Sekta ya mitindo inavyojikwamua kwenye mnaso wa COVID-19

Yoyo Zhou

Member
Jun 16, 2020
71
110
Wakati janga jipya la virusi vya corona lilipoibuka duniani limesababisha kila kitukikwame. Ugonjwa huu umekuwa na atharikubwa katika karibu kila sekta, hasa biashara yamitindo ambayo ilikuwa inachukuliwa kuwaisiyo na ulazima sana, ambapo katika kipindi cha mlipuko ilikuwa ikifanya vizuri.

Wakati supermarket na masoko mengine yavyakula yakionekana kuwa na mahitaji makubwaya wanunuzi wa bidhaa, lakini soko la nguo nabiashara nyingine zinazohusiana na mambo yamitindo, limeporomoka na kusalia kufungwa.

Sekta ya mitindo imeathirika vibaya na janga hiliikishuhudiwa kuporomoka sana katika mauzoyake duniani, baada ya mahitaji ya nguo nabidhaa nyingine za mitindo kutopewa umuhimu.Jambo hili limepelekea biashara ya sekta hiikuwa miongoni mwa biashara ambazo zitahitajikichocheo cha uchumi ili kuzinyanyuakama Covid-19 itaondoka duniani.

Kutokana na kufutwa kwa shughuli kubwa kamavile maharusi, matukio maalumu, na mapumzikobaada ya amri ya kuwataka watu wakae ndani, watu wengi wamekuwa hawajali kuhusu kuvaasasa, bali wanachohitaji ni kula na kuwezakumudu gharama zao maisha. Kutokana na hili, wengine wanaona hakuna haja ya kununua nguompya, suala ambalo limeathiri mauzo kwawanamitindo wengi

Zuio lililowekwa katika nchi nyingi kutokana najanga hili pia limesababisha kufutwa kwamaonesho mengi ya mavazi na hata waandaajikushindwa kuandaa maonesho ambayo tayariyalikuwa yameshapangwa.

Wiki kadhaa za mitindo ya mavazi ikiwemomaonesho ya mitindo ya mavazi ya wanawakeya huko New York, London, Milan, na Parisyaligubikwa na gonjwa hili thakili la COVID-19,huku maambukizi ambayo wakati huoyalisambaa sana Italia, katika kipindi ambachomaonesho ndio yalikuwa yanataka kuanza,yalipeleka kufutwa kwa maonesho hayo.

Mlipuko huu unamaanisha kwamba wadau wasekta ya mitindo watashindwa kufikia malengoya mwaka huu ikiwemo kuhamasisha mamodona wabunifu wa mitindo. Bila ya kuwepo jukwaala kuonesha mitindo yao, sekta hii huendaikaporomoka wakati wowote ule kama halihaitatengemaa.

Lakini ifahamike kwamba wanamitindo huwahawafanyi maonesho yao kwa ajili ya kuoneshamitindo ya nguo tu, bali wanafanya kwaajili yakuuza pia, kwani tunafahamu ya kwambabiashara itangazwayo ndiyo itokayo. Ni vigumukujenga chapa bila ya kupata faida kubwakwenye mauzo.

Ndio maana kuna msemousemao Mungu hukupa kilema na mwendo. Wanamitindo wengi hivi sasa wamegunduakuwa katika msimu huu pia wanaweza kuuzabila ya kukutana uso kwa uso. Badala yakewanatumia majukwaa ya kidijitali kuuza bidhaazao.

Ingawa inatia mashaka hasa kwa watejawanaopenda kuona, kugusa na kuzihisi bidhaawanazonunua, lakini wauzaji wa jumla wabidhaa za mitindo bila shaka watakuwawameshafikiria jinsi ya kutatua hilo katikamsimu ujao.

Mbali na hapo wanamitindo haohao wameamuakubuni barakoa sasa za mitindo ya ainambalimbali. Viwanda vingi vinaruhusiwakutengeneza barakoa ili kulinda afya za watu. Hii imekuwa ni fursa kwa wadau wa mitindokupata njia nyingine ya ajira. Barakoa imekuwabidhaa muhimu kwa watu wengi, ambapo wengiwao kama sio wote wanatafuta barakoazilizotengezwa katika nchi zao.

Barakoa pia umekuwa mwelekeo wa mitindo katika kipindicha corona, kifaa ambacho kilianza kama cha kujikinga tu na sasa kubadilika kuwa fasheni,ambapo wabunifu wa mitindo sasa wanatoachapa mbalimbali za barakoa.
 
Back
Top Bottom