Mindi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2008
- 3,523
- 4,991
Bila shaka kama mkakati wa kuongeza mapato ya serikali, bila kujali athari kwa wafanyakazi, hasa wastaafu, serikali ya Rais Magufuli imekuja na "uboreshaji" wauchangiaji huduma za Afya kwa njia ya Bima.
Wafanyakazi wa serikali na mashirika yake, kwa mujibu wa sheria, hukatwa michango ya kuchangia bima toka mishahara yao kila mwezi. Utaratibu uliokuwepo ni kwamba kama mfanyakazi anachangia huduma hii kwa muda usiopungua miaka 10, basi mara anapostaafu, atapewa kadi ya bima ya mstaafu, yeye na mwenza wake. Yaani kama anayechangia ni mume, mke pia atapewa kadi. Hii itatumika miaka yote ya maisha yao.
Sasa Rais Magufuli, baada ya kupandisha viwango katika huduma mbalimbali, ikiwemo kupandisha kiwango cha makato ya mshahara kwa wafaidika wa mikopo ya elimu, amekuja na utaratibu mpya wa makato kwa wastaafu.
Katika Sekula mpya ya hivi karibuni, ili mstaafu aweze kufaidika na huduma za bima kwa wastaafu, anahitajika awe amechangia kwa miaka 15. Kwa hiyo, kama mtu anastaafu akiwa amechangia kwa miaka 10, basi atalazimika kutoa fedha taslimu kufidia miaka 5. Hapo atalazimika kulipa wastani wa sh. Milioni 7 mpaka 10, kutegemea na mwenendo wa uchangiaji wake.
Maana yake, mstaafu atalazimika kupigwa panga kwenye malipo yake ya fedha za mafao ili kugharimia viwango vipya vya michango.
Huu ni mwiba mpya kwa wastaafu.
Siyo vibaya kurekebisha viwango kama hivi. Tatizo ni kiasi kilichoongezeka. Angalau ongezeko la miaka 2 lingeeleweka. Hapo ni kuongeza mapato lakini pia kuzingatia maslahi ya wahanga wa ongezeko hilo. Hapa inaonekanavni mtu asiyejali watu, bali vitu