Sekta ya Nishati bado inalo jukumu la kuhakikisha tunaendelea kuimarisha vyanzo vya nishati ili kutimiza lengo katika kuijenga Tanzania ya viwanda

ItsMi

Member
Sep 13, 2021
66
31
Nishati ni nguvu kazi ambayo inasaidia utendaji kazi wa nyenzo mbalimbali ikiwemo mashine za kukoboa na kusaga ambapo hutumia nishati ya umeme, vyombo vya usafirishaji ambapo hutumia mafuta na pia kuna vyanzo vya nishati hizo ikiwa ni pamoja na mwanga wa jua, mimea, makaa ya mawe, maji, upepo na vinginevyo

Tanzania ni nchi ambayo imeruhusu uwekezaji katika nyanja mbalimbali ikijumuisha maswala mbalimbali yanayolenga afya, kilimo, biashara, elimu, na na maswala mbalimbali ya teknolojia,

Lakini yote hayo ili yaendelee yanategemea sana uwepo wa nishati ambapo imekuwa na jukumu la kusambaza huduma zake maeneo mbalimbali

Kama tunavyojua kwamba nishati ni moja kati ya nguzo imara kwa taifa, hivyo kuna haja kubwa ya kuzipa kipaombele ili tuweze kuyafikia mafanikio tuliyojiwekea.

Sekta ya nishati inalo jukumu la kuimarisha njia za mawasiliano katika nyanja tofauti tofauti kwa sababu ili kurahisisha muda watu wamekuwa wakifanya shughuli zote kwa kutegemea mawasiliano yanayothibitiwa na uwepo wa nishati katika maeneo mbalimbali.

Pia kama tunavyojua viwanda vimekuwa mstari wa mbele katika kuongeza pato la taifa na kuleta maendeleo, Viwanda vikiwa vingi vitatusaidia kuzalisha bidhaa nyingi sana na kuziuza kwa wahitaji nje ya nchi na yote hii itaendelea kwa uwepo wa nishati.

Nishati pia itawezesha kuinua sekta binafsi na kuzipa ushirikiano katika utendaji kazi katika maswala mbalimbali yanayohusiana na nishati.

Kwa uwepo wa nishati bandari zitajengwa pia ilii kuweza kurahisisha huduma katika nyanja za kibiashara ili kuzidi kupanua wigo wa masoko na uzalishaji hatimaye kuinua uchumi wa nchi yetu.

Ni imani yetu kwamba hii sekta ya nishati itasaidia zaidi kuboresha shughuli za uchukuzi na mawasiliano, na kuwa chachu katika sekta mbalimbali katika kuleta mabadiliko zaidi na zaidi.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom