Kutokana na uhaba wa walimu uliokithiri katika maeneo mengi nchini kwetu haswa walimu wa hisabati na sayansi, nilikuwa naliomba bunge tukufu lije na sheria itayowafanya wahitimu wote wa vyuo bila kujali fani walizosomea kuripoti katika shule za serikali na kufundisha kwa miaka mitatu ili waweze kupata vibali vya kufanya kazi katika sekta walizosomea,hii italeta tija sana katika sekta ya elimu na kuleta matokeo chanya zaidi