKI....lakini wakifanya CCM nyie inawauma.....
Mimi mpaka infirnity naamini MAGUFULI kupitia teuzi zake ana nia njema kabsa na nchi hii...
HULKA YA BINADAMU yoyote ni kulinda maslahi yake na ndio maana MBOWE aliteua watu wake VITI MAALUMU kulinda mslahi yake ndani ya CHADEMA..so mjue MAGUFULI anafanya teuzi za watu ambao ni very ROYAL NA NCHI HII NA SI WASALITI
 
siyo kwa malaika mkuu aka jiwe
Tatizo lenu huwa mnachukulia kila jambo kisiasa
Umejichimbia wee kufukunyua kutafuta cv za wateule akaibuka na lalamishi dhaifu kama hili.
Kwanza Rais analetewa orodha kuna tume maalum inapitia sifa za majaji,ukikosa mwenye mapenzi na ccm utampata mwenye kupenda chadema,unataka wadau wasitimize haki zao za kuchaguliwa kisa huenda wakateuliwa kuwa majaji,Mwanahabari Huru atalalamika.
Una habari kwamba bosi wako Mbowe hajarudisha kadi yake ya ccm?
 
je hayo niliyosema yanauongo upi?
 
Mhimili wa mahakama unatakiwa kuishi "beyond suspicion" na mambo kama ya unasaba, udini, itikadi, na hata tuhuma za rushwa. Wanaomshauri mteuaji wanakosea sana. Mhimili ni wa kudumu lakini mteuzi anakuja na kupita. Wananchi wanapolalamika kuwa uhuru wa mahakama haupo, mara nyingi wanajenga hoja katika mazingira kama haya. Juzi juzi maaskofu wamesema

" Kubanwa na hatimaye kuelekea kupungua kwa uhuru wa Bunge, Mahakama, na Tume ya Uchaguzi. Hatua hii ni pamoja na kudhoofishwa kwa serikali za Mitaa."

Uteuzi wa jana umeacha maswali mengi sana.
 
Maskofu walikuwa sahihi kabisa
 
Back
Top Bottom